Umeitwa kwenye hii kesi,ungesuluhisha au kushauri vipi?

Hapo ndio ametupa kigugumizi,kwa kweli nimeshindwa kusema lolote maana nimemuuliza huyu ndugu yangu anajua madhara ya kutembea na mtu anaekaa nyumba moja na mkewe?
Kama alimpenda huyu housegirl bora angemuhamisha hapo nyumbani wafanyie mbali,
Ni kweli wifi yangu amekosea lakini kweli alistahili hili??
Anataka kuondoka kabisa,analia muda wote,mimewe hata haombi msamaha ananikera sana,nadhani mapenzi hayapo tena lakini wakiachana wale watoto ni wadogo na kazi za wazazi wao watakua na mazingir magumu kukaa kwa mzazi yeyote maana wanahitaji msaidizi,huyu ndugu yangu najua hataweza kabisa kulea hawa watoto,sio kipato,ila ni jinsi anavyoendesha maisha yake,
Huyu mke tunaona kabisa bado anampenda mumewe ila mume kajitia kiburi

Unajuwa dadaangu hakuna kitu kibaya kama kudharauliwa na wifi yako alifanya hayo kwa mumewe. Dharau hasa ikitoka kwa mwanamke ina sumu kubwa kwa ndowa na huyo mdogo wako aliila hiyo sumu muda mrefu kiasi cha kuuwa kabisa penzi lake. Kifacho kinatabu kuja juu.

Iwapo mambo yaliyomfanya aowe hakuyapata kwa wifi yako na badala yake anayapata pengine, shida ya nini? Huyo wifi yako akashughulikie alichokithamini na akiondoka basi ndugu yako atahalalisha yule anaemjali.
 
Mwali,sio kama waliwahi kutishiana,ila kaka anasema mara nyingi amewahi kumsema mkewe kuhusu kutowajibika kama mke,
Lakini kiukweli yule mke pia ana mchango mkubwa kwa familia yake kupitia hiyo biashara maana huyu ndugu yangu biashara yake ni ya kusafiri hivyo muda mwingi anapokua Dar anakua nyumbani zaidi.

Loose ends hapo ni kwamba huyo jamaa anajificha kwa alibi kwamba isingekuwa mke kuwa busy hivyo asingeenda kwa h/girl..
 
Pamoja na kuwa wote wanamakosa Lakini Pia Hakuna mapenzi ya Kweli kati yao

Ushauri; Wote watubu Kwa Mungu wao kwa makosa yao na Kisha wao wasameheane na Kuanza Upya

Wakirekebisha kila walipo kosea

Bila Mungu Hawataweza, Ni Lazima kuombe Neema ya Mungu
 
Pamoja na kuwa wote wana makosa lakini haimpi haki mwanaume kutembea na housegirl....... Yaani wanawake wote mpaka atembee na hg? Na mnapoambiwa ndoa inahitaji uvumilivu na ukomavu ndio hapo sasa........ Kama mwanaume angetafuta njia mbadala ya kumaliza tatizo na mkewe....... Si ndo maana mnajiita nyie ni kichwa cha familia? Kichwa kikiamua maamuzi 'utumbo' itakuwaje?


Kitendo cha mke kurudi saa sita usiku tu inaonyesha kuwa ndoa yao ina walakini,

keti nao wakueleze vizuri kuna kitu ambacho hakipo wazi hapo....na hakuna wateja wa saa sita usiku............

Nimachokiona ni kama wanakomoana, ndoa haina kukomoana, ndoa haina mbabe, ndoa inabebwa na kusikilizana, kujitoa, na KUVUMILIANA.......

Hawana watoto hao wana ndoa? Na kipindi mke kajifungua huyo mwanaume alikuwa anatembea na nani? Maana kipindi kile ni cha kusubiri kati ya wiki 2-siku40 au zaidi kutegemea na mwanamke na mwanamke......je huyo mwanaume alimaliza vipo mihemko yake?


Kuna tatizo kwenye hiyo ndoa, na tatizo si la mke kuchelewa kurudi wa lamume kutembea na hg, nahisi kuna kitu hawajakisema....


Ebu angalia Mwanaume anavyosema

1. Anasema
ameshachoka na mambo ya mkewe ameshamkanya sana
hasikii vilevile hata
unyumba hataki kunipa
nina mwezi sasa

2.nikimwambia anasema
anaumwa

3.kwahiyo nimeamua kuwa na huyu
msichana siwezi kupata
shida wakati kuna mtu
ndani anaweza kunipa
ninachotaka

Hebu angalia Mwanamke na Yeye

1.Yeye ana salon yake

2.huwa siku zote anarudi saa
5 hadi 6 usiku

3.hana hata
siku ambayo anakaa
nyumbani kuangalia watoto
au kumpikia mume wake kila kitu anafanya h.girl.

Ebu Angalia Nani ameacha Majukumu yake Hapo?

Wanawake nawasihi huku Moyo wangu unauma TIMIZENI WAJIBU WENU KWANZA.

hakuna Raha kama kuhudumiwa na Mke wako,
Ndo maana Tunawaoa na Kuwatolea Mahali maana Tunataka Mtuhudumie sisi na Familia Tutakayoanza
 
matatizo mengine wanawake tunachangia sisi wenyewe, hasa kuwepo kwa nyumba ndogo. wewe una mume, huna haya mtoto wa kike J3 mpaka j2 kwako unarudi 5 au 6 usiku. hujui watoto wameshindaje, wanaumwa, wamekwenda shule, wana homework. wewe ni pesa, pesa na wewe. hujui mume kala nini, kapenda chakula, basi umeshindwa vyote, na kitu tamu ambayo ni haki yake huwezi kumpa! salon gani hiyo ya kurudi ma-usiku kila siku, huyo atakua ana ki serengeti somewhere kinamkuna, ndio maana haraka haraka kakimbilia anataka kuachika, maana alikua anaisubiri hiyo siku kwa hamu. wifi yako hajatulia. shindwa vyote kwa mumeo, lakini unyumba MUST, anataka aende wapi? sasa kamkomoa, kachukua hsegal, ya nini aende mbali na anayemhudumia yeye na watoto wake yuko humo humo ndani. aache kulalama na kusema eti yuko kwenye siku zake, huo ni uzushi. kuna njia kibao za kumridhisha mwenzio hata kama uko kwenye siku. kanogewa kwa kiserengeti chake aache kutunga hadithi za vitabu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom