Umeme: January awa Bubu.

AK-47

JF-Expert Member
Nov 12, 2009
1,373
199
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini January Makamba leo ameshindwa kutoa mapendekezo ya kamati yake kuhusu ufumbuzi wa mgao wa umeme nchini, kama alivyoshindwa rais JK katika hotuba yake kwa taifa hapo jana.

Kamati hiyo iliyokaa siku nane mfululizo kutafuta tiba ya tatizo la umeme na ufumbuzi wa sakata la Dowans leo imeufyata mkia na cha ajabu imeamua kumtumia mkuu wa ulinzi wa ofisi za bunge DSM kuwa msemaji wake kwa waandishi waliokua na kiu ya kuyapata mapendekezo hayo.

Mlinzi huyo aliyekuwa amekariri vyema maagizo ya January alikuwa akiwaambia waandishi samahani M/Kiti wa kamati amesema hataongea lolote na waandishi wa habari na mapendekezo ya kamati yake sasa atayapeleka kwa Katibu wa Bunge na si kwa vyombo vya habari.
 
January Makamba ambaye pia ni msemaji(asiye rasmi) wa Dowans atasema nini?
Inabidi jamaa wakubali kuwa Dili la Dowans lishakuwa nyoka watafute mwanya mwingine tuu.
 
Back
Top Bottom