Umeme wakatika ndani ya Ukumbi wa Bunge

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Dakika tano zilizopita umeme umekatika/umekatwa ndani ya majengo yote ya ukumbi wa Bunge na hivyo kulifanya bunge kutokuweza kuendelea .

Alikuwa waziri wa Afya ndio ameanza kutoa majibu ya hoja mbalimbali za wabunge kwani ndio anahitimisha hotuba yake muda huu .


Hivi ni kweli kuwa Bunge halina generator ambazo ni automatic kwa ajili ya kutoa huduma za umeme pindi ukikatika?


Ntawajuza nini kinaendelea punde .
 
Sishangai.
Nasubiri kutangazwa kwa tume nyingine ya kuchunguza sababu za kukatika kwa umeme huko kwenye jengo la posho. Kama ambavyo amekuwa akiahidi Ngeleleja kuwa mgawo wa umeme utakuwa historia, na kweli amefanikiwa. Ni historia kubwa.
 
aTUNASUBIRI TUME NYINGINE IUNDWE. HII NI NCHI YA TUME. EVERYTHING NI TUME TU.
 
Hili swala la kukatikakatika kwa umeme sasa limekuwa unbearable...can someone at least be mature enough to show some responsibility for this mess please?
 
Sina nia mbaya lakini ili kutoa msukumo sahihi, na kama mungu anasikia naomba umeme ukatike bungeni na standby generators (zoooote) zigome walau kwa siku nzima ili wabunge wajue wajibu wao wa kuisimamia serikali hasa Wizara ya Nishati. Kila kitu kizimike!
 
Hilo Bunge ni la Tanzania au wapi??, sababu mimi hapa ninaangalia Bunge na nina uhakika ni Live unless macho yangu yananidanya na ninaota ndoto za mchana na sababu hili ni jukwaa la siasa kwahiyo hii sio Joke...:(

Please Kiranja naomba ufafanuzi
 
Hilo Bunge ni la Tanzania au wapi??, sababu mimi hapa ninaangalia Bunge na nina uhakika ni Live unless macho yangu yananidanya na ninaota ndoto za mchana na sababu hili ni jukwaa la siasa kwahiyo hii sio Joke...:(

Please Kiranja naomba ufafanuzi

Ni bunge la Tanzania , ilikuwa mara baada ya naibu waziri kumaliza kusema aliposimama waziri wa afya umeme ulikatika ukumbini8 na ulichukua dk 5-7 majenereta yakawashwa na sasa wanatumia majenereta , ni bahati kuwa TBC hawatumii umeme wa bunge bali jenereta nao wangepotea , ila waliokuwa star tv wameona ilipoitea kwa muda
 
Hivi Ngeleja hajui tu nini cha kufanya mpaka sasa?? Anasubiri nini ofisini sasa??? Anangoja kufukuzwa kazi kwa aibu??? JIUZULU kaka uwapishe wanaoweza kusimamia wizara hii.
 
Mi naomba ukatike nchi nzima na tuandamane na kufukuza Fisadi Kikwete Magogogni Mwizi mkubwa asiye na aibu, hana hata upeo wa kufikiria na wakusoma nyakati FUKUZA MWIZI MAGOGONI
 
Hivi Ngeleja hajui tu nini cha kufanya mpaka sasa?? Anasubiri nini ofisini sasa??? Anangoja kufukuzwa kazi kwa aibu??? JIUZULU kaka uwapishe wanaoweza kusimamia wizara hii.

Ngeleja hasipojiuzulu, nani unategemea atamfukuza kazi kwa aibu? Acha ndoto za mchana ndugu yangu!!!! Hakuna kitu kama kufukuzwa kwa kuwajibishwa kwenye serikali ya JK. Ngeleja sio wingu la mvua kulifanya bwawa la mtera kujaa maji!!!! Teteeeeteee!!!!!

Tiba
 
Sishangai.Nasubiri kutangazwa kwa tume nyingine ya kuchunguza sababu za kukatika kwa umeme huko kwenye jengo la posho. Kama ambavyo amekuwa akiahidi Ngeleleja kuwa mgawo wa umeme utakuwa historia, na kweli amefanikiwa. Ni historia kubwa.
hii nimeipenda 'JENGO LA POSHO'
 
Tusubiri siku moja umeme utakatika kwenye ndege ya ******
 
Back
Top Bottom