Umewahi kujutia kwanini umeoa au kuolewa?

Its a long story for me...maana imeshawahi kunitokea na kwa kweli tulikuwa tunapendana sana. the story is from my ex-girl friend ambaye alikuwa anasoma shule moja huko kusini mwa TZ. Siku moja wakati yuko shule (chuo) alinidanganya kuwa yuko shule, kumbe walikuwa wamefunga likizo fupi, na yeye alikuwa ametoka out somewhere na jamaa mwingine... nilipiga simu mara kadhaa hakupokei, mwishoe alipokea...nikamuuliza uko wapi? akasema shule..... Nikamwomba kuongea na rafiki yake mmoja (nikamtaja jina), akasema hayupo....nikataja mwingine...akasema hayupo. then nikamuuliza uko na nani..akakaa kimya kidogo..then akakata simu..na hakupatiakana tena hewani... baadae nikawapigia marafiki zake kwa nyakati tofauti tofauti kumuuliza yuko wapi, wakanipa majibu tofauti kila mmoja. Nilihisi kitu tofauti hapo, yaani nilijisikia vibaya mno.. Likizo ndefu ilipofika, walifunga na alirudi Dar...then nikamuuliza siku ile ulikuwa na nani...akaniambia alikuwa shule.
Hapo nyumbani alibadilika kidogo, simu yake alikuwa hataki ikae mbali nae..kila alipo, sim ameishika..akiwa anapika, anafua, anaosha vyombo mpaka hata bafuni anaenda nayo...wakati haikuwa kawaida yake. Siku moja wakati narudi kazini..alikuwa anaongea na simu sebuleni na hakujua kama mimi nakuja, maana siku hiyo niliwahi kidoggo kurudi. Nilipofika karibu na mlango nikasikia mtu anaongea na simu, nikasikiliza kwa muda kidogo kama dk 3 yale maongezi walivyokuwa wanaongea,,(yalikuwa ni maongezi ya kimaapenzi na mahaba mazito....mengine siwezi sema maana yananiuma mpaka hivi leo, maaana hata mimi nilikuwa naongelewa kama si chochote) then nikaingia ndani moja kwa moja mpaka chumbani kana kwamba sijamuona... alishangaa sana kuona nimerudi. Ghafla alikata simu na kufuta kabisa receiving calls zote na msg zote. Usiku nikamwomba simu yake...akataa. Nikaichukua kwa nguvu na tukagombana sana usiku ule.....nikaiangalia missed call. sms zote alikuwa amefuta... Ila asubuhi simu yake nikaenda nayo kazini...missed call na msg ziliingia toka kwa huyo mshikaji wake.
Yaani niliumia sana.....ngoja niishie hapo maana kasheshe yako hapo home mbona alinielewa mimi ni nani......maana nilikuwa nimampenda sana na hata ada ya chuo nilikuwa ninamlipia...... Kitu kingine kibaya hata wazazi wake walikuwa wananijua kuwa mim ni mchumba wa mtoto wao.. ILINIUMA SANA SANA........... Hapo ndo end of everything....tangu hapo nikaanza kujua kuwa wanawake ni waficha siri sana..

Utu uzima dawa mkuu..pole!
 
- Mara nyingi huwa na-regret na Mara nyingi huwa nafurahia maisha ya ndoa!

- Ndoa haiwezi ku-last forever!

- Nimejaribiwa mara nyingi sana ku-do nje ya mahusiano ya ndoa na mara chache huwa na-do!
 
jibu zuri utalipata kwa wanandoa waliotimiza miaka 15-20 ya ndoa
 
Firstlady swali lako limenikuna. Yani nimeJUTA sana kuolewa na furaha yangu ya mwaka huu ni kuhakikisha talaka imekamilika. Bwana kila siku wanawake mpaka kulala nao chumbani kwetu nilipokuwa safari halafu alinisema na kunitukana kwa hao wanawake kama siyo kudhalilika ni nini. siku zingine alinipiga na kunidharau sana na hapa nilipo naomba kudra za mwenyezi mungu niweze kumsamehe mana ninavyomchukia kama vile hakuwa mume wangu. miaka 4 ya ndoa yangu ni kama nilikuwa kwenye shimo la moto na ilikuwa ni uamuzi mgumu kuachana ila ilibidi hakika sasahivi nina amani na bila yeye maisha yangu yanaendelea ilimradi nilivyozaliwa sikujua nitakutana nae. mwanaume huyu mpuuzi kanipotezea ladha ya mapenzi kabisa kwa ubabe,dharau,ukorofi na umalaya wake.

Miss Pirate
Am so sorry for what happened to your marriage. Your post is so very touchy masikini. Pole sana

However reading your post, I have something to tell you mydia.

Unapogombana au kufarakana na mwenzi wako (hasa yule ambae mmefunga ndoa halali either bomani, msikitini au kanisani) si vizuri sana kurushiana naneno ya kashfa na kutoleana matusi. Avoid kum-call names kama hizo mpumbavu, mpuuzi, mjinga n.k. Hii si nzuri kwa afya yako mwenyewe kwani inakujengea chuki and when ukiwa na chuki you always frown uso wako na moyo mwishoni unajikuta unazeeka- Try not to be frustrated by his/her actions ambazo zimekupa hasira. Ishi kwa furaha no matter what.

Pili si vizuri kuanika siri, maovu yake hadharani hasa kwa watu wanaowafahamu isipokuwa tu kama mko kwenye mahakama ambako utatakiwa kuongelea makosa hayo na ushahidi -au hata hapa JF kwa kuwa hatufahamiani) Sababu ni kuwa inawezekana ikajafika wakati hasira zenu zimepoa au amejirekebisha na akaja kukubembeleza (Knowing jinsi unavyompenda) utajikuta unaaibika kwa wale ulokuwa unawasimulia mabo ya mwenzi wako.

FL1---- Kwa hii mada, sina cha kucomment tafadhali and I know you know why...but what I can advice ni kuwa if that person is your hubby/wifey halali basi muweke katika maombi ukiombea yale yote akutendeayo ambayo yanakufanya u-regret but otherwise try as much as U can to rebuke hizo feelings za ku-regret.... always have positive attitude.

Marriage are meant to last forever..... ni sisi tu binadamu na tamaa zetu na mioyo yetu migumu ........try to learn to understand your man/woman na kuyachukulia mapungufu yake kama changamoto ya maisha na buni njia ya kuyapa accomodation katika maisha yako. tafuta njia mbadala zitakazokufanya uyastahimili bila kusaha kumweka katika maombi yeye na ndoa yenu kwa ujumla.
 
Mkishaachana nijulishe niangalie namna ya kukusaidia !
 
very powerful msg dia, thanks.
 
Yap ilishawahi kuniokea na Ku-regret kwanini nimeingia kwenye Mahusiano na yule BINTI!!!
Its a Long Story but Binti alikuwa hataki hata kusikia naongea na SAUTI ya KIKE,
Anataka kuni MONITOR kila ki2,anaweza kupokea simu akisikia sauti ya KIKE 2
basi haulizi kinachofuata ni MATUSI hata akiwa ni DADA yangu as long as haijadisplay JINA!!!
Pole sana sana, msamehe tu, kaa nae umuelimishe labda ni utoto wa kimapenzi
 
Poleni sana all the ladies mliojeruhiwa kwenye ndoa zenu,
Msichoke kuwaombea wenzi wenu, jamani mambo ya ndoa yanataka moyo haswa.

Ninamshukuru Mungu wangu kwa kila siku inayoitwa leo kwa kunipatia wewe mpenzi mume wangu, kweli sijajuta na kila siku kwangu ni mpya ( miaka 10)
I don't know what the God has in store for me, but I leave all to the all knowing God.

Ushauri ni maombi na kuhakikisha hamlali mkiwa na bifu ambayo haijawa sorted out, pia communication
Mbarikiwe
Mhandisi Nsiande ( mama 3 )
 
Mimi ninajuta sana ni bora nisingejiingiza katika ndoa kwani ni kero kila siku. Naona bora kutembea na wauza bar kuliko mke wangu. Na mwaka huu hautaisha lazima nabwaga manyanga kudadadeki.
 
Men have power to do anything to women because we give it to them.
The power of a man wouldn't mean anything without a woman.
When times are hard btn you and your man remember that he can only do what you allow
 
Kujutia muhimu katika mapenzi unaoa au kuolewa pale usipo tarajia
 
Mimi ninajuta sana ni bora nisingejiingiza katika ndoa kwani ni kero kila siku. Naona bora kutembea na wauza bar kuliko mke wangu. Na mwaka huu hautaisha lazima nabwaga manyanga kudadadeki.

Dah naona umeongea kwa hasira sana pole omba mungu akupe hekima na maarifa usivunje ndoa
 
Kujutia muhimu katika mapenzi unaoa au kuolewa pale usipo tarajia

Mchwechwele nimependa avatar yako sana maisha bora kwa kila mtanzania
avatar34775_1.gif
 
Back
Top Bottom