Umefaidika nini na JF tangu ulipojiunga?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,782
Wapo waliopata wachumba na kuoana hapahapa JF, wapo wanaofanya biashara na kufanikiwa kupitia hapahapa JF, wapo wanaopata mawazo ya biashara na kijasiriamali.

Kuhusu elimu ndio usiseme, JF ni shule tosha. Marafiki pia wanapatikana kwa sana tu hapa mtandaoni, je wewe binafsi JF imekufanyia nini ambacho unaona ni kikubwa?
 
-Hapa nilipo nimepiga Tshirt na Jeans...all courtesy of www.jamiiforums.com.
-Nina marafiki(physical, not virtual) wapatao 50, wa kuaminika kabisa as far as maisha ya mujini is concerned!
-Nina marafiki(virtual) zaidi ya 200, ambao najua by 100% nikikutana nao ni full blast!
-I have gone to destinations i didnt dream of before!...www.jamiiforums.com took me there!
-Nimejifunza tabia, mpishano na mkwaruzano wa mawazo, kuvumiliana, kustahimili, love, hate, passion& all life ways!
-www.jamiiforums.com has been there for me during my saddest moments on Earth!...sitasahau hili!
and last, but not least, www.jamiiforums.com will soon be opening new doors of hope for me!
 
JF imenifanya nijue kwamba kupata mke mtandaoni ni jambo gumu sana!

Pia imenifanya nipate pahala pa kukimbilia nikitaka kubwatuka kwa kicheko - nako nikucheck mabandiko ya Bujibuji na yale ya Sura-ya-Kwanza yaliyopo!
 
1. Nimepata habari tele na majibu mengi kwa maswali yaliyokuwa yananisumbua
2. Nimejua raia waTanzania ni waaina gani? Hasa kwa maneno mengi vitendo kidogo
3.Ni sehemu yangu ya kujiburudisha ninapo kuwa na stress
4. Nimejua vitu vingi vinavyohusu nchi yangu na aina ya vioungozi tulio nao
5. Nimejua nani na nani ni mafisadi papa kwa undani zaidi
 
JF puts a smile on ma face even when there was supposed to be tears on ma cheeks.
Huwa nacheka,nawaza,nacalculate,naimagine,nafantasize,nakujifunza mengi sana
and above all,JF kwangu ni kisima cha habari
 
bwana mzee kwa muda mfupi sana niliokaa hapa nimejifunza jambo moja kubwa sana,kufikiri kabla ya kuongea!!!!!!!!!!!!hilo nilikuwa sina,,pia nimejifunza kuwa mvumilivu na kukubali kukosolewa,,,pia nimejifunza kumbe kuna watanzania wenye busara.
 
Nimejua jinsi Gani Watu wanaweza kufikiri,
Nimewajua Wenye Ubongo uloganda,
Nimewajua Watu wanaopenda Kuchallenge Kila kitu Hata ukiweka nukta watakuuliza kwanini,
Nimejua kwamba watzanzania wazalendo bado wapo,
Nemeona Jinsi Serikari yetu ilivokuwa Mbovu na ya Kifalme,
Nimeona Jinsi watu wanavoipenda CDM,
Nimewaona Makada wa CCM,
Nimeona Magamba ya CCM

Yaaaani nimekuwa Full informed, Mpaka najiogopa kwani kuna muda naanzaga kuyabishia mawazo yangu mwenyewe! Kudadek

Kama Kuna swali lingine weka ntakujibu
 
  • Thanks
Reactions: Paw
JF imenifanya nijue kwamba kupata mke mtandaoni ni jambo gumu sana!

Pia imenifanya nipate pahala pa kukimbilia nikitaka kubwatuka kwa kicheko - nako nikucheck mabandiko ya Bujibuji na yale ya Sura-ya-Kwanza yaliyopo!

Jamani my bujibuji wa moyo wangu.... Hhahahh hhahahhaha hahhahahahhahhah
 
JF puts a smile on ma face even when there was supposed to be tears on ma cheeks.
Huwa nacheka,nawaza,nacalculate,naimagine,nafantasize,nakujifunza mengi sana
and above all,JF kwangu ni kisima cha habari

u r so byutiful kudadake
 
Seriously, tangu nijiunge JF nimeingiwa na chuki dhidi ya dini zote "tulizoletewa" Waafrika. Nimejisomea na kuona ni jinsi gani jamaa wamefanikisha kutugawanya Wabantu na kutuacha tukifarakana kila leo hii huku wao wakipiga hatua za maendeleo katika jamii zao.
 
Mi nimefaidika na mengi isipokuwa 1 la msingi sana kwangu ni kuelewa kwa ukweli na ufasaha zaidi mambo mbali mbali (sana sana ya kisiasa) yanayoendelea nchini kwetu.
 
Napata habari hot ...najifunza mambo mengi ninayohitaji/nisiyoyahitaji.
WanaJF nimewafaham ni waungwana sana.
Humu ni bahari utapata utachotaka bila khiyana....lol.
Hakuna siku itapita bila kuangalia....nahisi nimeongeza kadigirii kengine humuJF.
 
Kwangu mimi ni haya:
1. Nimejifunza kungfu mpya za CDM
2. Nimejifunza juu ya aina za magambas
3. Nimejifunza jinsi ya kutumia utaalam wa kutumia maneno kiufasaha,mwalimu wangu akiwa Mwanakijiji.
4. Nimejifunza jinsi watu wanavyojua kuchambua pumba na mchele.
5. Nimejifunza watu wanavyosifia majaaliwa mbalimbali ya Watanzania.
6. Nimejifunza jinsi watu wanavyojua kuchambua mapenzi motomoto.
7. Nimejifunza juu ya experiences ambazo watu walizipitia maishani mwao hasa ya JKT, stori za utotoni, kwenye mapenzi, ndoa, kazi na mengineyo mengi.
 
Acheni utani, JF imekuwa ya msaada sana kwangu.
Nakumbuka zilikuwa zimebaki siku chache sana nifunge ndoa. Bestman wangu akawa haeleweki. Nikiwasiliana naye kuhusu mipango ya kwenda kufanya manunuzi (tena kwa ghalama zangu) ananikwepa. Nilipomkumbusha siku ya kwenda rehearsal na kubaini hatuko ukurasa mmoja nikachanganyikiwa. Haraka sana nikamkumbuka mtu mmoja aliyewahi kuniomba mchango wa harusi kwa PM hapa JF. Huyu mtu japo nilimchangia, hatukuwa tumewahi kukutana na wala hatukuwa tunajuana. Roho ikanituma kuwasiliana naye. Jibu lilikuwa, USIPATE SHIDA. Hivyo ndivyo ilivyokuwa JF ikawa imenipa Bestman and Best-friend. Asante sana JF, Udumu Milele
 
mimi nina penda sana siasa nilipoingia hapa jf ndipo nimepata kuijua siasa vizuri kwa sababu kuna vichwa hapa jf wanaoijua siasa si mchezo nimejifunzia hapa kujenga hoja na mambo mengi sana nawashukuru sana na wito wangu kwa yeyote mwenye kutaka kujua siasa na mambo mengi kuhusu mahusiano elimu afya uchumi karibu jf
 
Nimeijua kwa undani nchi yangu changamoto zinazoikabili pia nimefahamu inakotoka ilipo sasa hivi na inakoeleke
 
Nimeifahamu JF wakati nilipokuwa nataka kuchakachua modem yangu. Nikafanikiwa, the rest is a tale of discovery. Discovering truths, lies, laughs, joys, etc. Simply put, the whole of human whole!
 
Back
Top Bottom