Umeniharibia maisha! ...what?

Wanaume wengi tunashindwaga hapa!! Sijui ni kwanini . . . ??!! Mi nimejifunza sana hapa saa hizi!!

Tena afadhali wanaume my dia wanawake ndio kabisa tunapenda kulaumu bila kuchunguza ni wapi na sisi tunachangia au kukosea mimi katika mahusiano yangu yote yaliyopita huwa nalaumu halafu najichunguza na mie nilikosea wapi then maisha yanaendelea. Ila sasa hivi hata nikiwa na uhusiano na mtu silaumu kiviiiiiiiiiiile akijifanya kunitenda kwani umri wa kudanganywa umeshapita. Lolote linalotokea nakua nimejitakia mwenyewe
 
MTM na Mbu..., ninakubaliana na nyie 100% kwamba ni vizuri badala ya kupoint fingers tuwe tunajiangalia wenyewe..,

llakini point yangu ni kwamba "Behind every successful man there is a woman and vice versa is true..., ni kwamba in order to reach our potential lazima tupate support ya mtu and there is nothing better kama support ya mtu mnayeshare emotions.., ni kwamba huyu ni kama umempa your heart and he/she can make you or destroy you...., mfano mwingine Lauryn Hill (since ameolewa na yule bwana) she stopped pursuing her music career and the man has turned her into a house wife although she was a career woman... (ingawa angeweza kumsupport na angeweza kufanya vyote)

Ingawa kuharibu maisha its too bigger a word.., lakini am sure most of us kama tukiwapa support wenzetu kwa mambo wanayoweza kufanya effect yake inaweza ikawa better.., mfano wa mimba kama mtu atakubali kuwa mtoto ni wake na ku-offer support then its okay lakini pale anapomkataa mwanamke na kusema mtoto sio wake hapa atakuwa amempa mwanamke mzigo...

VoR aksante sana kwa kutufafanulia wazi. Kusema ukweli hii post yako inatufumbua macho na masikio na kutuonyesha umuhimu wa kujitambua na kujijua sisi wenyewe tunataka nini maishani, tuna malengo gani maishani na ni namna gani tuweze kuyachannel tunapokuwa katika mahusiano.

Mfano wa huyu Mama hill umeniuma kupitiliza laiti angejitambua na kugundua nini ni cha muhimu katika maisha yake (pengine music haukuwa wa muhimu kivile) na kuona namna anavyoweza kuishi na mpenzi wake pasipo kupoteza malengo na matarajio ya maisha yake.

Tukumbuke kuwa kila binadamu individually anayo malengo yake ya maisha, ni vema tukajifunza kudefine mapenzi kwa namna nyingine ambayo haitamaanisha kusacrifice malengo yako kwa kuwa unataka kumridhisha mpenzio, to me am sorry to say, mpenzi atakayenipenda huku akinishinikiza kuabandon my ambitions ambazo nilikuwa nazo tangu utoto, nimeincur au wazazi wangu wameincur costs kunisaidia nizifikie..............kwangu huyo hana mapenzi na kama nitamruhusu kufanya hivyo kwa kivuli cha love basi hata akijanitema baada ya mimi kupoteza uelekeo wa maisha sitamlaumu kuwa kaniharibia maisha....I let him do that, I allow him, I gave him that authority...its all my fault.
 
Tena afadhali wanaume my dia wanawake ndio kabisa tunapenda kulaumu bila kuchunguza ni wapi na sisi tunachangia au kukosea mimi katika mahusiano yangu yote yaliyopita huwa nalaumu halafu najichunguza na mie nilikosea wapi then maisha yanaendelea. Ila sasa hivi hata nikiwa na uhusiano na mtu silaumu kiviiiiiiiiiiile akijifanya kunitenda kwani umri wa kudanganywa umeshapita. Lolote linalotokea nakua nimejitakia mwenyewe
maty big up ni vizuri mtu ukijitambua aisee
 
if there comes a day nikamlaumu wife wangu kwamba kaniharibia maisha, basi ntakua nina matatizo makubwa coz i participated in the process

and if she come and say nimemuharibia maisha.... ntakubali coz women are alwayd right!!

MTM kamanda, what's eating you maazeee?
Usijitwishe mzigo wa lawama bila ku analyse tatizo ni nini na lilianzia wapi.

Women are always right? hiyo ni diplomatic approach kujustify mapungufu ya mtu..
Ipo siku hayo mambo ya 'funika kombe mwanaharamu apite' ~mw'mungu apishilie mbali~ yatakuletea BP, Kisukari na mwishowe Stroke! ...wanaume wengi miaka ya sasa ndiyo maradhi yanayotuondoa tena kwenye umri mdogo kabisa.

Stand Up for your rights!

Sasa hapa mkuu unaweza kusema NIMEHARIBU MAISHA YA MTU?

CPU, la hasha bana huyo alikuwa anakutegea 'bomu' uchukue jukumu la kujibinafsifisha familia yake yote!
Iwapo nawe kwa 'upofu' ungeingia kichwa kichwa kisa umependa, wallahi ungeturudia hapa na kilio cha umeharibiwa maisha ilhali utambuzi, uchaguzi na maamuzi yalikuwa yako mwenyewe!

Bado unaendelea nae?
 
Jaman jana tu mwenzenu aliyekuwa mpz wangu wa miaka kansalit na mwaka huu ndio nimefanikiwa fanya nae mapenzi kwani alikuwa bikla na tumefanya tendo hili mara 2 tu chakushangaza mwezi ulio pita alisafili kwenda hom kwao kwan tuna kaa wilaya tofauti baada yakufika huko nikapigiwa sim na aliwekuwa mpz wake wa zaman kabla yangu akiniambia kuwa mpnz wangu ana tembea na rafiki yake na siku ana piga cm aliwakuta mara ya 3 wakitoka guest house mi nikaamua kumuuliza akanijibu ni maneno tu ya watu alafu hapo hapo akampigia sim jama aliyenipa taarifa na kumtukana sana kisha aka mpigia huyo jamaa yake mpya kumuuliza kama ameniambia japo mimi hatufahamiani sasa mtu kama huyu haja nialibia kweli tumekuwa wote kwa miaka 3
kaka unaonekana unaandika kwa hasira sana mpaka storuy imekuwa kama hatuelewi vizuri, pole mwaya hapo hujaharibiwa maisha wala nini, ndio kwanza umeanza nae, jipe mapumziko ili upone jeraha na uendelee na maisha, usimpe kichwa na kusema kaharibu maihsha yako mwili wako baado unao

DWORK1, ....hujafa hujaumbika, kuna makubwa kuliko hayo. Chukulia hiyo ni safari ya maisha tu bana, jifunze kutokana na hilo. Ulimwamini, ukaweka matumaini yako kwake,....yeye amevunja uaminifu. Nadhani hapo ulipo umechanganyikiwa hujui umuamini nani japo umepewa 'ushahidi' wa yote.

Akili kumkichwe! ....maisha yako ya baadae na binti huyu yatategemeana na utambuzi, uchaguzi na maamuzi yako.
Ni weye mwenye maamuzi ya mwisho, ama kumsamehe au kuachana nae. Ni kwa MAISHA yako!
 
hii thread imenikumbusha mbali sana, hongera kwa wachangiaji wote, mmeelezea vizuri sana sana, hata mie niliwahi kumlaumu bfnd kwa "kuniharibia maisha" nadhani nilichanganyikiwa kiac nikawa cwezi kutofautisha kati ya "kuharibiwa maisha na kupotezewa muda" ki ujumla hakuniharibia maisha bali ningeng'ang'ana nae ndio huku mbeleni ningejiharibia maisha mwenyewe hakunipotezea muda coz muda wangu ulikuwa bado haujafika, haya mapenzi yanahitaji moyo, mie ni mmoja wa watu waliofikiria kujiua juu ya mapenzi japo ckuwahi kumtamkia bali nilikuwa napata hisia mbaya sana, nilijiona cna dhamani na wala nicngeweza kuishi bila yeye, jamani maisha haya wacheni tu.
 
Mi binafsi sipendi malawama nifanyapo maamuzi yangu, kwa hiyo ningependa kuheshimu maamuzi ya mwingine akiamua, sio kulalama tu umeharibiwa maisha, kwani mzazi wako huyo? mtu umekutana nae tu ukubwani lets say una miaka 25 then ukae nae miaka miwili useme kakuharibia maisha? umesahau miaka yote 25 uliyokuwa mwenyewe mwenye furaha?
Cha muhimu ni kuangalia wapi ulianguka ili usirudie tena kosa, na umshukuru mungu kwa uzima wako

hapa jamani wengine tulikumbwa na upofu, msiuombee huu upofu jamani, lakini tulijifunza kutokana na makosa, sasa hivi yaani roho nyeupe tayari kwa kupokea lolote litakalotokea.
 
Mkuu Mbu,

kwa mtizamo wangu mtu yeyote anayesema hivyo anakuwa amekata tamaa ya maisha na kukata tamaa ya maisha haikubaliki hata kwenye vitabu vya Dini

Mara nyingi msichana akipata ujauzito, tuseme kabla ya kuoana, inakuwa 'umeniharibia maisha' na hili linapelekea wengi kuzichoropoa thereby aggravating the problem

Au mwanaume mzima, mwanamke anakuwambia kwamba its over then unatafuta sumu unabugia....sioni sababu hata kidogo,

Kiafya ya akili, kutegemeana na exposure ya mtu, watu wanatofautiana na jinsi ya kuhandle hizi situations...lakini tuelewe kuwa there is nothing worth taking your life or some one else's life kisa eti mapenzi....haikubaliki

dah hapa funda moja tu la ziada, nitaumbuka....
 
CPU, la hasha bana huyo alikuwa anakutegea 'bomu' uchukue jukumu la kujibinafsifisha familia yake yote!
Iwapo nawe kwa 'upofu' ungeingia kichwa kichwa kisa umependa, wallahi ungeturudia hapa na kilio cha umeharibiwa maisha ilhali utambuzi, uchaguzi na maamuzi yalikuwa yako mwenyewe!

Bado unaendelea nae?

Mkuu kilichopo saa hizi ni kwamba, sijamtafuta kwa mawasiliano na wala yeye hajanitafuta. Miezi mi5 sasa.
Sasa sijui ndo tumeachana, au nimemuacha au yeye ndo kaniacha?
Hata sielewi elewi.

Nahisi kama akikubali kubadilika naweza kurudiana nae . . . lolz
 
Ngoja nikae pembeni kwanza mpaka hili sredi lianze maofu topiki....kuna watu humu nna hasira nao sana!

Subiri............!
Babu, huyo mtu kakuharibia maisha nini??
Heheh he heheh

...ha ha ha,....
Images_(25).jpg
....'nuff said! kajiharibia maisha mwenyewe,....
'Prince Charming' kosa lake nini kupendwa na 'SnowWhite?'
Snow-White-and-Prince-disney-couples-6007274-87-120.gif

Mi binafsi sipendi malawama nifanyapo maamuzi yangu, kwa hiyo ningependa kuheshimu maamuzi ya mwingine akiamua, sio kulalama tu umeharibiwa maisha, kwani mzazi wako huyo? mtu umekutana nae tu ukubwani lets say una miaka 25 then ukae nae miaka miwili useme kakuharibia maisha? umesahau miaka yote 25 uliyokuwa mwenyewe mwenye furaha?
Cha muhimu ni kuangalia wapi ulianguka ili usirudie tena kosa, na umshukuru mungu kwa uzima wako

...una busara sana wewe! Pole tena kwa kuumizwa moyo.
 
Mkuu kilichopo saa hizi ni kwamba, sijamtafuta kwa mawasiliano na wala yeye hajanitafuta. Miezi mi5 sasa.
Sasa sijui ndo tumeachana, au nimemuacha au yeye ndo kaniacha?
Hata sielewi elewi.

Nahisi kama akikubali kubadilika naweza kurudiana nae . . . lolz

lol, maisha haya, kwani kuna wa kuwapeleka skul kwenye hiyo familia au ni watu wazima wanahitaji msaada wako kwa namna moja au nyingine? sema mdada nae alilielezea vibaya.
 
Na ukimkatalia kama alikua rafiki basi ujiandae huo urafiki unakufilia mbali, utanona tu anaanza kukuchunia nia, mwisho dah

Kwa kweli nawashangaaga sana wanaume katika hili na wala siwaelewagi kabisa.
Hahahaha lol, wiki imeanza vyema mpenzi, kuwalaumu ni lazima ili wajue wafanyacho si kizuri hata kidogo.

Imagine mtu anaanza kutaka kumdanganya mtu mzima maty akifikiri nina miaka 20 lol. Na kwa sababu nimeshapita huo umri wa kudanganyika mtu anakuchunia eti, mwe!
Tena afadhali wanaume my dia wanawake ndio kabisa tunapenda kulaumu bila kuchunguza ni wapi na sisi tunachangia au kukosea mimi katika mahusiano yangu yote yaliyopita huwa nalaumu halafu najichunguza na mie nilikosea wapi then maisha yanaendelea. Ila sasa hivi hata nikiwa na uhusiano na mtu silaumu kiviiiiiiiiiiile akijifanya kunitenda kwani umri wa kudanganywa umeshapita. Lolote linalotokea nakua nimejitakia mwenyewe

...ha ha ha, Maty you are on fire leo e mama weeee!? nani huyo tena kakununia baada ya application na CV yake kukataliwa?
haya basi msitiri,....Very nice of you,...maana umegusia miongoni mwa points zangu za awali kabisa kwenye uanzilishi wa hii topik;

Tujadili kwanini kinyongo, chuki, fitna, wivu, hasira, yakichanganyika na mapenzi yanachangia walio wengi kupoteza matumaini ya maisha.

...ila wapo pia kina dada ambao nao huchukia kweli kweli iwapo mwanaume ataanzisha mahusiano na shoga yake (badala yake,) matokeo yake hata urafiki wao utalega lega au kufa iwapo mrembo nae atakuwa na msimamo thabiti kutetea mapenzi yake kwa mwanaume.

Bora mi sijakuharibia aiseee . . . . utaniachia yule mjukuu wako
Unataka kumharibia maisha?

Turudi kwenye mada:

Hii umeniharibia maisha: Inahusu jinsia zote mbili?........Bora mwanamke anaweza kulalama ameharibiwa maisha na lijanaume lililomchezea akawa na matumaini yang'arayo katika maisha...halafu ghafla bin vuu, nyota inafifia...... umri ushaenda.... cha kufanya tena hamna

Ila dume likimlalamikia mwanamke amemharibia maisha...........hebu mlilete huku nilibwenge makwenzi!
 
Mkuu Mbu,

kwa mtizamo wangu mtu yeyote anayesema hivyo anakuwa amekata tamaa ya maisha na kukata tamaa ya maisha haikubaliki hata kwenye vitabu vya Dini

Mara nyingi msichana akipata ujauzito, tuseme kabla ya kuoana, inakuwa 'umeniharibia maisha' na hili linapelekea wengi kuzichoropoa thereby aggravating the problem

Au mwanaume mzima, mwanamke anakuwambia kwamba its over then unatafuta sumu unabugia....sioni sababu hata kidogo,

Kiafya ya akili, kutegemeana na exposure ya mtu, watu wanatofautiana na jinsi ya kuhandle hizi situations...lakini tuelewe kuwa there is nothing worth taking your life or some one else's life kisa eti mapenzi....haikubaliki

dah hapa funda moja tu la ziada, nitaumbuka....

mie nilikuwa nahic ctaweza kuishi bila yeye, niliona maisha yangu bila yeye sio maisha, au hapa inategemea na c2ation yenyewe eg labda tungekuwa na maugomvi/tunakorofishana kwa muda mrefu bila suluhu labda ningeona sawa tu, lakini ile kuachwa kama jamaa alivyoniacha kweli aliniharibia maisha...hahahaha, brain yangu ilipoteza kumbukumbu kabisa, cjui ilikuwagaje aisee.
 
lol, maisha haya, kwani kuna wa kuwapeleka skul kwenye hiyo familia au ni watu wazima wanahitaji msaada wako kwa namna moja au nyingine? sema mdada nae alilielezea vibaya.

Mi mpaka leo sijajua lengo la kauli zake, alifanya makusudi, alikosea kujieleza, au nini haswa??

Ndio maana unasema
IT TAKES A SEC TO SAY I LOVE U, BUT A LIFETIME TO SHOW IT......
 
...ila wapo pia kina dada ambao nao huchukia kweli kweli iwapo mwanaume ataanzisha mahusiano na shoga yake (badala yake,) matokeo yake hata urafiki wao utalega lega au kufa iwapo mrembo nae atakuwa na msimamo thabiti kutetea mapenzi yake kwa mwanaume.

...........Mbu unaonaje hii ukaireserve for future use........?,
naona kama nayo inahitaji nafasi katika kudadavua kwa kina....lol...........
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom