Umeumizwa moyo mara ngapi mapenzini?

Nashukuru kwa ushauri Bishanga, huwezi amini huwa natamani hii hali iondoke kwangu ila imeshindikana, iliniathiri kwa kiwango kikubwa sana ndugu yangu, siku nilipogundua huo usaliti Faham zilinipotea kama dk 15, baada ya kuzinduka vikabaki vilio na majuto ya kumwamini mwanadamu kama mimi. Ila nilichojifunza mpaka sasa ni kwamba sintokaa nimwamini mwanaume yeyote mpaka siku naingia kaburini. Nilipatwa na mkasa wa karne ya sayansi na teknolojia! Sijui kama kuna siku ntasahau kabisa.
Pole sana SL kwa yaliyokukuta lakini miaka mitatu ya kilio na kusaga meno kusema ukweli thats too much hasa ukizingatia kuwa mwenzio anakula nchi na huyo aliyesababisha uumie. Ya nini bana binadamu aliyezaliwa na mwanamke kama wewe akutese kiasi hicho.Jitahidi tu nafasi ikitokea jenga imani na mtu mwingine na kisha usonge mbele.
 
Nimeumizwa mara 1! Sijasahau mpaka leo huu mwaka wa 3. Nikikumbuka naanza kulia upya kama vile ndo tukio la jana yake. Nimejitahidi kusahau nimeshindwa!

Pole sana dada, saa zingine ukiwaza sana unaweza kuanza kuua jinsia husika..
 
Nashukuru kwa ushauri Bishanga, huwezi amini huwa natamani hii hali iondoke kwangu ila imeshindikana, iliniathiri kwa kiwango kikubwa sana ndugu yangu, siku nilipogundua huo usaliti Faham zilinipotea kama dk 15, baada ya kuzinduka vikabaki vilio na majuto ya kumwamini mwanadamu kama mimi. Ila nilichojifunza mpaka sasa ni kwamba sintokaa nimwamini mwanaume yeyote mpaka siku naingia kaburini. Nilipatwa na mkasa wa karne ya sayansi na teknolojia! Sijui kama kuna siku ntasahau kabisa.
Labda mimi tu.
 
Ndugu yangu BAK utatofautishaje mapenzi ya 'kweli' na 'yaliyojaa usanii'?

Si rahisi kutofautisha hasa pale penzi linapokuwa changa lakini kadri siku zinavyosonga mbele utaanza kuyaona mambo anayokufanyia mwenzio ambayo hayaonyeshi upendo wa dhati na hata uaminifu na mengi mengineyo yanayohusiana na mapenzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom