Umeishi Kijijini? ...Mimi Nimeishi

Teh teh mama na mwana jamani mnakumbuka hata huko hadithi ya Adili na Nduguze mwaikumbuka nilikuwa siikosi na yule bibi mwenye sauti ya kutisha.

Mwakumbuka Mikingamooo??
Na mikingamo ndicho kipindi kilichokuwa chawaacha hoi wazeee wetu ile usiku shutuma wazi wazi, wazee wetu walikuwa na hali jojo.

Kipindi hicho (MIKINGAMO)kilikuwa hatari sana KWA mafisadi wa enzi hizo, in the name of "WAHUJUMU UCHUMI NA WALANGUZI" kam JF ilivyo kwasasa, au kama MWANAHALISI inavyowaumbua wala nchi!...

Utasikia "Mkuu ambaye jina lake linaanzia na "K", amehujumu mali ya kampuni.
tHANX ALOT MAN FOR this!
 
Umeishi kijijini, na una kisa chochote? tupe basi!

Teh teh enzi izo baada ya likizo narudi kijijni ukerewe kwa mama mkubwa to kea mwanza mjini tulikuwa twa panda Meli inaitwa Cralias au MV Butiama mpaka leo zipo,
Nilipokuwa pale skul nilikuwa navaa viatu kwa zile mara za kwanza si unajua ulienda mji kwa mama aka kununulia ukirudi lazima mtambishiane na wale watoto wa wakurugenzi wa majineri na wa wakuu wa chuo cha ualimu teh teh, ila at the end mkienda skul 99% wako mikuuu peku nasi ikatubidi tuwaige wanavyo kuja wenzetu miguu peku.

wakati wa kwenda kusenya(Kuokota) kunai huko mwa wakuta kaka zetu na videmu vyao mapolini wana do smthing teh teh, utaona baiskeli imepakiwa vichakani huko jamaani.

Kubwa zaidi enzi za harusi kulikuwa na ngoma ina itwa Kadogori a.k.a Ngoma tatu na mtaaalamu wa huo mchezo alikuwa anatokea huko mwibhara Mara Musoma anaitwa Joy wa matindo alikuwa anakatika kadogori huyo usipaime!!! Nilicho taka kusema kuhusu arusi za enzi izo ni kaka anapo mwoa dada ni shari kutaka kujua kama dada ni bikra ni lazima kaka na dada waende chumbani kitanda kimetandikwa shuka nyeuupe na shangazi wa kaka lazima awepo wakati wa tukio nalilikuwa likifanyiak mkiwa naked full full na mki do na dada ukamtoa bikra na damu ikaonekana Shangazi anapiga vigeregere na huku nje watu wanaitikia kumbuka hiyo ni mchana wa jua likiwaka na kadogori inapigwa mbaya sasa na watu wansherekea obhwenga(Harusi)

Je huko kijijini kwenu Je ilikuwaje???

Najua nduguzangu wasukuma mtaniambia mambo ya Chagulaga
 
....... in the name of "WAHUJUMU UCHUMI NA WALANGUZI" kam JF ilivyo kwasasa, au kama MWANAHALISI inavyowaumbua wala nchi!...

Teh teh mpwa umenichekesha sana nilikuwa nimepitiwa kidogo na hilo neno zima duuuuuh nawe umo kweli kweli,

Nakumbuka hupo Shinyanga kulikuwa na matajiri wa mafuta ya pamba Paul Ng'wani walitupa madebe na kumwagia Iodine weeeeee acheni bwana, wakina Mwankamba

Huyu Paul Ng'hwani na ndugu yake Edward Ng'hwani walikuwa na hela sana..Walikomba hela nyingi sana za SHIRECU hawa
 
Huyu Paul Ng'hwani na ndugu yake Edward Ng'hwani walikuwa na hela sana..Walikomba hela nyingi sana za SHIRECU hawa

Teh teh!!!! mpwa nilikuwepo Shy in 1999 nili pita pale kwao ukivuka kadara ka buluba secondary mbele kidogo karibu na kanisa kwa kweli ni wamefulia na kama wanazo basi ni kidogo sn, kwani SHIRECU kwisha habari yake tena na hata yale magodauni yamebakia vyuma chakavu jamani. wamebakia wakina salim amri ndio matajiri na viwanda vya mafuta ukivuka daraja jipya karibia na Halimashauri ofice kuelekea maganzo.

PJ.....pamoja na yote uliyosema hunifikii mimi. Nimezaliwa kijijini, nimekulia huko, nimesoma huko primary, kuchunga mbuzi, kuchnja kuni, yote hayo ni ya kawaida.....sasa kubwa ambalo wewe hukufanya na nahisi hutafanya maishani kwako ni nilikuwa natengeneza na kuuza gongo ili ninunue suruali, viatu na kunywa pia.
 
Mwana jamvi,

Wewe binafsi umeshawahi kuishi kijijini?

Ninaposema kuishi kijijini ninamaanisha kuwepo huko, kushiriki majumuiko mbalimbali, sherehe na kazi zote za uzalishaji za huko.

Nia ya swali langu ni kujaribu kujua hasa wakati tunapojadili masuala kama ya kumkomboa mkulima(peasant), au asilimia 80 ya watanzania kuishi vijijini, tunaongea kwa uchungu na kujua kiukweli maisha ya vijijini yalivyo?

Pia tunaongelea KILIMO KWANZA,ambapo kwa kiasi kikubwa kinatekelezwa vijijini.

Usikute watu wanajiita Mzee Mwanakijiji, Ng`wana Madaso, au Balantanda, kumbe wamezaliwa, kukulia, na kusomea mijini, na hawajaonja pepo ya kijiji!. Nina shaka na watu kama Bluray, Firstlady, Kigogo,bht na wengine, kama wanajua jembe, kama si kuliona kwenye nembo ya sisiemu!

Mimi binafsi nimezaliwa, kukulia, na kusomea kijijini.
Nimechunga mbuzi na kondoo, nikaokota kuni msituni ,na kucheza dimbadimba! Nimetembea pekupeku kwa kadiri ya muongo mmoja, thats me!

Umeishi kijijini, na una kisa chochote? tupe basi!

....PJ.....mbona wewe cha mtoto!!!!........je gongo ulipika, ukauza ili upate hela? na je ulikunywa hilo gongo???
 
Usikute watu wanajiita Mzee Mwanakijiji, Ng`wana Madaso, au Balantanda, kumbe wamezaliwa, kukulia, na kusomea mijini, na hawajaonja pepo ya kijiji!. Nina shaka na watu kama Bluray, Firstlady, Kigogo,bht na wengine, kama wanajua jembe, kama si kuliona kwenye nembo ya sisiemu!

Big up PJ wasiwasi wangu ni kwamba pamoja na reality ulizokuja nazo umekuja kichokozi zaidi. Siongezi neno ntakuwa mwongo!
 
Maskini hawezi msaidia maskini mwenzake
Mkulima hawezi msaidie mkulima mwenzake
Mfanyakazi hawezi msaidia mfanyakazi mwenzake

kuna haja ya kubadilisha kwa makusudi kabisa na kutengeneza mchanganyiko wa kijamii ile watu wa vijiji watambue umuhimu wa "ubora wa Maisha"

Kijijini kwetu hakuna tatizo la umaskini ila kuna tatizo la watu kutojua umuhimu na ubora wa maisha..sioni mantiki ya mwanakijiji mwenye ekari kumi na ng'ombe hamsini kuishi maisha duni (shelter sehemu anayolala, chakula anachokula, usafiri anaotumia, usafi wake wa mwili e.g. kuoga, kufua nguo etc) kupita muuza magazeti Dar anayeisha chumba kimoja tandika nafikir urban poverty is too critical than rural poverty

isipokuwa watu wa mjini wanafahamu umuhimu wa ubora wa maisha kama vile kuoga, kuvaa nguo safi, kulala eneo na sehemu nzuri (kitanda na godoro) vijijini mtu analala ovyo ovyo..japo ana ng'ombe..

Nimeishi kijijini siwezi kuishi kama nilivyoishi zamani lazima nipa-improve sana.
 
Nimeishi vijiji vingi sana Tanzania katika kazi zangu... vijiji vya wafugaji huko usitegemee maji ya bomba, maji ni ya malambo ambapo hutumika kwa binadamu na wanyama.Vijiji vya wakulima navyo vinatofautiana.Kijiji cha Kilimanjaro, siyo sawa na kile cha Nkasi Sumbawanga, wala cha huko Shinyanga Kolandoto au Meatu.
Usilinganishe kijiji cha Bagamoyo na kile cha Upareni au Tabora.
Kitu kimoja nilichojifunza ni kuwa kijijini siyo maisha laini wala hayana unafuu kama tunavyosikia kwenye nyimbo za wanamuziki wa bendi za Tanzania.Remmy aliwahi kuimba narudi kijijini kula kanyungu! Wengine wameimba kama maisha yamekushinda mjini rudi kijijini. Binafsi naweza kusema kuwa usithubutu kurudi kijiji kwa vile maisha yamekushinda mjini maana kule ni zaidi ya JKT!
 
uzuri wa kijijini mamisosi unlimited halafu natural.. ukisikia tu njaa unajisevia chochote tena cio kutoka kwenye frij toka mtini original/shambani
 
uzuri wa kijijini mamisosi unlimited halafu natural.. ukisikia tu njaa unajisevia chochote tena cio kutoka kwenye frij toka mtini original/shambani

Ishuguy,Kwa Mtazamao wa chakula, hakika kwa wale wazee wa vijijini wanaojishughulisha hawana tatizo.Unakwea mtini na kujisevia mapeasi ya kushiba, na huulizwi na mtu!Nakumbuka Baba yangu mimi alikuwa mlimaji mzuri sana, na mara nyingi watu werngi walitegemea chakula toka kwake.Pamoja na aina ya maisha ya shida za kawaida, (kama aliyoyaongelea Tumaini hapa juu), kwakweli njaa haikutupiga hata siku moja.Tatizo linakuja kwenye kutoa vipaumbele(nguo? viatu?chakula bora? etc)
 
....PJ.....mbona wewe cha mtoto!!!!........je gongo ulipika, ukauza ili upate hela? na je ulikunywa hilo gongo???

Tehe... teheeeeeMagezi...Umenifurahisha.Hakika, kijijini kwetu hapakuwa na hii pombe aina ya gongo!...Pombe inayotawala huko inaitwa KYINDI-mchnaganyiko wa mahindi na ulezi. Lakini pia kuna CHIMPUMU, ambayo ni pombe ya heshima sana. Hutumika katika matukio Maalum, kama ya kukirimia WAKWE wakiwasili!HiyO pombe ya Kyindi imekuwa inakorogwa na mama yangu kipindi chote hadi namaliza 4m 4!, na imesaidia mno kwa hali na mali, HAKIKA SIWEZI KUIDHARAU ILE POMBE, Vinginevyo nitakuwa naikana asili yangu..huh!..
 
Umeishi kijijini, na una kisa chochote? tupe basi!

binafsi sijazaliwa kijijini na sijakulia kijijini. Nimezaliwa mjini na kukulia mjini. Hata hivyo nimeishi kijijini na kufurahia maisha ya kijijini (kwa babu na bibi) ; kwenda ngomani, kuchota maji kisimani au kwenda kuoga mtoni kwenye mawe! Na baadaye nikafanya kazi vijijini kuanzia Bariadi, Nzega, Serengeti, Maramba, n.k Ni huko ndiko nikagundua kuwa nguvu ya mabadiliko ya taifa letu haiwezi kuletwa na watu wa mjini... hence the name!

Nisimulie nini kutoka kijijini? siku ile ambapo "tulibahatika" kuchungulia wali wa Kimakonde wakitolewa unyagoni mahali ambapo wanaume hawaruhusiwi kuwepo? Au nisimulie siku ambapo ulitogea ugomvi ngomani ambao ulisababisha vijana wa vijiji kadhaa kupigana hadi Polisi watoke mjini kuja kuzuia?

Au nisimulie siku ile mwenge wa Uhuru ulipopita kijijini kwetu na kutufanya wengine kuamini kuwa ilikuwa ni zawadi kubwa ya Mungu kwetu? Vipi kuhusu kwenda kukaa shambani kulima huku mmejipanga na mzee mmoja anawaimbisha nyimbo za kuhamasisha kwenye mashamba ya kijiji au yale ya kusaidiana na mkimaliza hapo mnakaribishwa kwenye ulanzi?

Au nielezee mojawapo ya vitu vinavyonisumbua nilivyoviona kule Nzega kwenye hospitali ya Misheni miaka ile ambapo karibu watoto waliozaliwa mwaka fulani walizaliwa wakiwa na kifafa kwa sababbu ya chanjo mbaya na hadi leo hakuna mtu aliyefuatilia? Ukienda kwenye hicho kijiji kiwango cha ugonjwa wa kifafa ni kikubwa kuliko inavyoweza kukadiriwa!
 
Ni kweli maana mzee wangu umepinda mpaka mgongo wako maana umebeba sana jembe lako, Hongera kwa kukaa kijijini
 
binafsi sijazaliwa kijijini na sijakulia kijijini. Nimezaliwa mjini na kukulia mjini. Hata hivyo nimeishi kijijini na kufurahia maisha ya kijijini (kwa babu na bibi) ; kwenda ngomani, kuchota maji kisimani au kwenda kuoga mtoni kwenye mawe! Na baadaye nikafanya kazi vijijini kuanzia Bariadi, Nzega, Serengeti, Maramba, n.k Ni huko ndiko nikagundua kuwa nguvu ya mabadiliko ya taifa letu haiwezi kuletwa na watu wa mjini... hence the name!

Au nisimulie siku ile mwenge wa Uhuru ulipopita kijijini kwetu na kutufanya wengine kuamini kuwa ilikuwa ni zawadi kubwa ya Mungu kwetu? Vipi kuhusu kwenda kukaa shambani kulima huku mmejipanga na mzee mmoja anawaimbisha nyimbo za kuhamasisha kwenye mashamba ya kijiji au yale ya kusaidiana na mkimaliza hapo mnakaribishwa kwenye ulanzi?

!

Loooo,
MKJJ,

Umenikumbusha kisa kilichotokea kijijini kwangu nikiwa shule ya Msingi!

Siku Mwenge ulipopita kijijini kwetu Kuna Mzee mmoja, kwa bahati mbaya katika pilikapilika za kuugusa mwenge(kwa kuamini kwamba una baraka za pekee) alimgonga skauti mmoja(japo hakuumia), lakini matokeo yake, baada ya mwezi kupita aliandikiwa barua toka serikalini/mkoani ikimtaka aandike maelezo kwanini aliutukana mwenge na kutaka kuukwamisha!

Hiyo ikawa ni ishu kubwa sana pale kijijini, maana hakuna akiyeacha kujua habari ya ujio wa barua hiyo kwa masikini mzee huyo. Ilibidi viongozi wa kijiji wakae kumsaidia kuijibu, na ikapelekwa mjini!
 
PJ hii Thread imenitoa machozi,imenikumbusha mbali saaaana,yaani nimekumbuka usiku tulikuwa tunakaaa nje tumeuzunguka moto huku tunapiga story,nimekumbuka pia tulikuwa tunachunga Ndama na Mbuzi pekupeku mapolini huku tukiokota kuni za kupikia,tunakwenda kuteka maji mtoni!!!!
 
Pole sana SWU.

Naamini kabisa kwamba wewe umekumbuka kiukweli yaliyojiri kipindi ukiwa kijijini.

Ukiangalia kwa umakini unakuta historia ya maisha yetu tulio wengi inashabihiana kwa kiasi kikubwa, na kwamba tumetoka kule tulikokuwa kupitia msaada wa Elimu.

Hakika tuna kila sababu ya kuwashukuru wazee wetu, na pale tupatapo hela ya sukari tusiwasahau
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom