Kama wewe ni Mtanzania na ulifahamu kuwa hizo ni ofisi za Tanzania na waliopo ni Watzania wenzako, kwa nini hukuongea nao Kiswahili? Yaani ukaowaona lugha ya mkoloni ndio ya kuongea na wenzio, halafu ulienda kumwona nani na kwa shida gani ambayo walishindwa kukutatulia? Ningesikitika kama ulienda ukiwa na shida fulani kama labda ulikuwa umeibiwa wakashindwa kukusaidia. Sasa wewe watu wako kazini, halafu wewe unaingia. Kumbuka ulipaswa kuwasilaina nao kwa barua pepe kuambia kuwa utaenda ili wajianda na kutafuta majibu ya maswali yako.