Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,319
- 33,125
Inaelezwa kuwa gharama za kulipia umeme zitakwea hewani kwa asilimia tatu zaidi kuanzia Septemba mosi, mwaka huu, ili kulipia Mfuko wa Umeme Vijijini (REA), imefahamika.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana na Ofisi ya Mawasiliano ya Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), wateja wote wanaotumia umeme na wananchi wote kwa ujumla, watatakiwa kulipa ushuru wa asilimia tatu kwa ajili ya mfuko huo.
Tangazo hilo lililosambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari jana, lilisema kuwa ushuru huo unatozwa kwa kuzingatia Tangazo la Serikali (GN) la Agosti Mosi, 2009 na ainisho la sheria ya Bunge kuhusu Wakala wa Umeme Vijijini (Rural Energy Act of 2005), kifungu namba 19 (3) ( c ) na (d).
Ushuru huu ni kwa ajili ya Mfuko wa Umeme Vijijini ambao matumizi yake ni pamoja na kuongeza kasi ya usambazaji umeme vijijini na mafunzo kwa wajasiriamali ili kuboresha maendeleo ya jamii kwa kutumia nishati bora vijijini.
Ushuru huu utakuwa ni asilimia tatu (3%) ya thamani ya umeme uliotumiwa katika mwezi husika, yaani juu ya gharama ya matumizi ya umeme, ilisema sehemu ya tangazo hilo.
TANESCO kupitia tangazo lake hilo, imeeleza kuwa yenyewe itakuwa ni mkusanyaji tu wa ushuru huo, ambapo makusanyo yote yatakabidhiwa REA.
Kutokana na tangazo hilo, sasa katika ankara ya umeme mteja atapaswa kulipia asilimia 18 kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), malipo kwa EWURA asilimia 1 na Mfuko wa Umeme Vijijini (REA), asilimia 3.
Hii inatokana na upungufu wa nafasi katika fomu ya Ankara. Hata hivyo, kwa sasa tunatengeneza fomu mpya ambayo itaonyesha kila gharama peke yake. Tunategemea fomu hii itakuwa tayari kabla ya mwisho wa mwaka 2009, ilisema sehemu ya tangazo hilo.
Source: DarHotWire.com