Umekutana na hili?

NATA

JF-Expert Member
May 10, 2007
4,492
1,311
Jamani hii biashara ya mikokoteni barabarani inakera sana

Kunasiku nilikwanguliwa gari yangu mpya na mkokoteni, na ilikuwa kwa makusudi mazima. huyo mwenye mkokoteni hata kukulipa hawezi. nikaishia kuingia mfukoni kwangu

Jana mkokoteni umesababisha foleni ndefu bila mpango umebeba mambao kibao ambayo ni hatari kwa usalama

Hivi serikali haina mpango wowote wa kuhakikisha inatenga njia kwa ajili ya hii mikokoteni?

Vinginevyo ni kero sana.
Hao nao wanalipa road licence na insurance cover?
 
Hawalipii kodi hao, ni kero sana barabarani.
 
Hili ni tatizo lakini haitoshi kulijadili bila kutafuta ufumbuzi. Kina nani wanawapa kazi zile? Je, tukiwaondoa kwenye kazi zile watapata wapi ajira? Au wafundishwe matumizi ya barabara kwa kuwajali watumiaji wengine? Hawa jamaa wanaumuhim kwa Watanzania wengi maana kusafirisha bidhaa kwa gari kutaongeza bei ya bidhaa kwa final consumer. Lakini maisha yao na mali za watumiajia barabara ni vyema kuzingatiwa.
 
Masikini akipata bwana, ****** hulia mbwata! Leo hii msukuma mkokoteni ameshakuwa kero wakati anatoa msaada mkubwa sana kwa wanyonge wenzake!
 
Hii mikokoteni inaoperate sana maeneo ya Ilala Sokoni na Buguruni kwa kweli ni kero kubwa, tatizo unaweza kuta sheria iko silence kuhusu hawa watu ndio maana traffic wanawachekea tu.
 
Masikini akipata bwana, ****** hulia mbwata! Leo hii msukuma mkokoteni ameshakuwa kero wakati anatoa msaada mkubwa sana kwa wanyonge wenzake!

Sidhani kama ni kuwakashfu bali ni kero kubwa wanapaswa kuwepo kwa maisha yao na ajira zao lakini serikali iliangalie hili kwa kifupi wanakera kwani wanmakusudi sana
 
Wawe na Utaratibu na sio kuendesha mikokoteni yao katikati ya barara
 
Masikini akipata bwana, ****** hulia mbwata! Leo hii msukuma mkokoteni ameshakuwa kero wakati anatoa msaada mkubwa sana kwa wanyonge wenzake!
Li jadili kiupeo kidogo mkuu!
 
Wanapaswa wawe wanapitia service roads pamoja na wapanda baiskeli, leo nimepita kilwa rd na ina service rd...chakushangaza mwenye baiskeli anabanana na magari barabarani mpk nikamsogezea ili aingie service rd aendeshe kwa uhuru & usalama. Hatimae alihamia service rd, ni elimu pia ya barabarani hawana hao. But our gov't could have well planned these roads to enable hao wasukuma mikokoteni + cyclists.
 
aisee wale jamaa ni wabishi na ubishi wao wa kijinga sana.. mi washantia hasara mara mbili

sijui tuwafanyaje hawa watu
 
Nafikiri alichokisema mpevu Elimu ni muhimu sana ili kujua mipaka yao na kuwa na heshma kidogo kwa watu wengine maana yake si kwa wenye magari tu nenda kariakoo sokoni mkokoteni utakupitia jiranai ili tu ukuguse hata kama umebeba uchafu
 
Hawa jamaa waliruhusiwa na Aliyekuwa rais wa awamu ya kwanza kipindi kile cha mafuta ya mgao! Ila wote tuwe na heshima barabarani ajali tutazisikia. Ila kama uko na haraka zako, kila siku utawakwangua.
 
Na wao watakukwangua hata kama huna haraka!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom