Umeme wakatisha maisha ya vichanga Hospitalini Muhimbili

Ahsante kwa kuniikumbuka, nimefika.

Jee, kama genereta lipo tatizo ni JK? ingekuwa genereta hakuna hapo ndio tungemshutumu Mkuu.

Haya ni makosa ya watendaji na inabidi hatuwa za haraka zifanyike na wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu kwa makusudi kabisa.

Uozo wa utendaji Muhimbili unaonyesha kukomaa, (nikikumbuka na kisa cha kizembe kabisa cha kuchanganya wagonjwa).

Maisha ya watanzania yanapokuwa hatarini na kupotea kama hili la muhimbili basi raisi wa nchi anakuwa responsible. yaani bucks zote zinaishia kwake!
 
Kwani wafanyakazi wa serikali mnajua mishahara yao? Ni laki 3, 4 au 5!

Angalia majumba walioporomosha ya 100m Kimara, Mbezi, Segerea n.k je hizi pesa wanapata wapi???

Kuna wizi na uporaji mkubwa wa pesa za serikali throgh bogus seminars za Morogoro, supersion za kiajabu ajabu mikoani na hii ndi mwanya ya pessa ya serikali kuliwa na kujenga hizo nyumba!

Wizara ya Afya alikuja tu KM mama Gonjwe akaziba hii kula kwa mda mfupi angalia walimpiga jungu kwa JK ili amwondoe na akaondolewa sasa RAS Kilimanjaro!

Kwa kifupi wafanyakazi ktk Wizara Tz hawaishi kwa mishahara.. ila hizi allowance na wizi wa mchana.. yet if you evaluate perfomance kila Wizara in say 5 years yuo find so little echievemets Mikoani! Zaidi tu outcome ni mijumba ya mamilioni ya pesa zilizoibiwa ndo utaziona!

Hii hali ni sawa ktk Tawala za Mikoa na Halimashauri za Wilaya!

Wizi na uporaji wa pesa za kodi ndo kinachoonekana zaidi sikalini!

JK analijua hili na hii ndi imekuwa ni utamaduni wa kulindana, Mawazarani, Sekratariate za Mikoa na Halmashauri za Wilaya!

JF Mnasemaje?
 
Ahsante kwa kuniikumbuka, nimefika.

Jee, kama genereta lipo tatizo ni JK? ingekuwa genereta hakuna hapo ndio tungemshutumu Mkuu.

Haya ni makosa ya watendaji na inabidi hatuwa za haraka zifanyike na wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu kwa makusudi kabisa.

Uozo wa utendaji Muhimbili unaonyesha kukomaa, (nikikumbuka na kisa cha kizembe kabisa cha kuchanganya wagonjwa).

Dar-es-salaam,
Kwa mara ya kwanza umeongea pointi,nadhani sasa umeanza kuelewa mfumo wa utawala ukoje toka juu hadi chini.Na kwa hilo tuko pamoja.Manaake wale wakurugenzi wa muhimbili,some ni presidential appointees,akiwamo waziri husika,hivyo kama waziri akishindwa kusimamia watumishi wa wizara au mtumishi wa wizara akifanya blanda ndio maana mtu wa kwanza kulaumiwa ni waziri hata kama hakuwepo wakati blanda inatokea,na wa pili ni Rais kama atashindwa kumwajibisha waziri wake.Vivyo hivyo katibu mkuu ndiye mkuu wa utumishi wa wizara,hao wakurugenzi,wahasibu n.k.wapo chini yake,na yeye yupo chini ya waziri na waziri yupo chini ya Rais, kwa hiyo chain of command ndio maana anayeonekana juu kabisa ya pyramid ndio tunaanza naye.wengine wanafuata baadaye.
Wenzetu kwenye sheria za makampuni wanaita doctrine of corporate veil. Kwamba kampuni ni lile shela,chochote kitakachofanyika tunaliangalia kwanza shela kama shela(yaani mkurugenzi mkuu na bodi) halafu baadaye ndio tunaenda kwenye kulifunua shela(lifting corporate veil) ambapo tunachambua sasa samaki yupi kaoza yupi bado mzima,kwa mantiki hiyo nani hasa anahusika.

Inapotokea hali kama hiyo usalama wa waziri ni kumuwajibisha katibu mkuu ili naye awawajibishe waliochini yake hadi tunamfikia mtu wa mwisho mhusika mkuu akishindwa kufanya hivyo na kusababisha bunge kuingilia kati au wananchi,sisi hatuwajui hao wafanyakazi yeye ndio anawajua vizuri,sisi na wabunge tunaanza na yeye waziri kwanza,akileta nyodo tunapanda kwa Rais.Na huu hasa ndio msingi wa kusema serikali haijafanya hiki au kile.Na tunaposema serikali kwa ufupi ni baraza la mawaziri.
Japo kinadhari na kisiasa watu watakuambia serikali ni mimi na wewe.Ndio maana wananchi wakiandamana magazeti hayaripoti kwamba serikali ya tanzania imeandamana,kama kweli wewe na mimi ndio serikali,ila waziri akisema jambo ama rais utasikia serikali imesema.Hivyo Dar-es-salaam kuanza na Rais ni sawa kabisa
 
Wanabodi ,

Ni jambo la kusikitisha kuona watoto wadogo wakipoteza maisha kutokana na uzembe wa watu wachache ! Ni lazima wawajibishwe wale wote waliohusika na kitendo hiki cha kizandiki. Pili napendekeza serikali isitishe mara moja mchezo wa kutibu viongozi nje badala yake watibiwe hapo nyumbani ili Hospitali hiyo ya Muhimbili iweze kuboreshwa.
 
Wakuu hiii ni JF, hatuandikii mate na wino upo wanaohusika watajwe hapa kuanzia wa chini mpaka wa juu, tutawasukumia kuanzia wabunge mpaka mwene kaya, waamue kusuka au kunyoa,

hao wazembe huko Muhimbili wanaohusika na hivi vifo vya watoto watajwe hapa, tukate mzizi wa fitina! Until then ninampa muungwana the benefit of the doubt kwenye hili!
 
Muhimbili kulikuwa na automatic standby generator labda kama wameiua.
Hivi Mkurugenzi mkuu wa hospitali ya Muhimbili ni nani sasa hivi...bado ni prof. Lema au!? Kuna yule jamaa Tregonin ni mbabe mmoja alikuwa raia wa Ireland alikuwa mkurugenzi pale sijui alienda wapi. Yule jamaa ni mzungu lakini inasemekana alikuwa anawapandishia huko wizarani wakichelewesha vitu vinavyohatarisha maisha ya watanzania pale hospitali. Nilipataga tetesi wakurugenzi waliokuwa chini yake walikuwa wanamchukia pale hospitali sababu ya kuwabania mafisadi wasile pesa za wagonjwa. Sina hakika kama aliondoka kwa heri.
 
Dar-es-salaam,
Kwa mara ya kwanza umeongea pointi,nadhani sasa umeanza kuelewa mfumo wa utawala ukoje toka juu hadi chini.Na kwa hilo tuko pamoja.Manaake wale wakurugenzi wa muhimbili,some ni presidential appointees,akiwamo waziri husika,hivyo kama waziri akishindwa kusimamia watumishi wa wizara au mtumishi wa wizara akifanya blanda ndio maana mtu wa kwanza kulaumiwa ni waziri hata kama hakuwepo wakati blanda inatokea,na wa pili ni Rais kama atashindwa kumwajibisha waziri wake.Vivyo hivyo katibu mkuu ndiye mkuu wa utumishi wa wizara,hao wakurugenzi,wahasibu n.k.wapo chini yake,na yeye yupo chini ya waziri na waziri yupo chini ya Rais, kwa hiyo chain of command ndio maana anayeonekana juu kabisa ya pyramid ndio tunaanza naye.wengine wanafuata baadaye.
Wenzetu kwenye sheria za makampuni wanaita doctrine of corporate veil. Kwamba kampuni ni lile shela,chochote kitakachofanyika tunaliangalia kwanza shela kama shela(yaani mkurugenzi mkuu na bodi) halafu baadaye ndio tunaenda kwenye kulifunua shela(lifting corporate veil) ambapo tunachambua sasa samaki yupi kaoza yupi bado mzima,kwa mantiki hiyo nani hasa anahusika.

Inapotokea hali kama hiyo usalama wa waziri ni kumuwajibisha katibu mkuu ili naye awawajibishe waliochini yake hadi tunamfikia mtu wa mwisho mhusika mkuu akishindwa kufanya hivyo na kusababisha bunge kuingilia kati au wananchi,sisi hatuwajui hao wafanyakazi yeye ndio anawajua vizuri,sisi na wabunge tunaanza na yeye waziri kwanza,akileta nyodo tunapanda kwa Rais.Na huu hasa ndio msingi wa kusema serikali haijafanya hiki au kile.Na tunaposema serikali kwa ufupi ni baraza la mawaziri.
Japo kinadhari na kisiasa watu watakuambia serikali ni mimi na wewe.Ndio maana wananchi wakiandamana magazeti hayaripoti kwamba serikali ya tanzania imeandamana,kama kweli wewe na mimi ndio serikali,ila waziri akisema jambo ama rais utasikia serikali imesema.Hivyo Dar-es-salaam kuanza na Rais ni sawa kabisa

Laiti ungekuwa unazitazama vizuri posts zangu kwa muono mpana ungenielewa vizuri kabisa.

Kumbuka uozo wa hii nchi kaurithi JK, na hivi sasa yupo jikoni kuutafutia dawa. Kwanza tumeona ameanza na rushwa, ubadhirifu na ufisadi na hivyo ndio vyanzo vya matatizo yote haya. Halafu yanafatia haya ya uzembe, kumbuka aliwekwa Muingereza pale Muhimbili kuiendesha, akapikiwa majungu mpaka akatimka, kwa nini? kwa kuwa alikuwa anawajibika ipasavyo na kuna wengi pale wakaona wanazibiwa njia zao za ubadhirifu na ufisadi na matokeo ndio hayo.

Uzembe huu (wa Muhimbili in particular) ni confined within Muhimbili na haujaanza leo na inabidi ushughulikiwe kikamilifu.

Hau-expect kuwa Rais wa nchi akumbushe mpaka mafuta ya genereta!

Hii itakuwa si kumtendea Rais haki, kabisa.
 
..............Jee, kama genereta lipo tatizo ni JK? ingekuwa genereta hakuna hapo ndio tungemshutumu Mkuu. ..............

.....Ndugu Dar Es Salaam...kwa hili nakuunga mkono na kw ahiyo swali la msingi la kujiuliza ni

1. Standby Generator Ipo au haipo?
2. Kama ipo nani yuko resonsible nayo? (nafikiri hapa ni uongozi mzima)
3. Kama haipo WHY?.....je ni suala la bajeti? je ilikuwa knocked out kwenye bajeti? (again hapa ni uongozi mzima unawajibika)

.........kuna vitu vingine ni very basic katika institution nyeti kama hii ambayo huwezi kukwepa kwa kusingizia bajeti au sababu yeyote ile......ni lazima kuwepo na Standby Generator tena iwe ina-chekiwa na kupashwa moto mara kwa mara

Kwanini JK analaumiwa........
mikataba mibovu na kushindwa kwake kuwashughulikia viongozi wabovu ndio unasababisha uzembe kama huu uliotokea Muhimbili.........this may not be seen by many of us.....lakini ndio ukweli wenyewe.....................kila mtu serikalini ameuchapa usingizi mnono.........mikataba mibovu hawaioni na hata wakiona hawasomi na hata wakisoma hawaelewi na hata wakielewa.............kwa sababu ya interest ambazo hazijulikani.............WANASAINI!!!............shame on them!!!..................all these blunders have a knock on effect ktk idara nyingine za serikali kiuchumi na ndio sababu mambo kama yaliyotokea Muhimbili yanakuwepo
 
Naona ndugu hapo hujaelewa kinachozungumziwa kabisa
Kwanza nikueleze, kikwete hajaonyesha dalili zozote za kiukweli zaidi ya unafiki mtupu katika kulitafutia swala la rushwa suluhu, kwa sababu nyingi tu, unakumbuka watu walipowataja mafisadi wakuu alitoa kauli gani ya kuwajibu wapinzani? lakini umeyaona yaliyoibuliwa na Slaah sasa,
Unakumbuka wakati anaongea na wazee wa mkoo wa Dar alieleza nini kuhusu EL na baadae alieleza kitu gani kuhusu Kamati teule ya BUNGE, kama unayo majibu hapo utakubaliana nami kuwa JK anatupuliza uku akitungata.
Na kinachozungumziwa hapa, sio kuwa JK anatakiwa kukumbusha mppaka mafuta ya Generate, swana ni kwamba kutokana na kasumba mbovu ya kuindesha serikali, ambapo anashindwa kuwawajibisha mawaziri wake, haya ndo yanatokea, na ndo maana watu wanamuona JK kama responsible person, kwa sababu hafanyti kazi zake huko juu, kama juu hawawajibiki inategemea nini huku chini kaka??
Tafakari haya mambo kaka

Kama mimi sijaelewa kinachozungumzwa nadhani na wewe hujaelewa kabisa nnchozungumza mimi, simply, Jee, unataka kumlaumu JK kwa kucheleweshwa kuwashwa genereta muhimbili? Ukisha jibu hilo itakuwa umeelewa nichozungumza.

Kuhusu maswala ya ufisadi na rushwa nadhani unajuwa ni nini JK anachokifanya kwa uozo alioukuta. Sina haja yakurudia rudia, tume zipo na kazi zinazofanyika zinajulikana kwa wanaotaka kuona.

Kuhusu kuwajibisha mawaziri wake, duhhh, unanishangaza, yaani hata mwezi haujapita, haujayaona ya kina Lowassa, karamagi na msabaha. Wacha kuwajibisha mawaziri. JK kaweka history ya kumuwajibisha waziri mkuu.

Kuhusu kuto-kufanya kazi zake, na hili pia unanishangaza sana tena sana, wewe unaujuwa uozo aliouruthi JK? au huujuwi? kama unaujuwa sina haja ya kuanza kukutajia mmoja mmoja, kama huujuwi niambie nikutajie na nikujulishe anaushghulikia vipi kama hujui.
 
Wanabodi ,

Ni jambo la kusikitisha kuona watoto wadogo wakipoteza maisha kutokana na uzembe wa watu wachache ! Ni lazima wawajibishwe wale wote waliohusika na kitendo hiki cha kizandiki. Pili napendekeza serikali isitishe mara moja mchezo wa kutibu viongozi nje badala yake watibiwe hapo nyumbani ili Hospitali hiyo ya Muhimbili iweze kuboreshwa.

Kwa hili Mkuu Rufiji nakuunga mkono mia kwa mia.
 
Jamani Jenereta ya kukaa standby kama pale Muhimbili inagharimu karibu dola laki moja hivi na kidogo. Kimsingi mnachosema ni kuwa katika Wizara yetu ya Afya hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuchukua dakika chake kuangalia mtandao na kugundua kuwa zipo "Standby Generators" ambazo tunaweza kuzimuda na tunaaweza kununua moja kwa moja toka kwa watengenezaji.

kwa vile mimi ni mzalendo nimewapa website ya kampuni ambayo ni "maslahi" kidogo. Nawashauri wawasiliane nao na wakiulizwa nani amewarefer waandike, http://www.klhnews.com ili na miye nipate katenda kidogo.

http://www.generac.com/Default.aspx
 
.....Ndugu Dar Es Salaam...kwa hili nakuunga mkono na kw ahiyo swali la msingi la kujiuliza ni

1. Standby Generator Ipo au haipo?
2. Kama ipo nani yuko resonsible nayo? (nafikiri hapa ni uongozi mzima)
3. Kama haipo WHY?.....je ni suala la bajeti? je ilikuwa knocked out kwenye bajeti? (again hapa ni uongozi mzima unawajibika)

.........kuna vitu vingine ni very basic katika institution nyeti kama hii ambayo huwezi kukwepa kwa kusingizia bajeti au sababu yeyote ile......ni lazima kuwepo na Standby Generator tena iwe ina-chekiwa na kupashwa moto mara kwa mara

Kwanini JK analaumiwa........
mikataba mibovu na kushindwa kwake kuwashughulikia viongozi wabovu ndio unasababisha uzembe kama huu uliotokea Muhimbili.........this may not be seen by many of us.....lakini ndio ukweli wenyewe.....................kila mtu serikalini ameuchapa usingizi mnono.........mikataba mibovu hawaioni na hata wakiona hawasomi na hata wakisoma hawaelewi na hata wakielewa.............kwa sababu ya interest ambazo hazijulikani.............WANASAINI!!!............shame on them!!!..................all these blunders have a knock on effect ktk idara nyingine za serikali kiuchumi na ndio sababu mambo kama yaliyotokea Muhimbili yanakuwepo

Mkuu, 1, 2, 3, hapo juu ni kweli kabisa na naunga mkono.

Ukishuka chini kuhusu mikataba mibovu, nadhani JK kisha weka tume huru ya kuichunguza yote hii. Ulitaka afanye nini zaidi ya hilo. Mikataba mingi sana kairithi na akienda nayo kwa pupa itamtokea puani, nadhani action yake kuunda tume ni muruwa na sahihi kabisa, tungoje Mheshimiwa Zitto kabwe na wenzake watatushauri nini baada ya kuipitia. Au unasemaje?

Yes, waliosaini mikataba mibovu wakakaaa kimya wakijuwa ndio imeshatoka hiyo, JK ndie atawaumbua hao, na kwa mara ya kwanza tunaona hata bunge limekubali kuweka library ya mikataba, kwa juhudi za nani? nani kiongozi wa nchi hii? utajaza mwenyewe hapo.

Hayo ma blunders unayoyasema nakubaliana na wewe mia kwa mia na hayo ndio urithi wa JK kwa aliomtangulia na JK ndio anajitahidi kurekebisha mambo na juhudi zake tunaziona. kafikia mpaka kumuaibisha sitta kwa kumteua Mheshimiwa Zitto kwenye kamati. Nadhani na hili pia unalijuwa. Kwa hiyo Tungoje tume zitasemaje.
 
Kuna watu wantaka kupotosha kuwa genereta ilikuwa hakuna, nawashangaa sana, yaani hamkuisoma ile post ya mwanzo? inasema hivi:

" ...Walieleza kwamba baada ya kukaa gizani kwa muda wa dakika 10, umeme wa jenereta uliwaka ambapo waliruhusiwa kwenda kuwanyonyesha watoto wao...

Jenereta lipo, tatizo ni kwa nini liwake dakika 10 baadae?

Jamani Jenereta ya kukaa standby kama pale Muhimbili inagharimu karibu dola laki moja hivi na kidogo. Kimsingi mnachosema ni kuwa katika Wizara yetu ya Afya hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuchukua dakika chake kuangalia mtandao na kugundua kuwa zipo "Standby Generators" ambazo tunaweza kuzimuda na tunaaweza kununua moja kwa moja toka kwa watengenezaji.

kwa vile mimi ni mzalendo nimewapa website ya kampuni ambayo ni "maslahi" kidogo. Nawashauri wawasiliane nao na wakiulizwa nani amewarefer waandike, http://www.klhnews.com ili na miye nipate katenda kidogo.

http://www.generac.com/Default.aspx

Inaelekea jenereta ipo ila inabidi iende kuwashwa umeme ukikatika! Haikosi kuna mtaalamu wa kuwasha ambaye inabidi kwanza atafutwe umeme unapokatika. Katika karne hii ya automatic switches! Ukifikiria mitambo sensitive iliyokuwepo pale, down time ya dakika kumi inaweza kuleta madhara makubwa sana. Sidhani kama wana UPS kwa ajili ya mashine hizi. Aibu tupu!

Kwa bahati mbaya watakuwa wameondoka bure tu maana hakuna kitakachofanywa ili hali hiyo isirudiwe tena. Wazazi watamwachia mungu na kusema kuwa hata wakishitaki kwani marehemu watarudi?

Mungu aziweke mahali pema roho za malaika wake.
 
Dar es Salaam,
Kuwa muelewa hapa sio manual Generate, watu hapa wanazungumzia kuhusu automatic standaby generate, yaani amabyo umeme ukikatika wala uwezi kujua kama umeme umekatika, hili ndo swala linalozungumziwa hapa, na sio generata za kufuta na kamba ndo ziwake jamani, ebu utuelewe tunachojaribu kueleza hapa

Ingekuwa ni hivyo usemavyo wewe basi kila siku tungesikia tatizo hilo.
 
JK ana ila ya kuwa haonekani kuwa na msimamo au kuwa mkali kwa watendaji wake.
mtu anaweza kufanya kashfa ya aina yoyote, asibabaike kwa sababu JK hatomuonya au kumuwajibisha.
matatizo kama ya muhimbili ni yake, kwa vile watu hawawajibiki na yeye anawatizama tu.
 
.. Mwafrika, kikwete hawezi kukwepa lawama kama hizi. Na ndio maana katika nchi za magharibi mambo kama hayo yanapotokea anayewajibika ni waziri anayehusika na hiyo sekta.

Lakini tujitizame na sisi wenyewe tunapofanya kazi. Je tunatimiza wajibu wetu??? Nadhani unakumbuka ulipokuwa Mlimani mkuu wa idara alikuwa anaweza kuikalia dissertation yako kwa miezi kadhaa kabla ya kupelekwa kwa external examiners. Sasa jamani, hapa kweli tatizo ni la waziri wa elimu ya juu au mkuu wa idara???

Kimsingi, nakubaliana na wewe kwamba kikwete hawezi kukwepa hizi lawama. Lakini uongozi wa hospitali unawajibika kwa huu uzembe.

Hizi hospitali zetu zinakuwa katika hali mbaya na ya kusikitisha kwa sababu viongozi wote si ajabu na familia zao wanatibiwa UK, Germany, France, SA, Marekani n.k. Wangekuwa wanatibiwa katika hospitali zetu basi wangehakikisha vifaa vya kileo vinapatikana. Tumeona juzi hapa kwa kuwa Rais Kichaka alitembelea hospitali ya Amana basi ghafla bin vu kila mgonjwa akawa na kitanda chake badala ya kulala chini au wagonjwa 7 au zaidi kushare kitanda kimoja. Hivi inabidi wangoje mpaka Kichaka aje ndio vifaa muhimu vya hospitali vipatikane? Wanamdanganya nani?

Kwa hiyo inaonyesha kabisa kwamba uwezo wa kuhakikisha hospitali zetu zina vifaa vya kileo ikiwamo majenerata tunao lakini 'viongozi' hawaoni umuhimu wa hilo.
 
wasee,
mie naona si kuwatendea haki watoto marehemu na familia zao, kwa juhudi zenu mlo wengi kujaribu ku-politicize hii tragedy!!
uzembe umetokea, tatizo liwe fixed......tunasonga mbele, after all issues za hawa watoto zilikuwa medical kwanza kabla ya kitu kingine!!
kutumia fursa hii kupakatana matope na kuingiza issue za richmond, sijui buzwagi, iptl na manyang'unyang'u mengine ni ku-deviate toka kwenye main point hapa!! ambayo ni kuna tatizo muhimbili, tunaomba kwa heshima na taadhima, wizara husika iweke uhakika ya kuwa kwamba upuuzi huu hautatokea tena!!!.
 
Mkuu! Automatic Generator haichukui dakika KUMI kuwashwa. Inajiwasha yenyewe. Hizo dakika kumi ni kutokana na maelezo yao.

Hayo ni maelezo ya kina mama wako quoted wewe, soma juu vizuri. The point is, iwe dakika kumi au ishirini, why? why not immediately as usual? kwani ingekuwa si jenereta la automatic mambo yangekuwa ni kama hili janga lililotokea sasa. Lakini kabla ya hapo hatukusikia ina maana jenereta lipo na ni automatic, what was the real problem? mimi conclusion yangu ni uzembe wa watendaji pale Muhimbili na si JK. Upo hapo ulipo?
 
Back
Top Bottom