Umeme na Nishati: Tatizo sugu Tanzania

Umesahau Uranium inaokotwa kwa vipolo !

Hapana kaka sio siku hizi. Wachukuaji (wawekezaji) wakubwa wameshaingia kuanzia hazina ya MAKETE, Mgeta hadi kusini. Na sasa tunashugulikia sera maalumu ya kuvutia uwezekaji zaidi/salama huko. Ule ulaji wa MCC una mkono wake hapo.

omarilyas
 
Siku hivi ziko kwenye Leadership, withouth leadership, management becomes void.

You lead people and manage process. Sasa sisi tuna hao combo ambao ni managelead ambao ni watupu kabisa upstairs.

Kaka umegusia suala nyeti.

Wakati tulipokuwa tunaanza kula vidonge LIBERALIZATION tuliamua kuachana na dhima ya ujenzi wa viongozi wajao katika sekta ya elimu. Tukaamua kutilia mkazo katika kile tulichoita "employability in globalized market" Mfano mzuri ni mabadiliko yalitokea UDSM. Ofcourse ujenzi wa viongozi wajao unaendana na ujenzi wa uzalendo. Sasa katika kutimiza mikakati ya LIBERALIZATION uzalendo kwa nchi ukageuka kuwa "ukorofi" na "uzamani". Sasa matokeo yake tumeshindwa kuzalisha hicho kizazi cha "imployability in globalized market" na tukafanikiwa kujenga "MFUMO FISADI" unaothamini uzalendo wa kitabaka usiojali maslahi ya taifa.

omarilyas
 
Haya ni maneno yako kutoka mtaa wa pili hukoo, "But who am I to talk power and energy while I am not an expert in engineering or energy but mbwabwajaji?" mwisho wa kunukuu. Rashidi, Nyepesi (Zitto) na karibu major players wooote ktk timbwili hili ni wabwabwajaji tu kama wewe, mna zero expertize ktk masuala ya umeme.........nimekosea?

Dogo YNIM,

On second thought, since you are so imersed into your chemucal sniffing life of engineeering or science, your lack of ungwinizm, failed to understand the Ngwini talk you have quoted above.
 
Maswali mengine bwana, utafikiri ule mchezo wa luninga wa sabuni ya OMO... ulikuwa unasema 'Money or Box'
 
Nchi ikiingia kizani sijui itakuwa kwa muda gani makampuni mengi yatasimamisha uzalishaji, kupunguza kwa kiasi kikubwa utendaji wake wa kila siku. Hili litasabiasha baadhi ya makampuni hayo kupunguza wafanyakazi aua kufunga kabisa viwanda vyao na matokea yake kodi zinazokusanywa na serikali toka makampuni na viwanda hivyo na wafanyakazi waliojiriwa huko yatapungua sana na kuathiri bajeti ya serikali na mipango yake mingi (kana wana mipango yoyote inayoeleweka na Watanzania). Tukikosa vitambulisho kwa maoni yangu tutakuwa tumeokoa shilingi bilioni 200 kama nchi tumeweza kuishi miaka 48 sasa bila vitambulisho na hakukuwa na matatizo yoyote yale, lakini tukikosa umeme hata kwa miezi sita tu athari zake ni kubwa mno.

Pole sana kwa analysis yako dhaifu sana... suala la vitambulisho lina umuhimu mkubwa na faida kubwa zaidi ya kusema sijui tumeokoa Bil.200

Ucheleweshaji wowote wa vitambulisho ni kuchelewesha maendeleo ya wanyonge ambao mfano... benki zinataka kuwakopesha lakini zinawaogopa kwa kuwa it is difficult to identify them. Faida ni nyingi sana...

Hata hivyo ni upuuzi kulinganisha hayo masuala mawili
 
At this moment in time Tanzania needs to concentrate on setting targets and strategies that will improving micro-economic. It needs to focus on what will enhance trades and investment at micro and macro levels (long term). If we can have a good budget on investing on

1. Power
2. Integrated Transport
3. Environment
4. Education and Health

We can see our economy grow with time and once it is grow then we can think of national identity card and so on. I personally work and do research on applied economy and sustainable developments and from my own working and research experience in these types of industries I can say that Tanzania does lack good leadership and public awareness. (Well Possible our countries leaders are being mislead by their advisers but again the leaders needs to have broad knowledge on this issues.. please correct me if I am wrong).

We all know (even a primary school student) having sufficient power supply will guarantee 24/7 productive work ours both in government and private sectors but still no one sees this has a priority issue??

Coming to the issue of transport, for years, Tanzania government has been focusing so much into road transport and it has forgotten what rail transport can play in reducing congestion and ensuring safety and quicker transit between inter-regional. Good and integrated transport will always allow more people to engage into trade especial in a country which we depend on agriculture and mining like Tanzania.

Nevertheless, all the above will always have to work with good Environment policies as well as having strategic plans… which I can confidently say Tanzania has very poor environment policies while it has very much to protect!! (What do our PMs do in the parliament? Just using tax payers' money?)

Personally, I do believe what we need in Tanzania is leadership with knowledge and expertise in economy and knowledge of sustainable developments. At the moment our country is just been run by mimicking developed countries which is ridicules!! The government and people always forget each country is different and mostly because of culture, economic and political influences and hence an economic solution in one country will hardly work in another as people are different and mostly will respond to a solution in different manner!!

We have seen a lot of new government agencies which deals with economic issues at the end of 1990's and beginning of 2000's and now it is almost 10 years down the line with no change! This is definitely not because of education but it is because of lack of competent on manpower as well as working strategies.
 
Pole sana kwa analysis yako dhaifu sana... suala la vitambulisho lina umuhimu mkubwa na faida kubwa zaidi ya kusema sijui tumeokoa Bil.200

Ucheleweshaji wowote wa vitambulisho ni kuchelewesha maendeleo ya wanyonge ambao mfano... benki zinataka kuwakopesha lakini zinawaogopa kwa kuwa it is difficult to identify them. Faida ni nyingi sana...

Hata hivyo ni upuuzi kulinganisha hayo masuala mawili[/Q

Kasheshe,

Vitambulisho sio maendeleo ya mngonge, unafiri kukopa hela benki ni maendeleo? culture ya buy today pay tomorrow, itafanya wangonge waendelee kuwa wanyonge na matajiri waendelee kuwa matajiri, ita endeleza classes tanzania. Pia kwanini passport zisitumike kama identity? Tanzania ni masikini inabidi wajue kumanipulate budget ya nchi ili kufanya mambo ya maana ambayo yataleta maendeleo kwa wote. Vitambulisho faida zake ni ndogo mara kumi iyo ila itumike kujenga urban railway isaidia congestion ya dar!!
 
Mkurugenzi wa Tanesco abanwa ajiuzulu kwa kashfa ya Dowans

Na Geofrey Nyang'oro

SIKU moja baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kutangaza kususa ununuzi wa mitambo ya Dowans, wasomi, wanasiasa na wananchi nchini wamezidi kumkaba koo Mkurugenzi wa shirika hilo, Dk Idrisa Rashid ajiuzulu.


Watu hao wanataka, Dk Raishid ajiuzulu kutokana na kauli yake ya kueleza kuwa kwa vile watu wengi hawataki mshirika lake linunue mitambo ya Dowans basi asilaumiwe kama nchi itakuwa giza.


Sambamba na hali, Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kumwonfdoa katika wadhifa wake Waziri wa Nishati na Madini, Wiliiam Ngeleja na kuvunja menejimenti nzima ya Tanesco.


Maneno yaliyomweka pabaya Dk Rashid aliyasema juzi katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa Shirika lake, likisema lisibebeshwe lawama kwa yatakayotokea.


Alisema wananchi wa Tanzania watafanya maamuzi yao hapo ambapo nchi itakapokuwa imegubikwa na kiza, mahospitali hayatoi huduma; viwanda havizalishi, wanafunzi vyuoni wanashindwa kusoma kwa sababu ya kushindwa kufanya maamuzi.


Uamuzi wake huo umekuja siku mbili baada ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta kueleza kuwa msimamo wa kamati ya Nishati na Madini iliyoshauri mitambo hiyo isinunuliwe ndio msimamo wa chombo hicho cha kutunga sheria na hivyo kumaliza mvutano uliokuwepo kati ya kamati hiyo na ile ya hesabu za mashirika ya umma, inayoongozwa na Zitto Kabwe iliyounga mkono kununuliwa kwa mitambo.


Mtaalamu wa Ugonjwa ya Ukimwi, Dk Fedelis Owenya aliliambia Mwananchi Jumapili jana kwa njia ya simu kuwa kauli ya Dk Rashid inaonyesha jinsi gani kiongozi huyo aliyeteuliwa kumsaidia rais ameshindwa kufanya kazi yake.


Alisema Dk Rashid amekiuka misingi ya kazi yake ambayo ilikuwa ni kuandaa mipango ya muda mufupi na muda mrefu ya upatikanaji wa umeme na kuishauri serikali, badala yake sasa ameamua kushinikiza kununuliwa kwa mitambo hiyo na kutoa vitisho kwa wanachi na rais wake.


Kauli kwamba anawaachia wananchi kuamua wenyewe pindi nchi itakapokuwa kuwa giza ni vitisho vinavyoitaka serikali kuvunja hata sheria ya manunuzi, kitu ambacho kinaonyesha kuwa kuna nguvu nyuma yake.


Alisema hatua aliyoichukua Mkurugenzi huyo inaonyesha kuwa hujuma nzinaweza kufanywa ili kukomoa wananchi, hivyo, hatua zaidi zinafaa kuchukuliwa dhidi yake.


"Hii ni nchi ya kidemokrasia,sisi tumemchagua rais na tumempa dhana ya kutuongoza,yeye kwa nafasi yake amewachagua watu watakaomsaidia katika suala zima la utendaji ili nchi iweze kuendelea,Dk Rahidi aliyeteuliwa na rais kushika nafasi hiyo, anawatishia wanchi au anamtishia rais aliyempa nafasi hiyo?alihoji Dk Owenye na kutongeza kuwa watu wa aina hii wanapaswa kushitakiwa.


Owenya aliiasa Serikali kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na sheria ya ununuzi wa umma ili kutunza na kuendeleza heshima na usitawi wa nchi na jamii yake.


Kwa upenda wake, Tundu Lisu ambaye ni mwanasheria licha ya kumtaka Dk Rashid awajibishwe pi alipendekeza uwepo uwajibikaji kisiasa na kuwataka waliomteua wawajibishwe pia.


Hayo aliyezesema juzi alipokuwa akichangia kwenye kipindi cha Kipamajoto kinachorushwa hewani na Kituo cha Television cha ITV.


Alisema kitendo cha kulazimisha ununuzi wa mitambo hiyo wakati akijua kuwa ni mitumba ni kuwatukana watanzania.


Lisu alipinga kuwepo kwa dhararu ndani ya shirika hilo na kueleza kuwa ni uharamia ulipangwa kufanyika ndani ya shirika hilo kwa kuwa wao walijua tangu siku nyingi.


Alisema kimsingi kampuni hiyo inapaswa kufikishwa mahakamani kutokana na mkataba wake kuwa tata anashangaa kuona mpaka sasa suala hilo halijafanyika.


Katika hatua nyingine mwanaharakati, Renatus Mpinga alimtaka rais Jakaya Kikwete kumwajibisha Mkurugenzi huyo haraka kwa kuwa ameonyesha utovu wa nidhamu mbele ya watanzania.


Alisema kitendo chake cha kulazimisha ununuzi wa mitambo hiyo kinataka kutonyesha kuwa mitambo hiyo ndiyo bora kuliko mengine.


Naye Mtaalamu wa sheria ya Manunuzi ya Umma, Wasonga Benjemani alisema sheria ya manunuzi inaeleza wazi kuwa mzabuni akionyesha dalala za kutumia rushwa katika kupata tenda yake anatakiwa kusimamishwa kushiriki katika kufanya biashara ya serikali kwa muda wa miaka kumi au kufikishwa mahakamani.


Alisema kitendo cha Taneseco kunuia kununua mitambo hiyo iliyozua mashaka hapa nchini ulikuwa ni ukiukwaji wa wazi wa sheria zilizopo.


Naye Joyce Mmasi anaripoti Mbunge wa Vunjo Aloyce Kimaro amesema watu watakao liingiza taifa katika ununuzi wa mitambo ya Dowans washitakiwe na kufungwa jela.


“Ule wakati wa kukosea na kujiuzulu umepitwa na wakati, sasa hivi ni mahakamani kwa wote waovu, wazembe na wanaotumia madaraka yao vibaya, sasa ni kufungwa sio kujiuzulu,” alisema.


Alisema serikali iache kutumia baadhi ya wabunge kuhalalisha uzembe. “Tujiulize hivi huku Tanesco kuna nini hadi kutaka kuvunja sheria? Haiwezekani kampuni ambazo zilizoifanya serikali nzima kujiuzulu leo tunaendelea kuzifuata,” alisema Kimaro.


Kimaro alisema anashangazwa na kitendo cha mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya kusimamia hesabu za mashirika ya umma alivyolikomalia suala hilo.


Naye Burhani Yakub,Tanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Dk Idriss Rashid,amelalamikiwa kwa kauli aliyotoa wakati akijiondoa katika ununuzi wa mitambo ya Dowans Tanzania Limited ya kuwa ikiwa nchi itakuwa giza asilaumiwe.



Wananci waliohojiwa nya kati tofauti jijini hapa jana , wamesema kauli hiyo haikupaswa kutolewa na kiongozi kama yeye kwa kuwa inatoa mwanya kwa watumishi wasiokuwa na uaminifu wa Tanesco kufanya hujuma.



Malalamiko hayo waliyatoa jana kwa nyakati tofauti wakati wakielezea maoni yao juu ya kauli ya Dk Rashidi aliyotoa kwa waandishi wa habari kuelezea kujito kwa Tanesco katika ununuzi wa mitambo ya Dowans.



"Asitufanye wananchi ni wajinga,inakuwaje wang'ang'anie kununua mitambo ya Dowans ilhali wanafahamu kuwa ni mikongwe?halafu anaamua kususa baada ya Kamti ya Bunge ya Nishati na madini kuweka msimamo wake"alisema Khamisi Ali mkazi wa Makorora Jijini Tanga.



Mustafa Shembeyu wa Barabara ya 15 Jijini Tanga,alisema kauli iliyotolewa na Dk Idriss inaonyesha kuwa ameshindwa kuliendesha shirika la Tanesco hivyo anastahili kujuzulu ili kuepusha madhara kama ataendelea kuwepo.



"Ili kuinusuru Tanesco inabidi Dk Idriss ajiuzulu,kwani kwa kauli yake inaonyesha kuwa mwisho wake wa kushauri umefikia kwa Kampuni ya Dowans na kwamba hana njia nyingine ya kuweza kutafuta ufumbuzi wa tatizo la umeme nchini"alisema Sembeyu.



Kiongozi wa umoja wa vyama vya upinzani Wilaya ya Korogwe,Calistus Shekibaha,alisema baada ya kusikia kuwa Rais Jakaya Kikwete amemteua Dk Idriss kushika wadhifa huo alipata wasiwasi kwa kuwa ndiye anayeshutumiwa kuivuruga hata benki ya NBC.



"Kwa wale wenye mazoea ya kusoma magazeti watakumbuka mara baada ya uteuzi wa Idriss nilitoa maoni yangu katika gazeti la Mwananchi na kumwambia Rais atavuna machungu kwa kitendo chake cha kumteua Dk Idriss kuongoza Shirika nyeti kama Tanesco.



Alisema wakati Dk Idriss akiwa NBC watumishi walimlalamikia kuwa alikuwa akiendesha benki hiyo kimabavu na kusababisha mabo mengi kuharibika jambo lililosababisha wamkumbe Mkurugenzi wao wa zamani Amon Nsekela.



Shekibaha aliipongeza Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli,William Shelukindo kwa msimamo walioonyesha katika kutetea mitambo ya Dowans isinunuliwe.



Aliitaka Serikali kutafuta mbinu za ununuzi wa mitambo mipya ili kumaliza kabisa tatizo lililopo kwani ni jambo la iabu kwa nchi ya Tanzania kuhangaikia umeme wakati ina vyanzo vingi.
 
Taifa letu liachwe kuendeshwa kiuenda wazimu!. Ni muhimu sasa watanzania waone ukweli kuliko kukubali kudanganywa tena na kuchonganishwa na wabunge waliowachagua kwa ajili ya kulinda masilahi ya watu wachache.
Yaani ndiyo kusema mitambo ya Dowans isiponunuliwa nchi itawekwa gizani ili tu kuwadhibitishia wananchi kuwa wabunge wao wamekosea kutokubali matakwa ya Menejimenti ya Tanesco!!. Tanesco haina vision yoyote nje ya kufanya dili na Dowans. Watanzania tusikubali tena kunyanyaswa na watu waliowekwa madarakani kwa ajili ya kututumikia sisi na tena wanalipwa kwa kodi zetu.
Nasubiri kwa shauku siku Tanesco watakapotuweka gizani kuona kama rais atakuwa upande gani. Atamtimua Dr. Idrisa Rashid? au atakaa kimya wananchi wakae gizani akiwa na uhakika kuwa ikulu haitakosa umeme?.
 
DR. Rashid akisema nilisha offer kujiuzulu rais akakataa watu watasemaje?


The buck stops at Kikwete's desk, not Dr. Rashid's.
 
DR. Rashid akisema nilisha offer kujiuzulu rais akakataa watu watasemaje?


The buck stops at Kikwete's desk, not Dr. Rashid's.
__________________

Kiranga: hapo awali alikuwa anatikisa tu kiberiti -- kuangalia uswahiba wake na JK umekaa vipi. akagundua umekaa barabara -- hivyo akapata kaujeuri ka-kuwatukana Watanzania na kutoa vitisho kwamba mkikataa mitumba hii ya Dowans mtalala giza.... Huyu mtu anaweza hata kufanya hujuma kwa kuagiza kukatwa kwa umeme kutimiza lengo lake.

Hujuma ndiyo zake -- alihusika kashfa la kuanguka kwa benki ya kwanza ya kigeni nchini -- Meridien Biao mapema 1994 -- kuchapisha noti mbovu za 1,000/- mwaka 1998 na hilo la rada.

Kuhusu Meridien Biao -- mchakato wake wa kuirithisha benki hiyo kwa Stanbic mwishoni mwa 1994 ulifanyika wakati JK akiwa Waziri wa Fedha na inasemekana uliendeshwa kwa kifisadi.
 
As TANESCO abandons dubious Dowans deal: Ngeleja, Dr Rashidi face public backlash

Energy and Minerals minister William Ngeleja
-And Zitto Kabwe continues to support turbines idea

THISDAY REPORTERS
Dar es Salaam


CALLS are on the rise for both Energy and Minerals Minister William Ngeleja and Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) Managing Director Dr Idris Rashidi to step down or otherwise be made accountable by the government should the nation be plunged into a new power crisis simply because the Dowans deal failed to take off.

The calls appeared to become stronger yesterday even as Rashidi announced at a morning news conference in Dar es Salaam that TANESCO was now abandoning its quest to convince the government to buy the used power turbines on offer from Dowans Tanzania Limited.

In his prepared statement laden with threats of a looming power crisis, Rashidi said the argument offered by the state-run power utility to justify the purchase of the controversial turbines was being ignored at the nation's own peril.

Asserted he: ''TANESCO would like to announce that it is withdrawing its intention of buying this (Dowans power) plant. We believe we adequately presented our case, and that the people of Tanzania will draw their own conclusions once the nation is engulfed in darkness, hospitals are left without health services, factories shut down, and students at institutions of higher learning start missing classes, simply because we were not decisive enough.''

He said TANESCO was withdrawing because the matter had become 'politicised,' and left the room abruptly after reading the statement, declining to respond to questions thrown at him by journalists as he departed.

But shortly after the remarks of the TANESCO boss were made public, a number of local commentators responded by voicing fresh fears of a possible conspiracy and sabotage to deliberately plunge the nation into a crippling power crisis - just to try and prove the Dowans turbines purchase bid as being the best option after all.

Contacted by THISDAY for comment, the chairman of the parliamentary energy and minerals committee, William Shellukindo - one of the fiercest critics of the proposed Dowans deal from the outset � said he was shocked by Rashidi's assertion suggesting that this could indeed turn out to be the case.

Shellukindo raised concern over possible sabotage actions by TANESCO executives disgruntled by the fact that the Dowans deal had been blocked, and who could therefore go ahead and plunge the country into darkness.

''It is up to the government to take stern disciplinary measures against him (Rashidi)...the chief executive officer of a public institution cannot be allowed to make such a statement that seems aimed at sending the public into unnecessary panic,'' the Bunge committee chief asserted, querrying further:

''Is TANESCO planning to sabotage the national power grid?''


According to Shellukindo, the country has sufficient infrastructure to produce over 1,000 megawatts of electricity, thus there is no need at all to rely solely on the Dowans turbines.

Also reacting to Rashidi's latest statement, prominent Dar es Salaam lawyer Mabere Marando minced no words in calling for the immediate dismissal of the TANESCO boss.

''I urge President Kikwete to sack him and give that job to someone else...there are many other competent people out there who can run TANESCO,'' Marando told THISDAY.

He suggested that the TANESCO boss appeared to have given his statement out of frustration, and questioned the real reasons for this.

''What was he (Rashidi) expecting to get out of that deal that has led him to make such a remarkable public statement?'' Marando remarked.

He said if indeed the nation is plunged into another power crisis, Rashidi will have to resign because of his failure to make proper contingency plans well in advance.


Another city-based lawyer and activist, Tundu Lissu, described Rashidi's statement as ''simply shameful.''

''Tanzanians will hardly blame him if he resigns from his position immediately to allow competent individuals to do their work,'' he said, suggesting that Rashidi should go ahead and resign if he truly believes that Dowans was the sole solution for the country's energy needs.

''If he still refuses to step down, he won't have any excuse should the country indeed be plunged into power blackouts,'' Lissu added.

The Legal and Human Rights Centre (LHRC), meanwhile said in a statement issued late yesterday that there seemed to have been ''a lot of pressure for the government to buy the (Dowans) turbines for the personal gains of a few individuals.''

''This also demonstrates weaknesses on the part of TANESCO lacking long-term strategies to ensure sustainable power supply in the country,'' said the statement issued by LHRC Executive Director, Francis Kiwanga.

In some quarters, criticism was as equally scathing on minister Ngeleja as on Rashidi.

''The sacking or resignation of Dr Rashidi is not the only solution...he is not alone in this rot, even the energy minister (Ngeleja) should go,'' said Peter Manchari, a Dar es Salaam resident.


Both the minister and the TANESCO chief had vigorously pushed for the purchase of the used 100MW thermal power plant from Dowans, despite the fact that the private company had inherited the same equipment from the fraudulent and long-disgraced Richmond Development Company LLC.

Meanwhile, the chairman of the parliamentary public accounts committee (PAC) Zitto Kabwe, in his own statement posted on the Internet late yesterday, steadfastly continued to support ''in explicit terms'' TANESCO's idea of ''acquiring gas-fired turbines to improve electricity generation to the country.''

''I stand firm to my decision, and am ready to be held accountable for that,'' Kabwe said.

He said he was maintaining his position in good faith, and that he was ''genuine and honest.''

''People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information I have - technical information. So long as I reached this decision without any influence whatsoever, I stand by it,'' the maverick opposition politician said.


The PAC committee chairman said he believed TANESCO's arguments had a solid foundation, while those of the energy and minerals committee under Shellukindo were just 'political' arguments.
 
Na Saed Kubenea
Mwanahalisi~Maslahi ya Taifa Mbele

KELELE za sasa ndani ya serikali kuhusu ununuzi wa mitambo ya Dowans ni jitihada zinazolenga "kukidhi maslahi binafsi," MwanaHALISI limegundua.

Vyanzo mbalimbali jijini Dar es Salaam na mikoani vimeonyesha kuwa hakuna tatizo la umeme hivi sasa nchini; wala hakuna upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme.

Uchunguzi wa gazeti hili sasa unathibitisha kuwa madai ya serikali, kwamba nchi karibu itaingia gizani kutokana na ukosefu wa umeme, hayana msingi wowote.

Kwa wiki nzima sasa serikali, ikishirikiana na Shirika la Umeme la Taifa (TANESCO) wamekuwa wakitoa tahadhari kuwa iwapo mitambo ya umeme ya kampuni ya Dowans haitanunuliwa mara moja, taifa litaingia gizani wakati wowote kuanzia sasa.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema serikali ina nia ya kununua mitambo ya Dowans ili kukabiliana na tishio la uhaba mkubwa wa umeme kutokana na mabwawa kukauka.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dk. Idris Rashid amesema kwamba mahitaji ya umeme yameongezeka nchini na kwamba kinachohitajika ni serikali kununua mitambo yote ya Dowans pamoja na vifaa vyote vya kuunganishia kwenye gridi ya taifa.

Hata hivyo, taarifa ndani ya TANESCO zinasema vyanzo muhimu vya nishati hiyo, ambavyo ni mabwawa ya maji, bado viko imara na maji yako kwenye viwango thabiti vya kuzalisha umeme.

Kwa mfano, hadi juzi Jumatatu, bwawa la Mtera mkoani Dodoma lilikuwa na maji ya kutosha ya kuzalishia umeme.

Kima cha juu cha ujazo katika bwawa la Mtera ni mita 698.50 na kina cha chini kwa ajili ya uzalishaji umeme ni mita 690.00. Lakini hivi sasa Mtera ina ujazo wa mita 695.91.

Hii ina maana kwamba kile kinachoitwa, "tishio la mabwawa kukauka," hakipo katika bwawa hilo. Kinachoonekana kuwa upungufu, wataalam wamesema, hakiwezi kuleta athari yoyote kubwa katika miezi ya karibuni.

Hali kama hiyo ipo katika bwawa la Kidatu mkoani Morogoro. Hadi juzi Jumatatu, maji katika bwawa hilo yalikuwa mita 449.37. Kima cha juu cha maji kwa Kidatu ni mita 451.00 huku kima cha chini ni mita 441.00.

"Kwa maana hiyo, mpaka sasa, na kutokana na takwimu hizi, hakuna ushahidi wa mabwawa hayo kukauka au kuwa hatarini kukauka," amefafanua injinia mmoja wa TANESCO makao makuu, Dar es Salaam.

Aidha, Mamlaka ya Hali ya Hewa imetangaza kuwa mvua kubwa zimeanza kunyesha katika mikoa ya Iringa, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga.

Wataalamu wa TANESCO wanasema ni mvua hizo ambazo zitajaza mabwawa ya Mtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu, Kidatu na Hale kabla ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu.

"Kwa mvua hizi zinazonyesha," kimeeleza chanzo chetu cha habari, "huenda zikalazimu TANESCO kuachia kingo za mabwawa na kuachia maji yatoke ili kuzuia yasibomoke."

Hadi Jumapili iliyopita, Waziri Ngeleja alikuwa ameanza kampeni kubwa akidai kuwa kununua mitambo ya kuzalisha umeme ya Dowans "siyo kufanya ufisadi" bali ni kuweka maslahi ya taifa kwanza.

Katika wimbo huo, Ngeleja aliungwa mkono na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe ambaye alisema anaweka mbele "maslahi ya taifa."

Lakini ni Ngeleja aliyeliambia bunge, zaidi ya miezi mitatu iliyopita, kuwa serikali haiwezi kununua mitambo hiyo kwa kuwa imetumika na kwamba kufanya hivyo ni kukiuka Sheria ya Ununuzi wa Vifaa na Huduma serikalini ya mwaka 2004.

Katika haraka isiyo ya kawaida, serikali na TANESCO wametupilia mbali ushauri wa Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge na kudandia Kamati ya Zitto wakidai wanatafuta bunge liwaruhusu kununua mitambo ya Dowans.

Kamati ya Nishati na Madini ilishauri TANESCO kufanya kile ambacho wanaona kimo katika uwezo na uamuzi wao. Dowans ni sehemu ya sakata la Richmond ambalo maazimio ya Bunge juu yake hayajatekelezwa na serikali.

Hata hivyo, bado serikali inakabiliwa na mgogoro wa nani hasa wajadiliane naye katika kununua mitambo ya Dowans iliyoko Ubungo, Dar es Salaam.

MwanaHALISI imebaini kuwa wakati kampuni ya Dowans ilikuwa inaweka mitambo yake na baada ya kuanza uzalishaji, haikuwa na ofisi nchini na wala mmiliki wake halisi alikuwa hajulikani.

Hadi sasa, Bunge ambalo liliunda Kamati Teule kuchunguza mkataba wa kampuni ya Richmond iliyokabidhi shughuli zake kwa Dowans, halifahamu mmiliki wa Dowans.

MwanaHALISI imegundua kuwa kuna kampuni inayoitwa Dowans Holdings SA (DH-SA) iliyosajiliwa nchini Costa Rica, Amerika ya Kusini, tarehe 1 Julai 2005 na kwamba ndiyo yenye uhusiano na Dowans iliyoko Ubungo.

Kampuni ya DH-SA ilianzishwa na mtu mmoja aitwaye Bernal Zamora Alce. Taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo gazeti hili limeona, zinaonyesha Zamora alisajili Dowans na makampuni mengine 99 yanayoishia na herufi "SA," kwa siku moja.

Taarifa zinasema kati ya makampuni hayo 100, Zamora alijitangaza kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika makampuni 52.

Hata hivyo, pamoja na utitili huo wa makampuni, imefahamika kuwa Zamora hana simu ya mkononi, hana sanduku la barua wala hajulikani mtaa anakoishi.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari wa kimataifa na wanasheria mashuhuri nchini Costa Rica umegundua kwamba kampuni ya Dowans haikuwa na ofisi nchini humo haikuwa na simu wala gari.

Si nchini Costa Rica tu, bali kampuni ya Dowans yenye mitambo Ubungo, kwa mujibu wa taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, haikuwa na namba za simu wala ofisi; wafanyakazi wake walikuwa wanatumia ofisi za kampuni ya Caspian Limited hapa nchini.

Kampuni ya Caspian inamilikiwa na mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz. Ni Rostam aliyethibitishia Bunge kuwa Dowans ilikuwa inatumia anuani zake.


Katika andishi lililotumwa serikalini na Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Costa Rica, kuitahadharisha serikali ya Tanzania kuhusu Dowans anasema, "Dowans ni kampuni ya mfukoni iliyoanzishwa mahususi kwa ajili ya kufanya kazi maalum."

Katika mazingira haya, Dk. Rashid alipoulizwa TANESCO inajadili na nani kuhusu ununuzi wa mitambo, alijibu haraka kuwa wao hawafanyi majadiliano bali wamepeleka mapendekezo serikalini. Alisema ni serikali yenye jukumu la kununua au kutonunua mitambo hiyo.


Alipoulizwa sasa serikali itajadiliana na nani wakati mmiliki wa Dowans hajajulikana, Dk. Rashid alisema, "Hayo si yangu. Ni mambo ya wanasiasa. Sisi tumetoa ushauri kwa serikali kwamba tunataka mashine za kuzalisha umeme…"

Alipoulizwa kwa nini TANESCO isishauri serikali kutaifisha mitambo ya Dowans, kwa hoja kwamba kampuni hiyo ilitapeli serikali kwa kurithi mkataba wa Richmond kienyeji alisema, "Hilo siwezi kulizungumzia."

Waziri Ngeleja hakupatikana kujibu swali kwa nini TANESCO inataka serikali kufanya mazungumzo na Dowans badala ya kuingia katika mchakato wa zabuni.
 
DR. Rashid akisema nilisha offer kujiuzulu rais akakataa watu watasemaje?


The buck stops at Kikwete's desk, not Dr. Rashid's.
__________________

Kiranga: hapo awali alikuwa anatikisa tu kiberiti -- kuangalia uswahiba wake na JK umekaa vipi. akagundua umekaa barabara -- hivyo akapata kaujeuri ka-kuwatukana Watanzania na kutoa vitisho kwamba mkikataa mitumba hii ya Dowans mtalala giza.... Huyu mtu anaweza hata kufanya hujuma kwa kuagiza kukatwa kwa umeme kutimiza lengo lake.

Hujuma ndiyo zake -- alihusika kashfa la kuanguka kwa benki ya kwanza ya kigeni nchini -- Meridien Biao mapema 1994 -- kuchapisha noti mbovu za 1,000/- mwaka 1998 na hilo la rada.

Kuhusu Meridien Biao -- mchakato wake wa kuirithisha benki hiyo kwa Stanbic mwishoni mwa 1994 ulifanyika wakati JK akiwa Waziri wa Fedha na inasemekana uliendeshwa kwa kifisadi.

ZM,

Naelewa hivyo, swali langu ni kwamba, kama huyu mtu anafanya madudu, halafu anataka kujiuzulu, rais anakataa, halafu anaendelea kufanya madudu, anayechukua wajibu wa mwisho ni yeye Dr. Rashid au Kikwete?

Kikwete kashampigia Dr. Rashid kura ya confidence, kama Dr. Rashid anachemsha na Kikwete hamuwajibishi, hili ni tatizo la uongozi kwa Kikwete zaidi.
 
Naelewa hivyo, swali langu ni kwamba, kama huyu mtu anafanya madudu, halafu anataka kujiuzulu, rais anakataa, halafu anaendelea kufanya madudu, anayechukua wajibu wa mwisho ni yeye Dr. Rashid au Kikwete?

Kikwete kashampigia Dr. Rashid kura ya confidence, kama Dr. Rashid anachemsha na Kikwete hamuwajibishi, hili ni tatizo la uongozi kwa Kikwete zaidi.

__________________

Kiranga: Ni kweli -- the buck stops at JK ambaye ni dhaifu kiasi kwamba hawezi kumwondoa rashid, in fact hawezi kumwondoa kiongozi yoyote labda ma-sisimisi tu -- yaani ma-DC wanaochapa walimu viboko. Kisha kumwondoa nani tangu aingie madarakani sasa zaidi ya miaka 3? hasa katika utawala wake ambao kashfa haziishi?
Huoni kichekesho kwamba kuna mafisadi wawili waliothibitishwa na Bunge ambao hadi leo hii bado wanaongoza taasisi nyeti nchini, mojawapo ni ile ya kupambana na ufisadi?
 
Ufumbuzi wa tatizo la umeme, ni kuwekeza kwenye hydro-power (umeme utokanao na nguvu za maji) kwani tuna mito mingi.Mfano kule Makete (Iringa) kuna mito ya uhakika yaani mito ambayo haikauki mwaka mzima, ambayo inamwaga maji yake ziwa nyasa.
 
Ndio maana mnaongozwa kwa kuwa kazi yenu ni kuangalia bisibisi mkimsikiliza Nyani awaambie nini cha kufanya kwi kwi kwi!


Na hilo ndio kosa lenu, ndio maana kila siku mna saini mikataba kama ile ya Mangungo na Carl Peters..........umeme waacheeni mabibi na mabwana umeme wawe na neno la mwisho!!! SIKILIZA MCHUNGAJI KISHOKA!
 
Last edited:
Na hilo ndio kosa lenu, ndio maana kila siku mna saini mikataba kama ile ya Mangungo na Carl Peters..........umeme waacheeni mabibi na mabwana umeme wawe na neno la mwisho!!! SIKILIZA MCHUNGAJI KISHOKA!

As Nyani would say Bwahaha bwana mdogo! chezea bika na maji ya rangi rangi, siye tutakupa njozi zetu ugeuze ziwe mali kisha tupewe sifa sisi kwa kufikiria hilo jambo. Weye huwezi kufanya kitu bila ngwini kulifikiria, maana uwezo wako na upeo wako wa kufikiria ni finyu, kazi kukokotoa mahesabu yaliyoandikwa na wengine kwi kwi kwi

Ngoja uonde kujikombakomba kwa cupcake wa watu Kelly01 huku Ngosha LeanBack akikusubiri! kwi kwi kwi!
 
As Nyani would say Bwahaha bwana mdogo! chezea bika na maji ya rangi rangi, siye tutakupa njozi zetu ugeuze ziwe mali kisha tupewe sifa sisi kwa kufikiria hilo jambo. Weye huwezi kufanya kitu bila ngwini kulifikiria, maana uwezo wako na upeo wako wa kufikiria ni finyu, kazi kukokotoa mahesabu yaliyoandikwa na wengine kwi kwi kwi

Ngoja uonde kujikombakomba kwa cupcake wa watu Kelly01 huku Ngosha LeanBack akikusubiri! kwi kwi kwi!

Unajaribu kuchekesha lakini haichekeshi....toka lini ngwini akawa na idea nzuri za maana za kisayansi?? Mfano wa mangwini wanapoingilia sayansi ni pale stem cell research inapopigwa marufuku ati kwasababu Rev. Kishoka kasema ni abortion, au marufuku "abc" ati kwasababu lelelalale....waacheni wanasayansi wafanye vitu vyao, ndio maana watu wakipata upenyo wanaingizana magharibi ambako kuna lipa na taaluma zao zinaheshimiwa!

Toka lini mwenye digrii ya kuchonga vinyago akawapa amri mafundi umeme bila kusikiliza mawazo yao?? ni Tanzania peke yako....aibu na ndio maana hatuendelei!

I hate ngwiniz dizaini yako........
 
I hate ngwiniz dizaini yako........

Ungwini wangu ni upi huo unaouchukia yakhe? au bado una hasira na mimi tangu enzi za Gimme the Loot?

I am not ngwini or a scientist, just an average guy like Joe the Plumber. I think, read and reason on everything.

For your information I am one of the few people who are trying to push for Tanzania to go Solar and Wind Power and reduce dependency on Hydropower because of draught and de-forestation!

Sasa kama nyie spana boi, hamuoni kuwa Umeme wa Pangaboi na Jua unaweza kutupa alternative japo 30% kupunguza hizo Hydro au Diseli ambazo zinapuliti nchi, je mmelala usingizi wa namna gani, mtoto wa mjini kama mimi niwaze ubora wa umeme wa jua?

Hate the game bwana not a playerR ndio maana nakuambia hata Kapukeki atakukimbia kisa unakokotoa hisabati left and right kujaribu kumwambia ana sura nzuri na umbo zuri!

Ukizidiwa chukua Shairi la Shekispia umuimbie Kapukeki na si Algorithim!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom