BAADHI ya wananchi wa Jimbo la Igalula ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametoa malalamiko kwa mwenyekiti wa chama hicho taifa kuhusu uongozi mbaya wa mbunge wao. Jimbo la Igalula linaongozwa na Tatu Musa Ntimizi.
Katika barua yao kwenda kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, wananchi hao wanasema hawataki kumwona mbunge huyo akiendelea kuliongoza jimbo hilo. Jimbo la Igalula lilianzishwa rasmi mwaka 1995 baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Tabora Kaskazini.
Baadhi ya tuhuma dhidi ya Ntimizi ni kwamba amekuwa akitumia nafasi yake ya uongozi kumlazimisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tabora Vijijini kumpatia mwanaye Musa Ntimizi kazi za ukandarasi wa majengo na madaraja.
Inadaiwa kuwa Musa hana taaluma wala sifa za ukandarasi, isitoshe hata kampuni ya ukandarasi hana.
Kwa mfano alipewa ukandarasi kujenga zahanati katika vijiji vya Imalakaseko, Igalula na Goweko pamoja na daraja la barabara ya Kigwa hadi Itundaukulu. Kibaya zaidi, baadhi ya watu aliokuwa anawapatia vibarua, hajawalipa fedha zao walizokubaliana hadi sasa, inasema sehemu ya barua hiyo.
Wadai wa Mussa wametajwa kuwa ni pamoja na Ashura Mfaume na Ashura Selemani wanaodai Sh 35,000, ambao walipewa kazi ya kuponda kokoto zilizotumika kujenga Zahanati ya Goweko. Wengine ni Kajuna Daudi na Michael Malambo wanaodai Sh 84,000 kwa kazi ya kusomba mchanga na kufyatua matofali.
Shule ya Sekondari Goweko inadaiwa kumdai pia Sh 405,000. Majengo ya Zahanati za Imalakaseko na Goweko bado hayajakamilika kujengwa hadi sasa, ingawa tayari ameshalipwa fedha kabla ya kumaliza kazi, inasema barua hiyo.
Lakini pia, Mbunge Ntimizi anadaiwa kuwanyanyasa wananchi katika masuala mbalimbali ya kijamii. Kwa mfano, inadaiwa Machi 25 mwaka huu, mbunge huyo alizuia basi lililokuwa limewabeba wana-CCM kuelekea Goweko kwa ajili ya sherehe za kuwasimika makamanda wa UVCCM Wilaya ya Uyui.
Wananchi hao wanasema: Mbunge Ntimizi, kwa kutumia madaraka yake, aliwaamuru polisi wa Tabora Mjini kumzuia mmiliki wa basi la NBS lililokuwa limekodiwa na CCM Wilaya kuwapeleka makamanda na viongozi wa CCM kuhudhuria sherehe hizo. Gari hilo lilizuiwa tangu saa mbili asubuhi hadi saa tisa alasiri liliporuhusiwa.
Aidha, Mbunge Ntimizi anadaiwa kukopa Sh milioni 40 kutoka Mfuko wa Pembejeo kwa kutumia jina la mtoto wake, Saidi Rashidi Omari.
Hata hivyo, pembejeo hazikupelekwa Jimbo la Igalula na hivyo kuulazimu Mfuko wa Pembejeo Taifa kumshitaki mbunge huyo. Kesi hiyo namba Na. 19 ya mwaka 2006 iko Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, wadaiwa ni Saidi Rashidi Omari na Tatu Ntimizi mwenyewe.
Inadaiwa pia kwamba mbunge Ntimizi amekuwa akivitumia vyombo vya dola kwa maslahi yake ili kuwasumbua wananchi ambao wamekuwa wakitangaza nia zao za kugombea ubunge wa jimbo hilo.
Baadhi ya wanachama wa CCM walioshitakiwa na Ntimizi kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa, ni pamoja na Hanifa Tambulu, Athumani Rashid Mfutakamba, Katibu wa CCM (Uchumi), Suma Mamloo, Katibu wa CCM (W) Uenezi, Kapalu na Mwenyekiti wa CCM (W), Kazwika.
Kuna madai kuwa Tatu Ntimizi amekuwa akitoa fedha za kiasi cha Sh 2,000 kwa wajumbe wa nyumba 10, makatibu wa CCM wa matawi Sh 5,000 na makatibu wa kata Sh 10,000 kwa kumtumia Katibu wa Mbunge, Johnson Banda.
Baadhi ya wanachama wanaomlalamikia Ntimizi na namba zao za kadi za CCM katika mabano ni Miraji Mwalau (9999211), Shami Tandiko (35648), Idd Mlenge (1747271), Said Sumuni (594754), Shabani Mayega (35362) na Joha Hussein (862969). Wengine ni Salima Mbogo (432740), Hamisi Sukwa (35302), Issa Mtiliga (35304), Zainabu Hassan na Hadija Ramadhani (35303).