Umewahi kusikia vioja vya VIBAKA-supported by picture

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Kwa ruhusa ya mwana JF mwenzetu KAKA JAMBAZI, natumia avatar yake ili tujadili vituko vya VIBAKA kwenye miji mikubwa EA hasa DSM.

Juzi juzi nilikuwa maeneo ya CENTRAL police niliona mtu mmmoja mfupi anakimbia mbio sana na akaingia moja kwa moja hadi ofisini kwa askari na kujifungia na kupiga kelele tafadhali nifungeni mimi ni mwizi wakati tunashangaa pale gafla likatokea kundi kubwa la watu na mapanga na mawe wakiomba ndugu yao kichaa wakamtibu yeye akasisitiza mimi ni mwizi jamani sio kichaa nimeiba simu na akaitoa ile simu ya blackberry.

Je wewe umeona kisa gani kingine cha kuchekesha na kuhuzunisha kutoka kwa hawa VIBAKA NA machokoraa?

mail
 
Ha ha haaa!! Kwa kweli hii ni kali. So funny!

Kusema kweli VIBAKA saa nyingine wanachekesha sana. Yule aliwaambia police msiwasikilize tangu kariakoo mpaka hapa hawaongei neno, hawasemi mkamate au muue huyo mwizi nikajua wanataka kuniiua ndio nikaja hapa
 
hiyo issue haikutokea central police kama unavyosema, ilitokea njombe, story told by radio one month or two ago katika kipindi cha mambo mseto.
 
Lumbe. Nimesema supported by picture so hilo swala la huko unakotaja sijalisikia. Na hio picha nimeichukua kwa Member humu JF na haisiani na thread ila inaendana nayo
 
Hii stori mbona ipo tu!!
ila ukiisikia mara ya kwanza inachekesha sana.
 
Kwa mtazamo wangu si vioja bali ni uchaguzi kati ya kufa na kufungwa. Huyo kibaka aliona kuwa adhabu nyepesi kwake ni kufungwa na polisi, kinyume na hapo lazima auwawe na 'wananchi wenye hasira kali'.
 
hiyo issue haikutokea central police kama unavyosema, ilitokea njombe, story told by radio one month or two ago katika kipindi cha mambo mseto.

Wewe elezea kama una kihoja cha vibaka wacha kukandia watu ovyo, kama ulikuwa unajua imetokea Njombe mbona hukuoleta mpaka mwenzio azungumzie? Mimi sina kihoja
 
Hii stori mbona ipo tu!!
ila ukiisikia mara ya kwanza inachekesha sana.

Issue ni kuwa una jipya? una nyingine ya namna hio? :confused2:

Wewe elezea kama una kihoja cha vibaka wacha kukandia watu ovyo, kama ulikuwa unajua imetokea Njombe mbona hukuoleta mpaka mwenzio azungumzie? Mimi sina kihoja

Asante kwa kuelewesha hii mtu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom