Umeme kwangu haujakatika wiki nzima!!!

Pole sasa kaka, hamia mitaa ya kwetu umeme wa kumwaga tangu jumatatu. We njoo ujitambulishe kwa mwenyekiti wa mtaa halafu uliza wapi kwa mwana JF, utaletwa nami nitakuelekeza kuliko na nafasi (nyumba nzima, chumba/vyumba au banda la uani) kwa kadri ya mfuko wako.
Hi
Niliku-miss.It is sad kwamba kwa ID hii hutowa nitambua, labda kwa ile ya zamani...teh..teh

nadhani unakaa maeneo ya savei huko haukatiki kwani ni laini moja na ile ya mlimani UDSM. kweli hata mm sijui kama kuna mgao hapa bongo labda kuna kigogo anaishi eneo langu sijamtambua bado.

Kwetu ulikuwa unakatika kila siku wakati eneo jirani na sisi walikuwa hawakatiwi. Ilibidi tupige simu Tanesco, siku ya kwanza wakasema kuna hitilafu kwetu. Tukapiga tena, tukasema hitilafu gani hiyo isiyorekebika? Tukauliza mbona eneo jirani wao wanapata mfululizo. Basi kesho yake tulianza kupata na haukatiki ovyo sasa imefululiza mpaka nimekuwa na wasiwasi kama Mama Mdogo kwamba huenda tutaingia zamu ya kukatiwa mfululizo. Bora kukatiwa kwa ratiba inayoeleweka kuliko kwa isiyoeleweka.

Kuna unafuu kidogo,kwetu ulirudi J4 saa 2 usiku umekatika leo saa nane mchana. Sijui nitauona lini tena maana Tanesco hawatabiriki.

Jamani hata mimi kidogo niulizie swala hili. Kwani ghafla generator yetu imezimaaaaaaa toka jana hadi sasa tunakula Tane. Ninashangaa mno kwani baada ya kuogelea gizani for 32 hrs na kuiangalia taarifa ya habari kuhusu uzalishaji wa Songa Ges, basi matumaini ya kuuona umeme wa Tane. yalikufaaaa. Lakini ghafla na la ajabu kwangu sasa nina Masaa 32 tena bila umeme kukatika. SWALI JE, HII SI MBINU YA KUIPITISHA BAJETI YA NGEREJA? Kama sivyo, je, wapo wanaokontroo umeme wetu ili waweke mitambo yao? Au?

Au imejulikana kuwa Jairo alitufanyia yale ambayo mwenzake wa siku nyingi zilizopita nilisikia aliwahi kuyafanya kwa kupokea mshiko toka kwa wauza mafuta na majenereta ili Tane isitoe umeme bali wao wapate biashara?

NDO UNAWAFIDIA KINA MA MDOGO! KM VILE DUNIA INAVYOZUNGUKA KWENYE MUHUMILI WAKE NUSU KUNAKUWA GIZA NUSU MWANGA!!! SUBIRIA NEXT WEEK UMEME WIKI NZIMA HAHAHAAAA

tanesco sio wa kuwaamini msishangae wiki ijayo wakiwakatia wiki nzima!

Kwa mkoa wa dar es salaam ambapo 60% ya mapato ya shirika yanatokea hapo, mgao umelegezwa...bwana awe nanyi...hata hivyo mafuta ya IPTL yakiisha! ! !

Njia kuu za kusafirisha umeme pia hazitokitoki mzigo si mkubwa...losses zimepungua!

Nsia usiku mwema....najiinjoiya tu umeme hapa lol....

Au imejulikana kuwa Jairo alitufanyia yale ambayo mwenzake wa siku nyingi zilizopita nilisikia aliwahi kuyafanya kwa kupokea mshiko toka kwa wauza mafuta na majenereta ili Tane isitoe umeme bali wao wapate biashara?

Naona Tanesco wameitikia wito waWaziri Mkuu aliyejiuzuru, wamechukua maamuzi magumu ya kukamua maji yote kwenye mabwawa ya Mtera, Nyumba ya Mungu, Pangani na Kidatu ili liwalo na liwe wananchi wapate umeme, maana ni bora lawama kuliko fedheha. Hadi muda huu niko na enjoy umeme hadi muda huu kwa raha zangu, siamini. Natamani jumapili niombe misa ya shukrani kwa controler wa Tanesco kusahaulishwa kuvuta switch, lakini nachelea maana hawa jamaa wa tanesco siwaamini kabisa, hawatabiriki!!!!

Ni kwasababu kile kifaa cha kukatia umeme kimeharibika vibaya baada ya kufanya kazi kubwa sana mwaka huu kuliko miaka mingine tangu kilipowekwa wakati wa mkoloni...kinatengenezwa, subiri kikirudi na nguvu zaidi, kasi zaidi na ari zaidi..

Mi niliambiwa kuna kigogo mmoja amehamia nyumba ndogo mitaa ya kwetu ndo maana haukatiki,kumbe sehemu zote upo.kuna ki2 sio bure!

Inchi za watu umeme haukatiki mwaka mzima,weye wiki moja tu ishakua tabu hadi kutangaza ndani ya forum.

Back
Top Bottom