Umeme na Nishati: Tatizo sugu Tanzania

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Jana nimejiuliza sana kwa nini Tanzania tunahangaika na ukosefu wa umeme kila mwaka na hata kuzorotesha uchumi n kukua kwa maendeleo? nikajiuliza ni mvua, mabwawa au mitambo? Nikapata tamati kuwa ni watu au kwa maneno sahihi ni Uongozi pofu na mbovu.

Leo hii nadamka asubuhi nasoma gazeti, nakutana na hii kauli ya Waziri Mkuu Pinda anayesema tukaribishe wawekezaji!

Je Tanzania si kuna IPTL, Songas, Agreko, Kiwira,Richmond, Dowans, Tanesco na Ewura na wengine wengi ukiongezea majenereta? Sasa kama tuna makampuni na taasisi zote hizi, kwa nini tuendelee kusema tunahitaji wazalishaji wapya wa umeme?

Kwani mahitaji yetu ni kiasi gani kwa mwaka? je mabwawa ya maji ya Kidatu, Handeni, Wami, Nyumba ya Mungu, Mtera, Kihansi na hata hili jipya la Ruhiji yana uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi gani?

Je gesi, mafuta, makaa ya mawe, jua na upepo zinatuzalishia megawati ngapi kila siku au kila mwaka kukidhi mahitaji ya Taifa?

Hivi kweli Tanzania tuna sera kamambe ya kujijenga katika miundombinu kama Umeme, Barabara, Maji, Simu, Bandari, Reli na mengineyo ambayo ni muhimu kwa kujenga Taifa lenye uchumi imara au kama suala la Umeme na Nishati tunakimbilia kusema "njooni wawekezaji"?


Pinda ataka wawekazajii wa umeme
Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amezita nchi wananchama wa Mamlaka za Udhibiti wa Huduma za Umeme Kusini mwa Afrika (Rera) kuvuta wawekezaji katika sekta ya umeme ili kuondoa tatizo kubwa la umeme linalozikumba nchi wanachama wa Jumuiya ya Biashara Kusini mwa Afrika (SADC).

Pinda aliishauri Rara kuweka mikakati imara
itakayozewezesha nchi wanachama kupunguza tatizo la upatikanaji wa nishati hiyo kwa sababu inawezekama juhudi na maarifa vikifanyika.

Waziri Pindi alitoa changamoto hiyo jana wakati akifungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Rare unaofanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

“Afrika ndiyo yenye kiwango kidogo cha upatikanaji wa umeme ambacho ni sawa na asilimia 25 tu, hali mbaya zaidi ni vijijini ambapo wakazi zaidi ya asilimia 75
huishi ambao hupata umeme wa asilimia mbili tu,” alisema Waziri.

Alitoa mfano wa Nchi za SADC ambazo zilipigania Uhuru wa Nchi hizo na kufanikiwa na kwamba iwapo Nchi hizo
zitaunganisha nguvu zao kwa kugawana vyanzo hivyo ni wazi watashinda.

Baadhi ya changamoto alizozitoa Waziri Mkuu katika kukabiliana na tatizo hilo ni kupanua huduma hizo kwa
kutumia nguvu za maji, makaa ya mawe, gesi asilia na mafuta.

Pia alizitaka nchi wananchama wa jumuiy hiyo kukabiliana na changamoto kadhaa kama uhaba fedha kwa ajili ya kugharamia miradi hiyo, ufundi, miundombinu na kuepukana na utegemezi zaidi katika umeme unaotokana na maji ambao sasa si wa uhakika.

Naye Waziri wa Nishati na Madini,
William Ngeleja alisema lengo kuu ni kuangalia ni jinsi ya kuunganisha nguvu katika kukabiliana na tatizo hilo.

“Ni wakati muafaka kwa nchi zetu kuhakikisha kwamba huduma
hiyo inaboreshwa na inakuwa endelevu,” alisema Ngeleja.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamla ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura), Simon Sayore alisema lengo ni kuhakikisha kuwa tatizo la uhaba wa umeme
katika nchi hizo.
Mkutano huo unawakutanisha wadau 150 wa kutoka nchi wanachana wa Rera na wasiowanachama kutoka nchi za Mozambique, Zambia, Malawi, Nigeria, Lesotho, Afrika Kusini, Namibia, USA, Norway, Madagascar, Angola, Botwsana, Uganda, Kenya and Tanzania.
 
Nyani,

Wala usione aibu, sema wazi tukusikie, "ndivyo tulivyo", wavivu w kufikiria, wavivu wa kufanya kazi, waoga wa kuingia gharama, tuliokosa ubunifu na zaidi mwamko wa uzalendo=Kutegemea misaada!
 
Fundi Mchundo, Mwalimu Kichuguu,

Hivi Tanzania inahitaji umeme kiasi gani kwa mwaka na tuna uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi gani kupitia mabwawa ya maji tuliyonayo?
 
Kwani tatizo la umeme Tanzania limetokana na nini? tumezungukwa na maziwa makubwa matatu, tuna mito bwelele, mabonde kibao n.k kwanini bado tunahangaika na nishati?
 
Nyani,

Wala usione aibu, sema wazi tukusikie, "ndivyo tulivyo", wavivu w kufikiria, wavivu wa kufanya kazi, waoga wa kuingia gharama, tuliokosa ubunifu na zaidi mwamko wa uzalendo=Kutegemea misaada!

Ushindi wa Obama si kwa watu Weusi na Waafrika tuu, bali ni kwa kila mtu ambaye siku zote amelelewa na kukuwa katika mazingira yanayomwambia kuwa yeye ni batili, nusu na hana thamani.

Furaha ya watu Weusi, mimi nikiwa mmoja wapo ni kule kuushinda Unyonge uliojengwa ndani yetu, ule wa Nyani wa Ngabu kusema ndivyo tulivyo, unyonge wa kuonekana kuwa hatuna thamani wala uwezo wowote.

Chagua upande. Simama uhesabiwe.

malc011_a.jpg


``I have more respect for a man who let's me know where he stands, even if he's wrong. Than the one who comes up like an angel and is nothing but a devil.´´
_____________
 
.....tatizo ni politiki za umeme Tanzania na Pinda naye anaongea kama mtu asiyejua kitu au ni kweli haelewi kitu ambacho ni hatari sana,na humu ndani ya JF wengi wenu ni makelele tuu na hamna idea na wala hamchukui muda kufanya research kidogo na ninakumbuka wengi humu mlikuwa staunch supporter wa wabunge waliokataa muswada mpya wa umeme halafu leo mnajiuliza kwa nini hatuna umeme? TZ kuna gas kibao ambayo ingeweza kuzalisha umeme na kubaki ziada,wananchi dont deserve this na hii ni kwa sababu moja tuu ya ukilaza na siasa chafu za watu wasiojua kitu....tatizo la kukosa umeme,migawo,rushwa na kutapeliwa kwenye sekta ya umeme ni moja tuu na mchawi ni sheria zilizopo na bila kuzibadili tusitegemee chochote,lakini at least JK alijaribu lakini wabunge kwa kutaka misifa au kutokuelewa basi wakaipiga chini bill yote,inasikitisha sana!
 
Kuna Stieglers Gorge mto Rufiji yenye uwezo wa kutoa hadi 1000 MW; kiwango hiki cha umeme kingekidhi mahitaji ya Tanzania na ziada. Nilikuwa na habari kuwa World bank walikuwa tayari kuu-fund mradi huu kwa masharti with prerequisite ya kujenga miundombinu ya kutosha kuiwezesha serikali kuuza umeme wa ziada huu nje ya nchi. Pamoja na vikwazo toka kwa wanamazingira, sijui hii plan iliishia wapi. Umeme wa maji ni rahisi kuufua, gharama yake kubwa ni kwenye ujenzi wa hizo turbines na mazagazaga yake. Afterwards n maintanance tu. Tanzania ingesahau tatizo la umeme.
 
hivi kukiwa na umeme sasa wale mafundi wa sido wa vibatari (wakina joe the plumber wa kibongo) wakale wapi? acheni nyinyi maneno yenu.........kukosekana kwa umeme ni industry flani na kupatikana kwake kunapunguza ajira!!

hizo ni two cents zangu, in a nutshell.....
 
Duuuh, yani we umeona ile quote ya Malcom pale inamfagilia ? Hebu pitia tena posti nzima.

Trust me, mwenyewe kaelewa!
 
Duuuh, yani we umeona ile quote ya Malcom pale inamfagilia ? Hebu pitia tena posti nzima ile.

Trust me, mwenyewe kaelewa!

unajisahau sana! nimeangalia post nzima na hiyo ni take yangu..upo hapo? suala si mwenyewe kuelewa, suala ni sisi adhila tunaonaje..........ukifuatilia thread za Rev. Kishoka ua zianaishia hewani, si mfuatiliaji na kwa maana hiyo ni mzushi flani tu anayependa kuja na mada mpya kila apatapo nafasi baada ya kunywa mvinyo wa dezo wa kanisa.

maneno mingi tu...
 
hivi kukiwa na umeme sasa wale mafundi wa sido wa vibatari (wakina joe the plumber wa kibongo) wakale wapi? acheni nyinyi maneno yenu.........kukosekana kwa umeme ni industry flani na kupatikana kwake kunapunguza ajira!!

hizo ni two cents zangu, in a nutshell.....

wale mafundi vibatari wataupgrade na kuuza zaidi. Wataanza kutengeneza majeri ken ya kumwagilia badala ya kutengeneza vibatari; hii itawaongezea kipato kwani jeri keni moja bei yake ni juu kuliko ya kibatari. Kumbuka unaweza kukaa na kibatari miaka mitano bila kununua kingine (kinawekwa pale kumulika tu-hakipati mikiki). Hata hivyo umeme utawasaidia kufanya kazi kwa urahisi na kutoa products zenye ubora utakaokidhi masoko nje ya nchi.
 
unajisahau sana! nimeangalia post nzima na hiyo ni take yangu..upo hapo? suala si mwenyewe kuelewa, suala ni sisi adhila tunaonaje..........ukifuatilia thread za Rev. Kishoka ua zianaishia hewani, si mfuatiliaji na kwa maana hiyo ni mzushi flani tu anayependa kuja na mada mpya kila apatapo nafasi baada ya kunywa mvinyo wa dezo wa kanisa.

maneno mingi tu...

Tatizo lenu ni kuogopa kufikiria na kushupalia udaku usio na nguvu! Mtu kutoa maoni yake kwa upeo wake wa kufikiria na kupima mambo mnaona mzushi!

Lakini mkiambiwa Manji ana kaswende, hamchelewi kujaza kurasa mia kuuliza alipataje kaswende, mara ana wanawake 10, mara laana ya kutumia Quran kwenye tiketi za Yanga, sijui kaiba EPA, mdogo wake ni mchumba wa Ridhiwani, ananyumba Makambako jirani na Sumaye na utitiri mwingi.

Vitu relevant ambavyo ndivyo mnapaswa kuvipima na kuvipigia kelele si kukosoa tuu hata kutoa tathmini au alternative hamna.

Yes Mchungaji ni Mzushi, huanzisha mada mpya ambazo hazina muelekeo lakini kama kawaida yenu mtarudi kuzikumbuka miaka ya baadaye.

Umesahau aliyeanzisha Kagoda, Meremeta, Richmond na nyinginewe ambazo mlizipuuzia unyasi ulipotikisika mkazubaa mpaka mkang'atwa ndipo mkaamka kwa ghadhabu?

Mimi si Malaika kama Kuhani anavyonipiga dongo, kuna tunayokubaliana na tusiyokubaliana. Kuhani kaona kauli zangu zina utata si mara ya kwanza, yeye ni mtaalamu, mkutubi wa kukumbusha kauli zilizotoka awali.

Weye shangilia ushindi wa Obama na naomba nisaidie kumwambia Nyani Ngabu anitumie Kavwasiye yangu, siku ya kuingia utumwani na kuuza uhuru (Thanksgiving) inakuja, baada ya shibe shurti uteremshie na maji yaliyochachuka!
 
wale mafundi vibatari wataupgrade na kuuza zaidi. Wataanza kutengeneza majeri ken ya kumwagilia badala ya kutengeneza vibatari; hii itawaongezea kipato kwani jeri keni moja bai yake ni juu kuliko kibatari. Kumbuka unaweza kukaa na kibatari miaka mitano bila kununua kingine (kinawekwa pale kumulika tu-hakipati mikiki). Hata hivyo umeme utawasaidia kufanya kazi kwa urahisi na kutoa products zenye ubora utakaokidhi masoko nje ya nchi.

Mama,

You are talking the right talk, progressive thinking and not a defeated and cowardly soul.
 
unajisahau sana! nimeangalia post nzima na hiyo ni take yangu..upo hapo? suala si mwenyewe kuelewa, suala ni sisi hadhila tunaonaje..........

Nimejisahau vipi sasa?

Kishoka hana spine ya kuchukua msimamo katika kutukana watu weusi. Siku ya ushindi wa Obama alipiga tarumbeta la hadhi ya watu weusi. Akakandya misemo ya ndivyo walivyo. Lakini akikaa kidogo ana flip, anaanza kukejeli race nyeusi kama walivyofanya ma "devil" wa miaka ya Civil Rights era. Ndio Malcom anasema ni bora Ku Klux Klan maana msimamo wao unajulikana, kuliko hawa wanaokuja kama Malaika.

Na kilicho repugnant zaidi ni kwamba, sio tu hawezi kuchukua msimamo, ila pia akianza kutukana watu weusi huwa hawezi kuongea mwenyewe mpaka atumie mgongo wa mtu mwingine. Hana backbone yake mwenyewe, ama balls, ama vyote. Ooooh fulani anasema ndivyo tulivyo, ooooh anavyosema inawezekana ni kweli. Siku nyingine anaiweka kama ni swali hivi, "je ni kweli," lakini wakati mwingine akipandwa na mukari wa ajabu anatukana bila simile za "inawezekana ni kweli."

Ndio maana ni bora yule anaekwambia yuko upande gani, hata kama yuko wrong.
 
ubovu wenyewe hujui Rev. Kishoka anasimamia nini!! ungekuwa unajua, usinge thubutu kumfagilia kwa kuweka hiyo quotation ya Malcom X wa Dudley.......

YNIM,

Do not mess with Zohan my friend! nenda katengeneze vibatari kwa Mjomba bichwa kubwa, is he still kicking?:p
 
Nimejisahau vipi sasa?

Jamaa hana spine ya kuchukua msimamo katika kutukana watu weusi. Siku ya ushindi wa Obama alipiga tarumbeta la hadhi ya watu weusi. Akakandya misemo ya ndivyo walivyo. Lakini akikaa kidogo ana flip, anaanza kutukana tena race nyeusi kama walivyofanya ma "devil" wa miaka ya Civil Rights era. Ndio Malcom anasema ni bora hata Ku Klux Klan maana msimamo wao unajulikana, kuliko hawa wanaokuja kama Malaika.

Na kilicho repugnant zaidi ni kwamba, sio tu hawezi kuchukua msimamo, ila pia akianza kutukana watu weusi huwa hawezi kuongea mwenyewe mpaka atumie mgongo wa mtu mwingine. Hana backbone yake mwenyewe, ama balls, ama vyote. Ooooh fulani anasema ndivyo tulivyo, ooooh anavyosema inawezekana ni kweli. Siku nyingine anaiweka kama ni swali hivi, "je ni kweli," lakini wakati mwingine akipandwa na mukari wa ajabu ajabu anatukana bila simile za "inawezekana ni kweli."

Ndio maana ni bora yule anaekwambia yuko upande gani, hata kama yuko wrong.

Amini uaminilo Kaka, kama sina uti wa mgongo, basi nateleza kama nyoka, mithili ya Kuhani alivyo! Chukua kioo ujiangalie! kwi kwi kwi!
 
Kuhani,

On a serious note though, hivi umeona kuwa natumia mgongo wa Nyani kutukana Watanzania na kuona sina kende kutukana kwa mdomo wangu mwenyewe?

Si wewe uliyeshangilia nilipomsiliba FMES kwenye hoja moja mpaka ukatoa tuzo ya Mtu mwenye Makende ya Chuma?

Umepitia Screw Muungwana? Je CCM adui wa Maendeleo nako huko nimekosa mfupa?

Sasa kwenye hili la Nishati na kutumia maneno ya Nyani "Ndivyo Tulivyo" nimekosea nini kueleza ukweli kuwa Serikali yetu na watendaji wake ni wavivu wa kufikiri, kupanga mambo na kuingia gharama?

Wewe ni mchumi, tupe basi zako nasaha kuwa tufanyeje zaidi ya kupembua utata wa tungo zangu au wasifu wangu.
 
Back
Top Bottom