Umewahi kujiuliza hili?

Raha ni nini basi? Je ni vile tunajisikia milango yetu ya fahamu inaposisimuliwa? harufu nzuri, utamu wa kitu, sauti nzuri, mguso mzuri, mwonekano mzuri n.k Kwamba milango yetu ikipata maximum stimulatioon basi tunasikia raha? Au raha ni zaidi ya hisia za milango ya fahamu na ni kitu kinachozama ndani ya mtu mwenyewe bila kutegemea sana kusisimuliwa kwa milango ya fahamu?

Kwa mfano, daktari ambaye anamesoma sana na kufanya kazi ya kuokoa watu, kila anapofanikiwa kuokoa maisha ya mtu anajisikia "raha" na anasikia kujitolesheleza kwa namna fulani je huyo naye anapata 'raha'? Yawezekana kumbe kuwa raha ni zaidi ya hisia zitokanazo na vionjo na milango ya fahamu bali ni kitu ambacho chaweza kutokana kabisa na aina ya maisha ya mtu anayochagua na yakamtosheleza?

Kwamba msomi aliyesoma sana na anatumia elimu yake vizuri na anajisikia 'satisfaction" lakini hana muda wa kwenda kwenye madisco, kudate, au kufurahia yale ambayo yanasisimua vionjo yawezekana kwamba naye ana enjoy maisha kwa namna yake?

Ninaamini kufurahia maisha ni zaidi ya kufurahisha vionjo; kufurahia maisha ni zaidi ya kusisimua milango ya fahamu. KUfurahia maisha ni pamoja na kutumia elimu, mang'amuzi na uzoefu mbalimbali katika maisha kuweza kujiletea furaha inayotosheleza mtu. KUfurahia maisha ni kupata ufahamu kuwa kile unachokifanya ni bora kwako, hakidhuru mtu mwingine na ukiambiwa urudie tena utarudia kwa furaha. Nafikiri kwa mtu mzima furaha au starehe ni zaidi ya zile za utoto ambazo bado ni za kusisimua vionjo.
 
Raha ni nini basi? Nafikiri kwa mtu mzima furaha au starehe ni zaidi ya zile za utoto ambazo bado ni za kusisimua vionjo.

Hili neno limenigusa!
Kuna watu wasiokuwa na hilo na kuingia kufurahia raha za kiutu uzima zenye kuhusisha wengine zaidi ya mhusika.Raha za kitoto ni za kibinafsi zaidi.
 
Kama binadamu wote ni sawa, kwa nini basi kuwe na wengine waonwao au wajionao kuwa ni wa muhimu zaidi (VIP)?

Kama wote tunapumua hewa hiyo hiyo kwa nini wengine wawe wa muhimu zaidi kuliko wengine? Wote tunaenda haja kubwa na ndogo, wote tuna hisia za aina mbalimbali, wote tutaishia kwenye mauti n.k.

Sasa kwa nini tujiwekee haya makundi wakati tukiwa hai? Faida yake haswa ni nini?
 
wat kind of raha do u like eeh?ni kama ivyo umekaa kwenye komputa na kuandika kama ivyo ndiyo raha zenyewe au we unataka upae kama ndege ndiyo uamini kuna raha duniani na kama haujaona bac fanya ivyo sa izi uone raha nyingine
 
Back
Top Bottom