Umeme Tanzania: Kikwete ndiyo tatizo? Jisomee 'ngonjera' zake tangu 2005-2011bila utatuzi!

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
"Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, wakati akifungua rasmi Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bungeni, Dodoma, 30 Desemba 2005

Mheshimiwa Spika:

Nishati ni sawa na chembe za damu mwilini. Serikali ya Awamu ya Nne itatoa kipaumbele katika kuboresha na kuendeleza upatikanaji wa nishati ya uhakika na rahisi vijijini na mijini.

Tutapanua wigo na aina ya vyanzo vya umeme na nishati kwa jumla ili kuwa na nishati ya kutosha na yenye gharama nafuu kukidhi mahitaji ya uzalishaji viwandani, utoaji wa huduma za kijamii, na matumizi ya nyumbani.

Tutayashughulikia kwa kipaumbele cha juu matatizo ya sasa yahusuyo upatikanaji wa umeme nchini
.

Mheshimiwa Spika:


Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa Oktoba 2005 inasema wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itaharakisha mradi wa kupata umeme kutoka makaa ya mawe ya Mchuchuma. Na hivyo ndivyo tutakavyofanya.

Aidha, Serikali ya Awamu ya Nne itafufua mipango ya umeme wa Mto Rusumo na Stigler’s Gorge. Tutaharakisha pia upatikanaji wa umeme kutoka gesi asilia ya Mnazi Bay.

Mheshimiwa Spika:


Lengo la Serikali ya Awamu ya Nne pia ni kuendeleza kazi ya kufikisha umeme katika miji mikuu ya wilaya isiyo na umeme hivi sasa, kuongeza kasi ya kupeleka umeme vijijini kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini, na kuiunganisha Mikoa ya Kigoma na Ruvuma katika gridi ya Taifa.

Hotuba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye Baraza la Eid-el-Fitr, Arusha, tarehe 24 Oktoba, 2006

Bahati mbaya sana kwa upande wa tatizo la umeme hakuna majawabu ya papo kwa papo. Hata kwa umeme wa dharura imetuchukua miezi isiyopungua mitano tangu tuanze mchakato wa kukodi mitambo ya kuzalisha umeme.

Ni sasa tu ndipo baadhi ya mitambo imewasili na baadhi kuanza kazi. Ni matumaini yetu kwamba ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao au hata katikati karibu mitambo yote ya kukodi itakuwa imewasili na kuanza kuzalisha umeme.

Mitambo hii itakapoanza kuzalisha umeme, tutakuwa tumepata nafuu. Lakini, jawabu hasa litakuwa limepatikana hapo mwakani wakati mitambo mipya ya TANESCO ya Ubungo na Tegeta itakapokuwa imeanza kutoa umeme



Salamu za Mwaka Mpya za Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Watanzania,
tarehe 31 Desemba, 2006

Mwaka 2006 ulikuwa mwaka wa aina yake. Upande mmoja ulikuwa mwaka wa mafanikio mengi mazuri na kuipatia Serikali yetu pongezi na sifa nyingi. Upande mwingine ulikuwa mwaka uliokuwa na matatizo machache makubwa ambayo yalileta usumbufu mkubwa na adha kwa watu wengi nchini.

Baadhi ya matatizo hasa ya ujambazi na umeme yaliwafanya baadhi ya wananchi kupunguza imani yao kwa utendaji wa Serikali na baadhi ya vyombo vyake. Bahati nzuri, kwa majaaliwa ya Mwenyezi Mungu tunaumaliza mwaka, matatizo ya ukame, njaa na umeme yakiwa hatunayo tena na ujambazi tumeudhibiti.

Tarehe 31 Januari, 2006, nilipoongea na Watanzania kupitia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam nilieleza kuwa uzalishaji wa umeme katika mabwawa yetu ulipungua kutoka megawati 561 hadi megawati 167.5 tu.

Nilitahadharisha kuwa mgao wa umeme hauepukiki. Niliwasihi Wananchi wenzangu kuzidisha kumuomba Mungu atujalie mvua za kutosha ili baa la njaa liishe na tatizo la umeme lisichukue muda mrefu kuisha.

Kutokana na kujirudia kwa tatizo la mgao wa umeme unaoleta usumbufu mkubwa kwa watu na kuathiri uchumi wa taifa letu changa, nilielezea dhamira ya Serikali ya kuanza kuchukua hatua za dhati za kupunguza kutegemea mno umeme wa maji.

Nilieleza uamuzi wa Serikali wa kuongeza matumizi ya gesi asilia na makaa ya mawe kuzalisha umeme. Nafurahi kusema kuwa tumekwishachukua hatua muafaka.



Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa Nane Wa CCM, Ukumbi wa Kizota, 03 Novemba 2007

Nishati

Mwezi mmoja tangu Serikali ya Awamu ya Nne ianze kazi ya kuwatumikia Watanzania, tulikumbana na tatizo kubwa la aina yake la ukosefu wa umeme.

Tatizo hilo lilisababishwa na ukame ambao haujawahi kutokea kwa miaka mingi hapa nchini. Maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme yalikauka, hivyo uzalishaji umeme ukapungua sana na kwa baadhi ya vituo kusimama.

Kwa rehema za Mwenyezi Mungu mvua kubwa zilizonyesha Desemba, 2006, tatizo la umeme limeisha. Ili kuhakikisha tatizo hili halijirudii tulifanya uamuzi wa makusudi wa kuongeza wigo wavyanzo vya kuzalisha umeme badala ya kutegemea mno maji.

Kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa tumeongeza kwa asilimia 60 umeme unaozalishwa kutokana na vyanzo vingine.

Kutokana na jitihada hizi, sasa hivi tuna ziada ya umeme kwenye gridi ya Taifa. Sio rahisi sasa katika miaka michache ijayo nchi yetu kupata tatizo la upungufu wa umeme kama lile labda kutokee dharura aina nyingine.


Changamoto iliyobakia sasa ni kuyaingiza maeneo mengi zaidi kwenye Gridi ya Taifa na kuwasambazia kwa umeme watu wengi zaidi. Mpaka sasa ni asilimia 10 tu ya Watanzania wanapata umeme, hivyo kuna kazi kubwa ya kufanya katika eneo hili.

Katika kutekeleza Ilani, tumeongeza kasi ya kusambaza umeme vijijini kwa kuanzisha Mfuko wa Nishati Vijijini. Mwaka huu, tumetenga shilingi bilioni 10 kwa ajili hiyo

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, wakati akiwahutubia Wananchi wa Dodoma na Wabunge kwenye Ukumbi wa Kilimani, Dodoma tarehe 10 Juni, 2009

Mwisho kabisa, nawasihi viongozi wenzangu na wananchi kwa ujumla, tuwe wavumilivu na tuiunge mkono Serikali katika kutekeleza mkakati huu.

Tangu mwaka 2006, mambo hayakuwa mepesi sana, tumepitia misukosuko mikubwa kwa uchumi wetu: mgao mkubwa wa umeme
, njaa, bei kubwa ya mafuta na bei kubwa za vyakula na sasa msukosuko huu wa aina yake.

Kwa kila tatizo tumepambana nalo kiume na kwa umakini mkubwa na kuvuka salama. Mshikamano wetu, umoja wetu ndiyo uliotufikisha hapo.


Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika Sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa Somanga-Fungu, 16 Agosti, 2010

Nakushukuru Mheshimiwa William Ngeleja, Waziri wa Nishati na Madini kwa kunialika katika hafla hii ya uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa Somanga Fungu.

Mradi huu wa umeme ambao umezinduliwa leo, ni mwendelezo wa hatua za Serikali za kutekeleza sera zake za msingi za kuhakikisha kuwa wananchi wanapata nishati ya uhakika, yenye gharama nafuu, na isiyoharibu mazingira yetu

Changamoto ya kwanza iliyo mbele yenu ni ujenzi wa nyumba bora ili muweze kuunganishiwa umeme majumbani kwenu.

Serikali itafarijika sana endapo baada ya muda mfupi tutaambiwa kuwa, umeme huu ambao leo unaonekana ni mwingi kuliko mahitaji yenu, hautoshi kwa kuwa matumizi yamekuwa makubwa kuliko umeme uliopo. Hiyo itakuwa changamoto nzuri kwani itadhihirisha kuwa malengo ya mradi huu yamefikiwa.


Kikwete aahidi umeme mikoa ya Kusini
Lindi,19 October 2010

Mgombea Urais kupitia CCM, Rais Jakaya Kikwete, amesena tatizo la umeme lililokuwa linaikabili mikoa ya kusini sasa litabaki historia baada ya kufanikiwa kupatikana kwa umeme wa gesi ya asilia kutoka Songosongo.


Alisema wilaya ya Kilwa ambayo ilikuwa ina tatizo la umeme kwa muda mrefu, sasa ina umeme wa uhakika baada kupatikana kwa umeme huo


Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, katika Ibada ya Kumweka Wakfu Askofu Mteule Gervas John Nyaisonga wa Jimbo Katoliki Dodoma, tarehe 19 Machi, 2011, Dodoma

Jambo lingine ninalowaomba viongozi wa dini muendelee kuiombea nchi yetu ipate mvua za kutosha, mabwawa yajae, umeme upatikane na nchi iwe na chakula cha kutosha.

Kadhalika msichoke kuiombea nchi yetu amani na upendo miongoni mwa wananchi wake. Jambo kubwa la kusisitiza hapa ni kuwataka watu wapendane, washirikiane na kamwe wasibaguane kwa rangi, kabila, dini, jinsia, maeneo wanayotoka au itikadi za kisiasa.

Haya ni miongoni mwa mambo ya tunu ambayo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere alituachia Watanzania. Ndiyo siri ya amani na utulivu wa nchi yetu. Hatuna budi kuyaenzi na kuyaendeleza."




My take: Hizi Ngonjera hizi za Rais sio nzuri kwa mstakabali wa Taifa tokea 2005 mpaka sasa ni mikakati kwenda mbele.
 
Alafu naona anasisizita sana swala la kumuomba Mungu kutatua kero ya umeme, huwa anamaanisha
Mungu gani,huyu huyu ambaye huwa anakwenda kutoa kafara na kumuwashia ubani kwenye viduku...
 
Technologia imetusaidia kuwaumbua watawala waongo na makanjanja.. kama kuna mtu ana audio ya ahadi za Kikwete 2010 naomba atusaidie kuzibandika hapa na ikiwezekana Mod aziweke juu kabisa kama alivyofanya kwenye mswada wa katiba ili tuendelee kuwakusha kama wamesahau...!
 
Yawezekana kabisa hajawahi kupitia aliyoyatamka kwenye hotuba zake za awali, na wasaidizi katika hotuba zake nao pia yaonekana hawajali wala kutilia maanani umuhimu wa kutorudia rudia yaleyale ambayo yanazidi kugeuka ahadi hewa. Ni kitu gani la msingi jamani ambalo tutaonekana tumeweza kwa asilimia mia na kutamba nalo ndani ya miaka kumi hivyo kuupongeza uongozi wa Mh. Kikwete katika kulifanikisha??

- Umeme: Tatitzo sugu, ni ahadi tu zimebaikia, kero zinazidi

- Kilimo kwanza: Kimebakia kwenye manifesto tu, mbolea, pembejeo bado aghali, mazao bado yanaozea mashambani.

- Ufisadi: Tumebakia kuambiwa ni kujivua magamba tu, hatuoni sheria zikitumika kuwaadhibu waliwo jivalisha magamba hayo.

- Muungano: This is a time bomb! Kuchomeana makazi na biashara kumeshaanza...

- Katiba: Bila ya wananchi na Wanachadema kugangamala tungebakia kubambikizwa Katiba kufuru kwa Taifa letu, huku CCM wakibakia kupiga makofi na vigelegele Bungeni!! Katika hili, Mh. Kikwete ana nafasi nzuri ya kujiwekea kumbukumbu ya kutukuzwa katika historia, as long as atabadilika na kuanza kutumikia kiapo alichotoa pale uwanja wa Taifa!!
 
Technologia imetusaidia kuwaumbua watawala waongo na makanjanja.. kama kuna mtu ana audio ya ahadi za Kikwete 2010 naomba atusaidie kuzibandika hapa na ikiwezekana Mod aziweke juu kabisa kama alivyofanya kwenye mswada wa katiba ili tuendelee kuwakusha kama wamesahau...!


AUDIO YA NGOJERA ZA UMEME WA UHAKIKA TANZANIA

 
Last edited by a moderator:
Kwa hali ya kawaida kabisa ukiona nchi inaongozwa na kiongozi ambaye ni malaya basi lazima ufahamu kuna tatizo kubwa. Mtikisiko ambao tunakumbana nao ni kutokana na kuwa na rais ambaye sifa yake kubwa ni hiyo, sasa atapata wakati lini kutatua maswala ya kitaifa? Natumaini wengi wanafahamu nini kinaendelea kule Italy ambako wana tatizo kama letu lakini wenzetu wako mbali zaidi ndio sababu hawana mkwara mkubwa kama wetu. Keki yetu ni ndogo na ni hiyo hiyo anayotumia kuwahonga mafisadi sasa hatuwezi kufika mbali ni machungu tu yataendelea hadi pale tutakapoweza kumng'oa kutoka pale magogoni na kumrudisha Msoga.
 
Yawezekana kabisa hajawahi kupitia aliyoyatamka kwenye hotuba zake za awali, na wasaidizi katika hotuba zake nao pia yaonekana hawajali wala kutilia maanani umuhimu wa kutorudia rudia yaleyale ambayo yanazidi kugeuka ahadi hewa. Ni kitu gani la msingi jamani ambalo tutaonekana tumeweza kwa asilimia mia na kutamba nalo ndani ya miaka kumi hivyo kuupongeza uongozi wa Mh. Kikwete katika kulifanikisha??

- Umeme: Tatitzo sugu, ni ahadi tu zimebaikia, kero zinazidi

- Kilimo kwanza: Kimebakia kwenye manifesto tu, mbolea, pembejeo bado aghali, mazao bado yanaozea mashambani.

- Ufisadi: Tumebakia kuambiwa ni kujivua magamba tu, hatuoni sheria zikitumika kuwaadhibu waliwo jivalisha magamba hayo.

- Muungano: This is a time bomb! Kuchomeana makazi na biashara kumeshaanza...

- Katiba: Bila ya wananchi na Wanachadema kugangamala tungebakia kubambikizwa Katiba kufuru kwa Taifa letu, huku CCM wakibakia kupiga makofi na vigelegele Bungeni!! Katika hili, Mh. Kikwete ana nafasi nzuri ya kujiwekea kumbukumbu ya kutukuzwa katika historia, as long as atabadilika na kuanza kutumikia kiapo alichotoa pale uwanja wa Taifa!!

Sijui kama Rais huwa anarudia hotuba zake kusoma aliyoyaandika
 
Kwa kua Mh Rais anakaribia muda wake wa kuondoka madarakani si vibaya tukamkumbusha alichoahidi na hajakifanyia kazi. Back Tanganyika.
 
"Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
wakati akifungua rasmi Bunge Jipya la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Bungeni, Dodoma, 30 Desemba 2005
Mheshimiwa Spika:
Nishati ni sawa na chembe za damu mwilini.
Serikali ya Awamu ya Nne itatoa kipaumbele
katika kuboresha na kuendeleza upatikanaji wa
nishati ya uhakika na rahisi vijijini na mijini.
Tutapanua wigo na aina ya vyanzo vya umeme
na nishati kwa jumla ili kuwa na nishati ya
kutosha na yenye gharama nafuu kukidhi
mahitaji ya uzalishaji viwandani, utoaji wa
huduma za kijamii, na matumizi ya nyumbani.
Tutayashughulikia kwa kipaumbele cha juu
matatizo ya sasa yahusuyo upatikanaji wa
umeme nchini.
Mheshimiwa Spika:
Ilani ya CCM ya Uchaguzi wa Oktoba 2005
inasema wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Nne
itaharakisha mradi wa kupata umeme kutoka
makaa ya mawe ya Mchuchuma. Na hivyo
ndivyo tutakavyofanya.
Aidha, Serikali ya Awamu ya Nne itafufua
mipango ya umeme wa Mto Rusumo na
Stigler’s Gorge . Tutaharakisha pia upatikanaji
wa umeme kutoka gesi asilia ya Mnazi Bay.
Mheshimiwa Spika:
Lengo la Serikali ya Awamu ya Nne pia ni
kuendeleza kazi ya kufikisha umeme katika miji
mikuu ya wilaya isiyo na umeme hivi sasa,
kuongeza kasi ya kupeleka umeme vijijini
kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini, na
kuiunganisha Mikoa ya Kigoma na Ruvuma
katika gridi ya Taifa.
Hotuba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
kwenye Baraza la Eid-el-Fitr, Arusha, tarehe
24 Oktoba, 2006
Bahati mbaya sana kwa upande wa tatizo la
umeme hakuna majawabu ya papo kwa papo.
Hata kwa umeme wa dharura imetuchukua
miezi isiyopungua mitano tangu tuanze
mchakato wa kukodi mitambo ya kuzalisha
umeme.
Ni sasa tu ndipo baadhi ya mitambo imewasili
na baadhi kuanza kazi. Ni matumaini yetu
kwamba ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao
au hata katikati karibu mitambo yote ya
kukodi itakuwa imewasili na kuanza
kuzalisha umeme .
Mitambo hii itakapoanza kuzalisha umeme,
tutakuwa tumepata nafuu. Lakini, jawabu hasa
litakuwa limepatikana hapo mwakani wakati
mitambo mipya ya TANESCO ya Ubungo na
Tegeta itakapokuwa imeanza kutoa umeme
Salamu za Mwaka Mpya za Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa Watanzania,
tarehe 31 Desemba, 2006
Mwaka 2006 ulikuwa mwaka wa aina yake.
Upande mmoja ulikuwa mwaka wa mafanikio
mengi mazuri na kuipatia Serikali yetu pongezi
na sifa nyingi. Upande mwingine ulikuwa
mwaka uliokuwa na matatizo machache
makubwa ambayo yalileta usumbufu mkubwa
na adha kwa watu wengi nchini.
Baadhi ya matatizo hasa ya ujambazi na
umeme yaliwafanya baadhi ya wananchi
kupunguza imani yao kwa utendaji wa Serikali
na baadhi ya vyombo vyake. Bahati nzuri, kwa
majaaliwa ya Mwenyezi Mungu tunaumaliza
mwaka, matatizo ya ukame, njaa na umeme
yakiwa hatunayo tena na ujambazi
tumeudhibiti.
Tarehe 31 Januari, 2006, nilipoongea na
Watanzania kupitia Wazee wa Mkoa wa Dar es
Salaam nilieleza kuwa uzalishaji wa umeme
katika mabwawa yetu ulipungua kutoka
megawati 561 hadi megawati 167.5 tu.
Nilitahadharisha kuwa mgao wa umeme
hauepukiki. Niliwasihi Wananchi wenzangu
kuzidisha kumuomba Mungu atujalie mvua za
kutosha ili baa la njaa liishe na tatizo la
umeme lisichukue muda mrefu kuisha.
Kutokana na kujirudia kwa tatizo la mgao
wa umeme unaoleta usumbufu mkubwa
kwa watu na kuathiri uchumi wa taifa letu
changa, nilielezea dhamira ya Serikali ya
kuanza kuchukua hatua za dhati za
kupunguza kutegemea mno umeme wa
maji.
Nilieleza uamuzi wa Serikali wa kuongeza
matumizi ya gesi asilia na makaa ya mawe
kuzalisha umeme. Nafurahi kusema kuwa
tumekwishachukua hatua muafaka.
Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Jakaya Mrisho Kikwete, Kwenye Ufunguzi
wa Mkutano wa Nane Wa CCM, Ukumbi wa
Kizota, 03 Novemba 2007
Nishati
Mwezi mmoja tangu Serikali ya Awamu ya Nne
ianze kazi ya kuwatumikia Watanzania,
tulikumbana na tatizo kubwa la aina yake la
ukosefu wa umeme.
Tatizo hilo lilisababishwa na ukame ambao
haujawahi kutokea kwa miaka mingi hapa
nchini. Maji katika mabwawa ya kuzalishia
umeme yalikauka, hivyo uzalishaji umeme
ukapungua sana na kwa baadhi ya vituo
kusimama.
Kwa rehema za Mwenyezi Mungu mvua kubwa
zilizonyesha Desemba, 2006, tatizo la umeme
limeisha. Ili kuhakikisha tatizo hili halijirudii
tulifanya uamuzi wa makusudi wa kuongeza
wigo wavyanzo vya kuzalisha umeme badala ya
kutegemea mno maji.
Kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa tumeongeza
kwa asilimia 60 umeme unaozalishwa kutokana
na vyanzo vingine.
Kutokana na jitihada hizi, sasa hivi tuna
ziada ya umeme kwenye gridi ya Taifa. Sio
rahisi sasa katika miaka michache ijayo
nchi yetu kupata tatizo la upungufu wa
umeme kama lile labda kutokee dharura
aina nyingine.
Changamoto iliyobakia sasa ni kuyaingiza
maeneo mengi zaidi kwenye Gridi ya Taifa na
kuwasambazia kwa umeme watu wengi zaidi.
Mpaka sasa ni asilimia 10 tu ya Watanzania
wanapata umeme, hivyo kuna kazi kubwa ya
kufanya katika eneo hili .
Katika kutekeleza Ilani, tumeongeza kasi ya
kusambaza umeme vijijini kwa kuanzisha Mfuko
wa Nishati Vijijini. Mwaka huu, tumetenga
shilingi bilioni 10 kwa ajili hiyo
Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete, wakati akiwahutubia Wananchi wa
Dodoma na Wabunge kwenye Ukumbi wa
Kilimani, Dodoma tarehe 10 Juni, 2009
Mwisho kabisa, nawasihi viongozi wenzangu na
wananchi kwa ujumla, tuwe wavumilivu na
tuiunge mkono Serikali katika kutekeleza
mkakati huu.
Tangu mwaka 2006, mambo hayakuwa mepesi
sana, tumepitia misukosuko mikubwa kwa
uchumi wetu: mgao mkubwa wa umeme, njaa,
bei kubwa ya mafuta na bei kubwa za vyakula
na sasa msukosuko huu wa aina yake.
Kwa kila tatizo tumepambana nalo kiume na
kwa umakini mkubwa na kuvuka salama.
Mshikamano wetu, umoja wetu ndiyo
uliotufikisha hapo.
Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
katika Sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa
Umeme wa Gesi wa Somanga-Fungu, 16
Agosti, 2010
Nakushukuru Mheshimiwa William Ngeleja,
Waziri wa Nishati na Madini kwa kunialika
katika hafla hii ya uzinduzi wa Mradi wa
Umeme wa Gesi wa Somanga Fungu.
Mradi huu wa umeme ambao umezinduliwa
leo, ni mwendelezo wa hatua za Serikali za
kutekeleza sera zake za msingi za
kuhakikisha kuwa wananchi wanapata
nishati ya uhakika, yenye gharama nafuu,
na isiyoharibu mazingira yetu
Changamoto ya kwanza iliyo mbele yenu ni
ujenzi wa nyumba bora ili muweze
kuunganishiwa umeme majumbani kwenu.
Serikali itafarijika sana endapo baada ya
muda mfupi tutaambiwa kuwa, umeme huu
ambao leo unaonekana ni mwingi kuliko
mahitaji yenu, hautoshi kwa kuwa
matumizi yamekuwa makubwa kuliko
umeme uliopo . Hiyo itakuwa changamoto
nzuri kwani itadhihirisha kuwa malengo ya
mradi huu yamefikiwa.
Kikwete aahidi umeme mikoa ya
Kusini Lindi,19 October 2010
Mgombea Urais kupitia CCM, Rais Jakaya
Kikwete, amesena tatizo la umeme lililokuwa
linaikabili mikoa ya kusini sasa litabaki
historia baada ya kufanikiwa kupatikana kwa
umeme wa gesi ya asilia kutoka Songosongo.
Alisema wilaya ya Kilwa ambayo ilikuwa ina
tatizo la umeme kwa muda mrefu, sasa ina
umeme wa uhakika baada kupatikana kwa
umeme huo
Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
katika Ibada ya Kumweka Wakfu Askofu
Mteule Gervas John Nyaisonga wa Jimbo
Katoliki Dodoma, tarehe 19 Machi, 2011,
Dodoma
Jambo lingine ninalowaomba v iongozi wa dini
muendelee kuiombea nchi yetu ipate mvua
za kutosha, mabwawa yajae, umeme
upatikane na nchi iwe na chakula cha
kutosha.
Kadhalika msichoke kuiombea nchi yetu amani
na upendo miongoni mwa wananchi wake.
Jambo kubwa la kusisitiza hapa ni kuwataka
watu wapendane, washirikiane na kamwe
wasibaguane kwa rangi, kabila, dini, jinsia,
maeneo wanayotoka au itikadi za kisiasa.
Haya ni miongoni mwa mambo ya tunu
ambayo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere
alituachia Watanzania. Ndiyo siri ya amani na
utulivu wa nchi yetu. Hatuna budi kuyaenzi na
kuyaendeleza."
 
Back
Top Bottom