Umeshaisikiliza 'Shika adabu yako' ya Ney wa Mitego?

Hivi Shetta si alikuwa anajitapa 'shikorobo' imemuingizia mpunga mnene, inakuwaje anashinda kwa Diamond na kuhongwa magari?
 
Hii ngoma ikosawa lakn yule mwingine ambae anagari analala kwa mademu sijajua nani nijuzeni kwenye iyo ngoma ya ney
 
Ngoja niisakue make kwa mtazamo inakosha sana, jamaa anajiamini sana.
Safi sanaaaaa
 
Hahaahah, hizi ndio nyimbo nazo zipenda kwa NEY... jamani tuache fake life... hizi, ndio maana mimi insta nili amua kukaa pembeni nione maigizo.... nime kua mtu waku like na ku comment baasi, baada yaku safisha account yangu iliyo kua na pices kama 300 na ushee si kidogo... INSTAGRAM ime wafanya vijana wengi wa bweteke na kuhisi mbona kama mimi ndio niko slow mambo yangu haya ninyookei????? Hell no kuna fake lifestyle mle balaaa... ndio hayo sasa NEY ka aamu kuwanyea!!!!
 
Sikuona umuhimu wa kuimba tungo hii hasa kwa mtu aliyetoka kama Ney!
Hawa watoto wa "Tandale" smts inabidi wajitambue...
 
Acha kumdhalilisha Eminem wewe

Thank you.
Kuna watu wanajua kuropoka balaa.

Kwa mfatiliaji mzuri wa mziki wa mbele huyu Ney anajitahidi kutumia/kuiga marketing strategy ya 50 Cent. Atafanikiwa kwa kiasi flan ila....

Ni upepo tu, atapita.
 
Baba kailaaa hahaha" Nay Sio mtu mzuri ila nilkua najiulizaga sana shetta anapata wap jeuri ya kununua ndinga kali sahv anaendesha Discovery 4 sijui 6 ile kumbe Chief Kiumbe anasmamia show
 
Huyu mtu kupenda wasuta wenzie hajambo sema alikolulia (manzese)ndio waishivyo
Hao bongo movie wengi wao hajieleewi na shule hawataki kurudi si zasanaa au nyingnezo sijui hawaoni upepo unaokuja mbele uko
 
THE TRUE BOY IS IN THE BUILDING!

Wimbo mpya wa Mipasho (Diss track) kutoka kwa msanii 'mtata', Ney wa Mitego umesikika Live kwa mara ya kwanza kupitia kipindi cha XXL.

Katika wimbo huo uitwao 'Shika Adabu Yako', Ney amewaumbua kwa kuwataja majina wasanii na watu maarufu nchini akianika ubovu wa matendo yao na kuwataka wabadilike.

Kuonyesha anajua anachokifanya, msanii huyu anayejiamini kupitiliza, ametamka wazi ndani ya wimbo huo kuwa hatishwi na chochote na kuwataka wenye ubavu waende kushitaki kokote kwani yeye hana cha kuhofia.

Itakumbukwa kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Ney aliandika baadhi ya mashairi ya wimbo huo na kusema kuwa huu wimbo ni wa kusikiliza getto kwani akiutoa patachimbika!

Hata hivyo, pengine kutokana na athari za mikwara ya hapa na pale kutoka kwa wasanii haswa wa Bongo Movie waliosoma mashairi hayo kutaka kumpeleka mahakamani kwa madai ya kudhalilishwa, Ney ameamua kuupeleka hewani na kutoa picha huenda ameona kama Mbwai iwe Mbwai tu!

Miongoni mwa vijembe vinavyopatikana kwenye wimbo huo ni;

Msanii Ray kujifanya Mkongo kwa kununulia mkorogo fedha zinazotokana na mauzo ya movie zake na kuishi kwao hadi sasa, Bongo Movie imekufa kufikia hatua wasanii wa kike wa filamu kutaka kuimba km snura na shilole, Niva kuishi kwa mademu na huku akimiliki gari ya M10 wakati hana getto, wanafunzi wa chuo kuishi maisha ya anasa na kupoteza dhana ya usomi. Wadada wengi wa mjini na kutovaa chup**, biashara?

Hakuishia hapo, alihamia kwa BASATA, kwa kuwashangaa wanavyoshindwa kufanya kazi yao kwa weledi na kuishia kuwafungia wasanii nyimbo bila kujua ugumu wanaopitia..

Pia, akaendelea na wadananda kwa kumtaja Shetta kuwa anaringishia gari ya kifahari aliyohongwa na Chief Kiumbe kwa kujitapa 'My new ride', Ommy Dimpoz kuhusishwa na Ushoga kitaani, DJ Choka kuwa bize na bata bila kujali familia huku hana hata godoro la kulalia.

Mimba ya Wema Sepetu ni ya kweli au kiki za msimu? Na anamshauri aangalie umri unaenda asiendekeze kiki kwani mwishowe ataitafuta Kiki hadi kwa FID Q.

Serikali ya Magufuli nayo haikuachwa...

Nimechoka kuandika. Itafuteni muisikilize.

Asanteni wadau..
Mbona ameacha ya kwake na mama watoto wake Curtis kuambiwa mtoto si wake
 
Back
Top Bottom