Umaaarufu wa carol light unatokana na nini?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,885
Sina uhakika kama nimepatia jina hilo...
But naamini nimeeleweka...

Juzi nilikuwa sehemu hivi,kama restaurant hivi
akatokea mwanaume,umri over 50 kwa muonekano....
Sasa alikuwa anaonekana kama ana mikono mieusi
na uso mweupe hivi,kama kajichubua hivi....
Baadhi ya watu hasa kina dada waka aanza kumzungumza
so nikaona mazungumzo yanakwenda kwenye
kitu kimoja tu,ni mafuta nafikiri yanaitwa carol light..
Nikavuta kumbukumbu nikagundua kuwa hata kwenye nyimbo yanatajwa
haya mafuta.....
Sasa nimekuwa na maswali...

1.carol light ni nini hasa?mafuta?mkorogo?lotion?
2.kwa nini yamekuwa maarufu sana hasa kwa wadada
3.wanao tumia ni watu aina gani?
4.ni kweli yana madhara?tfda,serikali.tbs wapo wapi?
5.ni kweli yamepigwa maruku baadhi ya nchi?uganda?malawi?
6.tanzania ni kampuni gani inahusika na biashara hii?
7.nini kinaongezeka kwa mtumiaji?
8.kama ni mkorogo kwa nini umekuwa maarufu kuliko mingine?
9,na akina baba wanaotumia?inakuwaje?

10.au kuna kitu kingine kinaitwa carol light na sio huo mkorogo??????????
 
Nijuavyo mimi huo ni mkorogo wa kisasa. Umepaishwa sana na bibie Khadija Kopa aka Malkia wa Mipasho kwenye lile jisongi lake la Full Stop. Anakwambia yeye hababaishwi wala kutishwa na visichana vinavyopaka huo mkorogo. Yeye ni baby cutie wa Kiafrika na hataki uso wenye mabaka kama paka.

Kwa hiyo kwa kifupi ni mkorogo tu.
 
Hivi bado kuna watu wanajichubua. Binafsi hiyo caro light naisikia sana, ila sijawahi kuitumia. I really like the vaseline lotion.
 
mkuu mbona jina umelipatia sana lazima waijua hiyo noma kamanda

Natumaini unatania tu. Maana mtu kujua kitu si lazima ajihusishe nacho kihivyo. Kuna watu wengine tunapenda sana kujifunza na pindi tusikiapo ama tuonapo kitu ambacho ni kigeni na hatukijui basi tunapatwa na shauku ya kutaka kujifunza na kujua juu yake.
 
Hivi bado kuna watu wanajichubua. Binafsi hiyo caro light naisikia sana, ila sijawahi kuitumia. I really like the vaseline lotion.
Ni nzuri sana kwa ngozi yako! jaribu kuitumia ujionee
 
Natumaini unatania tu. Maana mtu kujua kitu si lazima ajihusishe nacho kihivyo. Kuna watu wengine tunapenda sana kujifunza na pindi tusikiapo ama tuonapo kitu ambacho ni kigeni na hatukijui basi tunapatwa na shauku ya kutaka kujifunza na kujua juu yake.

Mhhh.............
 
Ukitumia lazima after a month urudi kuomba ushauri kwa JF DR. 'Jamani nisaidieni ngozi yangu inakuwa na mabaka mabaka kama imeungua vile'
 
ni mkorogo upo juu kwa wadada/kaka tena ukienda kununua usisahau na maji yake........unakuwa mweupe........tahadhari usitembee kwenye jua maana uso unakuwa mwekundu kama umetoka kutwangwa makofi
 
si mnawaona akina nyoshi el sadat wanavyowakawaka hayo ndo matunda ya carol mweupee. waafrika lini tutajipenda sisi tulivyo? kila mtu anajifanya yeye mzungu kweli? basi hao wazungu wanawawekea sumu humoooo mkizaa mnazaa watoto wa ajabu ajabu tuuu
 
Mh! Hiyo sumu mbaya.
 
Huu mkorogo umeanzia West africa huko ukaingia Congo kinshasa to Bongo. Ni hatar wabongo wakaongeza na mambo yao balaa. Mwangalie Sauda mwilima wa star tv, hata baadh ya wabunge wanawake shurti wana mustach. Loo! Ntabaki mweus hv hv sitaki mabaka kama paka.
 
Caro light ni cream nzuri inayoweza kusababisha aliezaliwa 1961 awe na uso kama kazaliwa 2009, lakini miguu itafanana na ya mwanamgambo alietafuta uhuru mwaka 1950's.
 
Caro light ni cream nzuri inayoweza kusababisha aliezaliwa 1961 awe na uso kama kazaliwa 2009, lakini miguu itafanana na ya mwanamgambo alietafuta uhuru mwaka 1950's.
Kwahiyo kua mweupe ndio upya wa ngozi?!Na kua mweusi ndio uchakavu?! Kweli utumwa uko ndani ya ubongo wa mtu na sio vinginevyo.
 
Kwahiyo kua mweupe ndio upya wa ngozi?!Na kua mweusi ndio uchakavu?! Kweli utumwa uko ndani ya ubongo wa mtu na sio vinginevyo.
ulishawahi kujifungua mtoto kama mjaluo mzee? Au we mtumiaji? Mhh! Kweli hapa kuna kazi!
 
ulishawahi kujifungua mtoto kama mjaluo mzee? Au we mtumiaji? Mhh! Kweli hapa kuna kazi!

Kwahiyo weusi na uzee ni wapi na wapi?!Weupe na upya nao wapi na wapi?!

Ningekua mtumiaji nisingeshangaa unachoongea bali ningeungana na wewe.
 
Back
Top Bottom