Elections 2010 Umeonawapi Fisadi wa Kikristu akipipambana na kufarakana na Fisadi wa kiislam?

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
3,362
1,130


Watanzania inabidi tuone kuwa Ufisadi ndio chanzo na msingi wa mgawanyiko wa Kitaifa unaotishia nchi yetu na tutambue kuwa mafisadi sasa hivi tayari wanafaidi mgawanyiko huo na kuwa wangependa uendelee hata kwa gharama ya udini na ukabila nk.

Inabidi tuone ni nani anataabika kwa unyonge na kuvuna maumivu ya kutosha kutokana na mgawanyiko mkubwa unaoweza kulikumba taifa.

Hivi ni huyo Mkristu na Muislam aliye fukara, mgonjwa na maskini asiyejua mlo wa siku moja ataupata wapi?... Au ni huyo Fisadi aliye kiuka misingi ya uongozi bora na kuruhusu uwekezaji mbovu wa mali ya asili ya Taifa na kuifaidi yeye, familia na marafiki zake?

Hivi wanao faidi mali ya asili ya taifa kifisadi, wametengana kulingana na makabila yao? umewasikia wakigombana kwa udini wao? Umesikia wapi Fisadi wa Kikristu akipipambana na Fisadi wa kiislam, umeona wapi Fisadi waliobobea wakitofautiana katika biashara haramu kwa sababu eti sio wa Kabila moja? au kwa kuwa rangi za ngozi hazilandani? Gundua kuwa wameshikana na Kulindana kwa nguvu zote ili hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao sasa na hata milele!

Itambulike na kueleweka fika ; Kwa nini iwe sasa baada ya miaka karibu 50 ya Uhuru wa taifa hili swala la ukabila, udini, ukanda nk vinaanza kuonekana kuwa na sauti?

Jibu ni kuwa Taifa la Tanzania halijawahi kufikia katika uongozi unaolindana kifisadi na usio na maadili kama leo. Tanzania haijawahi kuubusu na kuupakata ufisadi kama leo! Uovu wa kuikubali na kuihalalisha rushwa na kuulinda ufisadi uko kileleni.

Chimbuko la nyaraka za Kiislam na Kikristu: Ni kukomaa na kulindana Kifisadi Kunakoyumbisha UONGOZI DHAIFU WA TAIFA. Nyaraka na viongozi wa dini zote ... walifanya hivyo baada ya kuona kuwa Taifa limekuwa ya Tima. Ombwe la uongozi ni kubwa na Jamii ya Watanzania imesahaulika. Ni hakika na ni kweli kuwa kama Hatua madhubuti za kisheria zingechukuliwa dhidi ya mafisadi wakuu wa Taifa hili NYARAKA ZA KIDINI zisingekuwa na nafasi na hivyo aibu ya misigano ya kidini na kikabila isingekuwako. Dini zingebaki kuwa dini na siasa zingebaki kuwa siasa kama ambavyo ni jadi ya Watanzania. Lakini hadi leo KAGODA na wenzake wanaburudika na hawana haraka ya kuwaunganisha watanzania kwani mifarakano ya kitaifa inapotokea Mafisadi wnapata CHAKA LA KIJIFICHA NA KUFICHIA MAOVU YAO!!

Kwa sisi tunao dhulumiwa; Si upuuzi tu, bali ni ujinga na uzuzu kuchukulia jibu rahisi la tatizo hili ni Kunyoosheana vidole vya udini na ukabila kwani Fisadi asiye na chembe ya aibu na hekima yoyote hicho ndicho anachotaka Ili kujidumisha katika kuwatumia na kuwatawala wakristu na waislam waliolala na kutawaliwa ufukara, umasikini, usugu wa magonjwa na dhuluma zote na kutokuwa na sauti yeyote juu ya mali na utajiri wa Taifa lao; Nini kitatokea kama dini zote zingeungana na kutaka hatua za kishera dhidi ya EPA, KAGODA nk zichukuliwe. Ni Kiogozi yeyote wa kifisadi atazima jaribio hilo hata kama nchi ikiingia kwnye machafuko ya kidini na kikabila.

TUAMKE;

1. Viongozi wa Kidini waungane na kuwajulisha waumini wao ukweli wa tatizo la kijamii na kuwa jibu si uadui wa kidini wala kikabila ila ni kupwaya kwa uongozi wa juu wa Taifa baada ya udhaifu na uzembe uliopelekea uogozi huo kumezwa na ufisadi. Sasa mafisadi wanaligawa taifa ili wadumu na kushamiri.

2. Tutambue kuwa ufisadi ni uovu na wanao utumia na kuwekeza kwenye ufisadi huo hawatenganishwi na udini, ukabila, ukanda, rangi zao, lugha zao nk. Na itambulike kuwa Fisadi wa kikristu hana uchungu na mkristu wala muislam na fisadi wa kiislm hana huruma kwa muislam wala mkristu. Ufisadi ni Udhalimu uliokidhiri na hauna dini wala kabila katika kufikia malengo yake.

Swali kwanini sisi tunodhulumiwa tunatengwa na kuburuzwa na tunakubaliana kuvunja UMOJA NA MSHIKAMANO WETU?
 
Back
Top Bottom