Umeme na Nishati: Tatizo sugu Tanzania

Ungwini wangu ni upi huo unaouchukia yakhe? au bado una hasira na mimi tangu enzi za Gimme the Loot?

I am not ngwini or a scientist, just an average guy like Joe the Plumber. I think, read and reason on everything.

For your information I am one of the few people who are trying to push for Tanzania to go Solar and Wind Power and reduce dependency on Hydropower because of draught and de-forestation!

Sasa kama nyie spana boi, hamuoni kuwa Umeme wa Pangaboi na Jua unaweza kutupa alternative japo 30% kupunguza hizo Hydro au Diseli ambazo zinapuliti nchi, je mmelala usingizi wa namna gani, mtoto wa mjini kama mimi niwaze ubora wa umeme wa jua?

Hate the game bwana not a playerR ndio maana nakuambia hata Kapukeki atakukimbia kisa unakokotoa hisabati left and right kujaribu kumwambia ana sura nzuri na umbo zuri!

Ukizidiwa chukua Shairi la Shekispia umuimbie Kapukeki na si Algorithim!

Unachemka! Kama kawaida stori mureeeeefu, mie wala sikumbuki mambo ya gimme the loot.....sinaga mashinde na mambo ya JF, kwangu mimi hii ni pastime tu!! LOL

Kuhusu solar power wewe unajuaje kama mabibi na mabwana umeme hawajawaambie hao mangwini wenzako juu ya hilo?? Mie nina mshkaji anafanya kazi na GE kule Erie tena wanamwamini kaa nini sijui.....lakini mchizi angekuwa bongo angekuwa anauza masufuria kwenye duka la muhindi....watu hawapewi nafasi, hawasikilizwi, mishahara midogo yaani alimuradi ni tafrani tupu...

Mnaua nchi....
 
Hehehehehe by the way aliyegundua solar power alikuwa ngwini George W. Bush..........mangwini ni kiboko yao!
 
Sehemu ya hotuba aliyoitoa Rais Jakya Kikwete tarehe Mei 9, 2006 kwa wadau wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), ilikuwa na maneno yafuatayo kuhusu matatizo ya umeme. (Hii ni kulingana na mwandishi wa Raia Mwema, Godfrey Dilunga ya leo Machi 11, 2009)


We have been grappling with this problem for quite some time now – but only with ad hoc measures.The recent power problems have afforded us the opportunity to rethink our energy strategy in holistic terms. We have learnt that ad hoc measures are costly in the long run and have their own limits. As we grapple with our energy problem, we are witnessing an upsurge of interest for investments in power generation in Tanzania. We are confident that in two years time, we will be on course to realize reliable power supply in Tanzania.

Toka Mei 9, 2006 hadi leo ni miaka karibia mitatu na ndio kwanza tunafikiria kununua mitambo ya dharura na chakavu kutoka kampuni tapeli. Je tunaodai tuna uongozi wa kisanii na kwamba CCM ni chama cha kilaghai tunakosea ? Je kama bunge letu lingekuwa linatimiza wajibu wake, sio wakati muafaka wa kumkaanga Raisi kwa kutoa ahadi hewa ? Je tatizo sugu la umeme na nishati Tanzania inatumiwa kama mianya na fursa kwa wezi na wahujumu kuendelea kuitafuna nchi ? Je tutaweza kuondokana na tatizo hili chini ya viongozi wanaopewa madaraka kupitia hiki chama kinachojali maslahi yake badala ya taifa ?
 
Mag,

I am glad you kept records of this! This reminds of the CNBC guy Kramer who gave ill advise on Bear Sterns and when the stock tanked and company belly uped, he denied giving strong and positive advice for people to buy the damn stock.

Lakini watu walikuwa na nukuu ya kila kitu!

Sasa leo nitaomba kama nikiwa ni mwandishi wa habari na Kikwete au Ngeleja anaongelea hili suala la Dowans, ningehoji hiyo kauli na kuuliza kilichofanyika mpaka dakika hii!
 
Wadau,

Ikiwa bado sijapata bei kamili za ile GE na Siemens turbines, utafiti wangu unaonyesha kuwa kwa kutumia takriban dola za kimarekani $500 tunaweza kupata mitambo 200 ya 1.5 mw (jumla megawati 250 au zaidi) yenye kutumia nguvu za upepo kuzalisha umeme.

Bado naendela na utafiti!
 
Normally, I would agree with you 100%, but unfortunately due to reasons I have cited in my posting on page 6, this is not true in Tanzania. Hence my argument and I agree with Rev Kishoka, that despite his lack of engineering knowledge he would make a good manager of TANESCO. For example do you think that in order to manage Muhimbili, we need a doctor to manage it? Or to manage KIA airport we need a pilot? No, we need good managers! Expertise advise is essential and a good manager is the one who gets the right experts to advise him and implement plans.

This is a fact - Plessey Engineering ya Uingereza kwenye miaka ya sabini, ilijaribu kwa kufanya mabadiliko katika uongozi wake na kupendekeza kuwa ili ufanisi uongezeke, nafasi ya CEO mpaka wakurugenzi mbalimbali zishikwe na mainjinia. Matokeo ya zoezi hilo yalielezeka kwa neno moja tu "disaster". Within one year kampuni ilikuwa inachungulia kaburi na hao walioitwa mangwini ilibidi watafutwe haraka kuifufua Plessey. Toka wakati huo iliamuliwa kuwa ni busara zaidi CEO wa Plessey asiwe Engineer - lakini kamwe asithubutu kupuuza bali azingatie ushauri wa wataalamu (Engineers).

Mimi ni engineer by profession.
 
Hizi longo longo zimekuwa nyingi sana ,wakati wa Mchonga tulikuwa hatusikii fisadi kusema kuna tatizo la umeme na wakati wa mkoloni wa mwanzo ndio kabisa ,huduma kila palipokuwa na umati wa watu ,yaani hata ukitembelea vijijini unaweza kukuta kisima na kuambiwa kilichimwa tokea wakati wa mkoloni.

Alipoondoka mkoloni na baada ya kufariki Mchonga ,tukaanza kusikia ndogondogo zikipigwa na kuwadanganya wananchi na hata viongozi wasio kuwa na uelewa ,kuwa mvua zimeanza kuwa ndigo mara kuna Alminyo mara mvua zimeadimika mara unaanza kusikia kina cha maji kimepungua tena si bwawa moja mabwawa yote kwa mpigo ,wafuasi mafisadi wakaamua kutafuta njia za kupambana na hali hiyo , ili njia hiyo ifanikiwe wafuasi wa Sultani CCM wakaanzisha umeme wa mgao ili kuwatesa wananchi na kuamini kuwa kina cha maji kimepungua ,na kuwashinda maarifa wengine kukaamuliwa njia ya kupata umeme ambao ni kutafuta wawekezaji ndipo kukazuka akina Richmond na hatujakaa vizuri akina Dowarn na wengine kibao na ba katika mpito huo kukaibuka makampuni kibao mpka ya kuchimba dhahabu na kukoboa mkaa wa mawe ,yaani vijikampuni vikawa vinatajika japo havina hata ofisi ni majina tu yakienda huku na kule kutafuta fedha za kuendeshea miradi ambayo ni hewa ,kwa vile waliokuwa na miradi ndio haohao wakubwa serikalini mambo yalikuwa yakisainiwa bila ya vizuizi ambavyo mkulima anaekwenda kutafuta mkopo wa kununulia mbolea huwa vinamkuta.

Miradi ya kuchunguza uranium huisikii kutajwa ,kuna mfuasi mmoja wa Sultani CCM alikurupuka na kusema umefika wakati wa kutumia rasilimali hiyo ili tupate umeme wa uhakika lakini miaka inakatika ,hatujui hata njia aliokwendea.

Sasa Mheshimiwa Pinda kazuka na jipya ,na kwa kweli nilijua tu hizi heka heka za kupongezana na kuchapuka mwendo katika kutembelea mashariki na magharibi huku akiweka mikakati ya kila jambo liwe limefuatiliwa kwa pale alipopaona pana harufu za ufisadi au hapaeleweki kimapato ,Pinda amezuka na alke la kuwataka wawekezaji wajitokeze kuwekeza Umeme , hivi hasara za hayo anayoyatafuta hajaziona ?

Ikiwa wawekezaji tumewaona kuanzia kwenye madini ,usafiri wa anga ,usafiri wa reli na hata huko kwenye umeme ndio kwanza kumeondoka moto ,sasa Mh.Pinda ameanza kupuliza na dalili za kufuka moshi karibu zitaonekana.

Matumaini ya kutumia Uranium Mheshimiwa Pinda yamefikia wapi ? Mbona siku hizi huko majuu limekuwa ni jambo la kawaida na kwa vile hatuna wataalamu ambao wanaweza kufikia utengenezaji wa bomu ni rahisi sana kwa kukubaliwa na sehemu za kutupa takataka kwa Tanzania hii hatukosi tuna mabonde ya ufa kibao ambayo mengine hata chini hukuoni.Tutazidi kuyachimba na kufukia takataka hizo huko.

Mambo haya ya kuburuzana ni kutaka tuendelee kukaa gizani ili muzidi kutuibia kwani umeme ukiwepo kila pembe secury camera zitaenea kila nyumba na hivyo kuweza kuweka alarm za kuwakurupusha majambazi lakini hayo hamyataki kwani bado katika serikali yenu kuna akina Zombe na Mahita ,ambao kuwakosa ni muhali.

Mh.Pinda kumbuka maneno ya Mchonga kuwa UCHUMI UNAUKALIA ,hivyo usitafute wawekezaji changamkia tenda ya umeme wa uranium tuone kama itamaliza miaka miwili hatujaenza umeme mpaka kwenye mbuga za wanyama. Angalau wao nao wafanane na sisi maana kwa hali hii tuliyonayo hivi sasa kiza hiki basi ni sisi tunaofanana nao.
 
Hebu tuchukue hatua moja na kuliangalia hili jambo la nishati kwa mtazamo mwingine wa ki-ngwini!

Nitaanzia na Zanzibar. Zanzibar, mpaka leo wanafanya wateja na watumwa wa Tanesco kwenye suala hili la umeme.

Je mahitaji ya Umeme Zanzibar kwa ajili ya nyumba, maofisi na viwanda ni kiasi gani? Tukishajua mahitaji hayo, kuna uwezekano wa Zanzibar kujitutumua na kuwa na mitambo yao ambayo ni huru kutoka Tanesco kujizalishia umeme na hivyo kuondokana na Ukiritimba wa Tanesco?

Kama Zanzibar matumizi yao ni 250 MW, wakinunua mtambo wa MW 500, umeme wa ziada kuunganishwa kwenye gridi ya Taifa na zaidi unaweza kusaidia kupanuka kwa matumizi ya Umeme Zanzibar na hivyo kuhakikisha kila nyumba ina umeme madhubuti na viwanda kuweza kuongezeka hivyo kukuza uchumi na kuawa huru ki-nishati?

Je suala la Zanzibar kuwa na mfumo huru wa Umeme ni lazima lipate baraka ya Serikali ya Muungano au SMZ ina uwezo tosha kupitia fungu lake lenyewe kujizalishia umeme huru ya kufuatilia makubaliano yaliyo chini ya Wizara ya Nishati na mfumo wa Umeme Tanzania?

Kama Zanzibar wataweza kujitoa kwenye utegemezi huu wa Tanesco kujipatia na kujizalishia umeme na wao wakawajibika kwa EWURA na hata mfumo wao kuweza kuzalisha na kuchangia kwenye Gridi ya Taifa, hatuoni kuwa kutakuwa na manufaa katika maendeleo yetu kama Taifa na kuondokana na mikorogano tuliyonayo na lawama kuwanyanyasa Zanzibar?


Nikirudi Bara, tuna wilaya takriban 130. Je ukiondoa miji mikubwa kama Dar, Moro, Arusha na mingineyo ambayo kuna viwanda, je mahitaji yetu na nyumba zinazotumia umeme ni kiasi gani?

Ni nyumba ngapi katika wilaya ya Hai ambazo zinatumia umeme wa Tanesco na si vibatari? Je wilaya ya Kondoa, Bahi, Manyoni, Nzega na Kigoma Vijijini?

Je umeme uliopo ambao ni wa Diseli ambao tunajua kwa takwimu za Tanesco ni 34 MW
ISOLATED DIESEL POWER STATIONS
• Total installed Capacity – 33.8 MW
• Available generation varies from month to month, but in 2006 it averaged 17.5 MW.
• TANESCO’s isolated diesel power stations which are not connected to the national grid system are located at Mtwara, Lindi, Songea, Masasi, Tunduru and Kilwa Masoko. Other townships are Mpanda, Kigoma, Mafia, Ikwiriri, Ngara, Biharamulo, Liwale and Njombe.
• Most of the diesel power stations are aged and urgently require running spare parts to improve their operational performance. Some of the power stations need upgrading and major rehabilitation to meet the growing consumer demand in the townships.
tunaweza kuongeza kwa kubadilisha na kutumia mitambo ya umeme wa upepo na jua?

Tunaweza kuwekeza Umeme nchi nzima n akuondokana na Tanesco kama tukiruhusu kwa nia ya kweli kuwepo kwa ushindani wa ufuaji umeme na usambazaji.

Mathlani na hili ni poendekezo langu ni kwa kila wilaya kuwa na uwezo binafsi wa kuzalisha si chini ya megawati 20 za umeme kutumia umeme wa Upepo.

Mapendekezo yangu ni kwa Wilaya hizi kuchukua hatua kupitia vyama vya ushirika, bodi za biashara na wananchi wenyewe kuwa wamiliki na wazalishaji wa umeme huu. Mtaji wao unawezekana kupatikana kwa kutoa Bond au Treasury Bill ya miaka 10 pale BOT, na wakanunua mitambo ya umeme wa upepo na Jua au hata kama ni wa gesi ya makaa ya mawe (kiwira will be the supplier) au Jatropha (nitaliongelea hapo chini).

Ikiwa kila wilaya inaweza kuzalisha umeme mwingi na waziada, kama nilivyozungumzia suala la Zanzibar hapo juu, basi kila nyumba, shule, ofisi, hospitali, zahanati zitakuwa na umeme na uwezekano wa kuwa na viwanda kuongezeka na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta ya Diseli katika kuzalisha.

Kitendo hiki cha kusambaza umeem na kuhakikisha umiliki ni wa wananchi wenyewe kwa kuuziwa na kununua hisa katika mradi, kitakuwa ni kitendo cha kishujaa na cha msingi katika kuleta utatuzi wa muda mrefu kwa tatizo sugu la umeme. Umeme wa ziada ambao hautatumika, basi utaunganishwa kwenye gridi la Taifa na kuuzwa kwa wale wenye kuhitaji umeme mwingi zaidi.

Nimeongelea Jatropha hapo juu na hasa ukizingatia kuwa sasa hivi, kuna wawekezaji wengi wa nje ambao wanakuja Tanzania kununua na kukodisha ardhi ili wazalishe mmea wa Jatropha ambao ni chanzo cha mafuta yanayoweza kutumika badala ya mafuta ya uarabuni.

Kwa sasa hivi na bei za mafuta kushuka duniani, Jatropha inaonekana kama ni biashara ambayo haitalipa.

Lakini sisi tuna nafasi basi kulima Jatropha kwa wingi, na kuizalisha kuwa mafuta ya viwanda na kutumika kuzalisha umeme na kuachana na matumizi ya Dizeli.

Pendekezo langu ni kuhakikisha kuwa tuna ukulima stadi wa Jatropha ambao hautatuletea tatizo la njaa kutokana na wakulima kuacha kulima mazao ya chakula au mazao mengine ya biashara ;pamba, tumbaku n.k.

Tutumie nyenzo za ndani iwe ni SUA, TBS au TPDC na UDSM kuweza kuwa na uzalishaji wa kusindika Jatropha na kuzigeuza kuwa mafuta ya kuendesha mitambo.

Hili si kwamba litatupunguzia gharama za kuagiza mafuta pekee, bali litatoa ajira kwa wajasirimali na wawekezaji wa ndani, ukianzia na wakulima mpaka viwanda vy akuzalisha mafuta. OKwa uziada tuu, machicha ya Jatropha yanaweza kuwa ni mbolea au chakula cha wanyama kama Ng'ombe, Kuku, Kondoo, Mbuzi hata Nguruwe na Farasi.

Hivyop basi tukiweza kuwa na Tanzania yenye umeme thabiti na wenye kusambaa kila kona, basi hatua zetu za maendeleo zitasonga mbele na hizi mbio za kuhujum nchi ambazo zilianza nyakati zile za majenereta ya petroli kwa kila nyumba na sasa hivi mkorogano wa IPTL, Kiwira, Richmond an mengineyo ambayo hatuyafahamu, yatapungua.
 
Dondoo..

Tanzania



Geothermal as an Alternative Source of Energy for Tanzania
TanzaniaMapKomplet.gif

Tanzania is endowed with a huge geothermal potential which has not been used by now, and has only been explored to a limited extend. Experiences in the neighbouring country Kenya show that geothermal power is a reliable low-cost alternative for energy supply in East Africa.
The Government of Tanzania intends to diversify the country's energy mix and is looking for alternative sources of energy. Currently, the national power system is mostly relying on hydropower. A long period of drought between 2003 and 2006 leaded to shortfalls in electricity supply from the hydropower stations. Hitherto power generation of TANESCO (Tanzania Electric Supply Company Limited) depended on hydro by almost 90% and on thermal generation by only 10%; this generation pattern was switched to 30% dependence on hydro and 70% on thermal due to the dwindled water inflows into the dams. As a consequence of the cost intensive thermal power generation, by 1st of June 2006, TANESCO increased the power tariffs by 5%.
Figure 1: Songwe geothermal prospect is located about 20 km west of Mbeya, which is the third-largest city in Tanzania.
Geothermal power generation is regarded as one opportunity to contribute to stabilising energy supply and energy prices. Thus, the Ministry of Energy and Minerals of Tanzania ( MEM ), the Geological Survey of Tanzania ( GST ) and BGR initiated a project in the frame of the GEOTHERM programme to pave the way for using the country's geothermal energy resources. The activities of the GEOTHERM project "Geothermal as an Alternative Source of Energy for Tanzania" started in June 2006.

The project is aimed to initiate a successive expansion of the geothermal power sector in Tanzania. Main components of the project will be:
  • Training of Tanzanian experts in acquiring, analysing and interpreting exploration data
  • Recommend potential locations for a geothermal exploration borehole in Songwe on the basis of modern geothermal exploration methods
  • Enabling MEM and GST to continue with geothermal exploration works
  • Dissemination of information about possibilities of geothermal energy use in Tanzania among decision makers
  • Search for funding for shallow drilling in Songwe
Tanzania_fig02_www.jpg

In May 2006, the project team (Figure 3) carried out an assessment of promising geothermal sites in the SW area of Tanzania and agreed to focus detailed investigations on the Songwe geothermal prospect.
Songwe is located about 20 km west of Mbeya, which is the third-largest city in Tanzania. Mbeya is a fast-growing city with a high energy demand. The prospect is only a few kilometres away from the national grid (Figure 2). Songwe is an impressing geothermal site: Several hot springs emanate near the river of Songwe, with temperatures between 50 and 80°C and flow rates of 50 - 75 kg per second. Former estimations of the geothermal reservoir temperatures in the subsurface indicate temperatures of up to 255°C. These studies concluded that the Songwe hot springs are the outflow of a geothermal reservoir which might be located far away from the springs. A large volume of travertine (Figure 3), which is deposited at the Songwe hot springs, points to a long depositional history. It was concluded that the Songwe geothermal prospect is a significant geothermal resource with promising indications to be viable for electricity production.


Figure 2: Small hot spring at a clearly visible fault where strong hot spring activity in the past has built up an impressive travertine ridge in the Songwe area.

Tanzania_fig03_Crew.jpg

MEM, GST and BGR will carry out detailed geological, geochemical and geophysical investigations to assess the Songwe geothermal prospect and to locate a geothermal reservoir. It is planned to have a first field survey in November 2006. In the end of the project the project team plans to recommend potential locations for geothermal exploration drilling.




Figure 3: The Project team in front of Lake Nyassa (back row from left): Lightness Mnzava, Katrin Kessels, Abdul ???, , Christopher Stadtler, Michael Kraml, Isdory C. Fitwangile, Lucas Rurataze; (front row from left): Festo ???, Paul B. Ndonde, Gerald ???


Contact:
Eng. Ngosi Mwihava , MEM, Tel. +255 22 2119159
Eng. Paul B. Ndonde , GST, Tel. +255 26 2324943
Dr. Ulrich Ranke , BGR, Tel. +49 511 643 2647
BGR – Geotherm Programme – Projects – ...
 
This is a fact - Plessey Engineering ya Uingereza kwenye miaka ya sabini, ilijaribu kwa kufanya mabadiliko katika uongozi wake na kupendekeza kuwa ili ufanisi uongezeke, nafasi ya CEO mpaka wakurugenzi mbalimbali zishikwe na mainjinia. Matokeo ya zoezi hilo yalielezeka kwa neno moja tu "disaster". Within one year kampuni ilikuwa inachungulia kaburi na hao walioitwa mangwini ilibidi watafutwe haraka kuifufua Plessey. Toka wakati huo iliamuliwa kuwa ni busara zaidi CEO wa Plessey asiwe Engineer - lakini kamwe asithubutu kupuuza bali azingatie ushauri wa wataalamu (Engineers).

Mimi ni engineer by profession.

Je ushauri wa mainjinia unasikilizwa ipasavyo ktk Tanzania!? Na isitoshe hakuna mtu anayependekeza mainjinia washike nyadhifa kama CEO n.k bali wasikilizwe, kwani wao ndio wataalamu....nadhani wana ideas better than hiyo kununua upuuzi wa Dowans!

Mimi nipo ktk sekta ya afya na si injinia!
 
Back
Top Bottom