Umesha wahi kufikiria...Labda M-pesa ya inaweza kutumika kutoa na kupokea rushwa?

Yawezekana, tuombe Mungu TICRA wakamilishe zoezi la usajiri wa namba za simu mapema iwezekanavyo...
 
M-PESA huwa wanasajili wateja wao baada ya kuonyesha vitambulisho vyao. Kwa hiyo inawezekana kum-trace mtu aliyetoa au aliyepokea hongo. Ugumu wa kupiga vita rushwa upo kwenye fact kwamba wote mpokeaji na mtoaji wanakuwa wamekubaliana. Ikitokea mmoja hajaridhika ndipo crime chain inapoweza kukatika. Otherwise, it is simply difficulty.
 
M-PESA huwa wanasajili wateja wao baada ya kuonyesha vitambulisho vyao. Kwa hiyo inawezekana kum-trace mtu aliyetoa au aliyepokea hongo. Ugumu wa kupiga vita rushwa upo kwenye fact kwamba wote mpokeaji na mtoaji wanakuwa wamekubaliana. Ikitokea mmoja hajaridhika ndipo crime chain inapoweza kukatika. Otherwise, it is simply difficulty.

Ni sawa lakini kuna wale wateja ambao hawajasajiliwa, anatumiwa pesa tu anaonyesha kitambulisho anapewa, hata kitambulihso hakitolewi copy , hapo kutakuwa na ushahidi gani,
Halafu hilo zoezi la kusajili namba ni zoezi gumu sana kwa tanzania kwa sasa watapoteza biashara, wana vijana wengi sana wamewaajiri wauze sim card, kwa ajili ya ushindani na kutafuta wateja, huoni watu wataepuka kusajili namab nyingi, maana unakuta mtu 1 ana sim card tatu na zote anazitumia hawezi kuzisajili zote. kwa hiyo watapoteza wateja.
 
Kama mtu hatasajili sim card yake ni kwamba itakuwa blocked ifikapo Desemba mwaka huu. Kuna njia nyingi za kumfuatilia mtu. Voda wenyewe wanaweza kutumika kuwa-trace wahusika wote wawili endapo mmoja hajasajiliwa. Hili la kupoteza wateja halitakuwepo kwa kuwa inaruhusiwa kusajili line zaidi ya moja. Zoezi la kusajili sim card likikamilika litatatua matatizo mengi ya uhalifu, hata ule wa kutoka nje ya ndoa!
 
Basi kwa kifupi sasa hata polisi wana punguziwa vocha alafu inatumwa kwa dada yake...Rushwa ya kigoma ina pokelewa Dar!!
 
Usajili ukikamilika hata kama ukipeleka kigoma toka dar. Kinachomatter ni kuwa traceable. Kwani akina mzee wa vijisenti si walipeleka vijisenti vyake nje ya nchi, mbali sana na upeo wa macho yako lakini aliweza kugundulika. Kumbuka kuwa M-PESA ni mfumo wa kibenki kama zilivyo systems zingine. So, geographical location doesnt matter really. What matters is who did what and for what intention. Usiniulize utajuaje intention-its a matter of investigation. Every case stands on its factual situation. Evidence determines whether the case should stand or fall.
 
Back
Top Bottom