Elections 2010 UmmaTunavyoweza kuhakikisha kura haziibiwi

B.Louis

Member
Aug 5, 2009
81
38
Ni matumaini yangu mu wazima nyote. Kwa mawazo yangu ninaona ni vyema taasisi na asasi zote binafsi kufungua ama kuanzisha mtandao ambao utakua ukikusanya matokeo ya kila jimbo.

Mfano, Jamiiforums inaweza kutumia fursa kwa kuwahusisha wanajamii (wanaoaminika) walioko nchi nzima kupost matokeo katika majimbo yao punde tu uhesabu wa kura unapoisha. Hii itatusaidia, kwani pindi tume ya uchaguzi itakapotangaza matokeo "rasmi" nchi (umma) utakua umeshajua matokeo kwani si siri. Lakini pia itatia changamoto na ni njia mojawapo ya kudhibiti hasa wanaofikiria au kutegemea kuiba kura.

Tanzania professionals Network (TPN), TAMWA, na taasisi nyingine zaweza tusaidia kukusanya matokeo na kupata idadi "huru" kwani kama tunvyojua tume yetu ya uchaguzi si huru 100%. Kama lengo ni jema, gharama na mengineyo nadhani yanajadilika na hayawezi kuwa pingamizi katika kulitimiza.Inawezekana kabisa hili lisiwe jibu kamili katika kuzuia tatizo, lakini ni vizuri kuboresha kwani nadhani ni kwa kusudio sahihi.
 
Back
Top Bottom