Umeshawahi kuusikia huu wimbo?angalia tafadhali huyu jamaa sijui aliwaza nini?

charger

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
2,320
1,369
Habari wana jamvi,hope wkend inakwenda fresh.

Mimi sio mpenzi wa bongo flava kivile ila kuna wimbo nimeusia "NILIPE NISEPE" kwakweli huyu dogo amejitahidi kuwakilisha one of tabia za watu ambazo binafsi sizipendi!!

Unajua unaweza ukawa na ndugu,rafiki au jamaa,jirani mnaheshimiana vizuri tu ikatokea amepata shida akaja kwako mikono nyuma na maneno mazuri kuomba umsaidie fedha(umkopeshe).Tunajua wote hakuna fedha isiyokuwa na kazi lakini kutokana na maelezo utakayo yapata toka kwa huyo mkopaji unaweza ukaona umuhimu washida yake ukadiriki hata kuahirisha mipango yako flani kwa ajili ya kuokoa jahazi lake.Mnakubaliana vizuri atakulipa ndani ya muda flani ili nawewe usikwame.Shughuli inakuja muda mliokubaliana unafika mtu haonekani,simu hapokei au anapokea ukitaja tu hela anajifanya hakusikii,anabadilisha njia,anabadilisha kijiwe kifupi ni kwamba anakukwepa na ujajikuta umeingia kwenye matatizo kwa ajili ya huruma yako.

Umeshawahi kukumbwa na hili?
 
kuna mwingine unampigia anakwambia hela yenyewe kidogo lakini wanisumbua utafikiri milion je ingekuwa milion ungedai vipi maneno kama hayo unapata kichefuchefu..................... hiyo ipo sana ndipo undugu/urafiki unakwisha............. itafika mahali hakuna kusaidiana hata ukiwa na hitaji la namna gani................. heri uamue kusaidia kuliko kukopesha........ heri lawama kuliko fedheha

 
Huyu Belle9 kajitahidi sana aisee, kuna stori ya Baba mkwe na mkwe wake nilíileta humu jamvini nikawambia Baba mkwe alizuia mazishi ya mwili wa binti yake marehemu (mke wa mkwe, ambaye ni mwalimu) mpaka atakapolipwa mahali yake yote iliyobaki. Kweli Nilipe nisepe!
 
kiukweli hilo lipo,mimi kuna jamaa wa dar,alikuja kunitafta mjini.ofisin kwa ndugu yangu akanikosa,cm hana akamuomba bro wangu cm akanipgia nikamwambia nakuja mda sio mrefu.nikaenda önana ne,tukasalimiana vizur akaanza kunielezea shida yake, akatoa na dawa za antibiotics akanambia anaumwa sana choo kigumu,na madawa anayotumia yanaitaji kula sana,kwel jamaa dom mgen na wazaz wake wapo dar,na nimwanachuo mwenzangu,basi nikampa pesa ilikua jumapili,makubaliano jumatano atakua ameshapata na atanilipa,yani ndo mwanzo wa uadui na mwanachuo mwenzangu yani mpaka leo hajanilipa,na hata urafiki haupo tena.
Note.kumkopesha mtu ni kuua mahusiano yenu.
 
Hii inaboa sana, mie sipendi kweli kukopeshwa na kukopa ila katika maisha yetu haya lazima utajikuta unakopa au kukopeshwa tu
 
mwingine anakulipa kidogo kidogo kiasi kwamba baadaye unaona aibu kumdai maana anakulipa nusu nusu tu.
 
Back
Top Bottom