Ultimatum: Serikali ina siku 14 kutangaza mahakama ya Kadhi! - Wahadhiri

Status
Not open for further replies.
halafu dhana hii ya utegemezi ni mbovu kabisa!!! jifunze kujitegemea!!!kama unataka kusaidiwa kwa masharti hayo,si lazima wakusaidie ukiwa huku,unaweza kwenda huko kwao ukafaidike vzr na hiyo misaada unayofdhani huwezi ipata ukiwa huku!!

Nitajie Shule au Hospitali iliyojengwa na Wakristo wa Tanzania bila Msaada wa NJE ya Nchi?
 
balaghasia siyo vazi la waislamu pekee yao. Ile ni kofia tu kama kofia zingine, hivyo yeyote anaweza kuvaa. Mimi ninamvalisha mbwa wangu hapa nyumbani.


unamaanisha unamvalisha mwanao? Sababu hakuna mbwa anvaa balaghashia, kama una mean mbwa basi wewe unamatatizo, kamuone mwana sakojia.

Balagashia nivazi la kiislam silakikristo, taarifa.
 
Jamani,

Mimi sielewi kitu kimoja; naomba msaada - mahakama ya kadhi itakuwa ya waislamu, na siyo ya serikali; sasa ni kwa nini waislamu wanataka serikali ndiyo iwaanzishie hiyo mahakama? Kwa nini wasianzishe wao wenyewe huko misikitini or wherever?

Jifunze Historia.....Mahakama ya Kadhi ilikuwepo before na wakati wa COLONY Time....Nyerere ndie aliekuja kuvunja...!!!

Mahakama ya Kadhi itachukua nafasi kupunguza Kesi nyingi ktk Mahakama za Kisekula. Maamuzi yake hayataweza kubadilishwa na Mahakama za Kisekula.

Kama Umesoma Laws..utaambiwa...Islam has a complete guidance ktk Family and Inheritance Laws....!!!
 
Tueleze ukweli wewe maana najua unafahamu sababu wala haikuwa uonevu, hata mimi ningeweza kuwafukuza.


ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya..., hiyo ndio strategies inayotumika,

hakuna atakayeamini au kuulewa ukweli wa dhuluma zitendekazo ila kwa wale yanayowagusa, ili kuwa na amani! amini ukweli ulionao nami nabaki na ukweli nilionao, itakuwa mjadala usio na mwisho!
 
unamaanisha unamvalisha mwanao? Sababu hakuna mbwa anvaa balaghashia, kama una mean mbwa basi wewe unamatatizo, kamuone mwana sakojia.

Balagashia nivazi la kiislam silakikristo, taarifa.


Kwi kwi kwi....kaaazi kweli kweli..!! Anyway, you made my day bro!
 
Kwasababu wanataka iwe na nguvu ya kiserikali na serikali iwalipie gharama za kuiendesha. Kazi kweli kweli hawa watoto wa mjakazi. Akili zimebunguliwa na madrasa hawawezi hata kufikiria mambo ya maana.
Kwa kweli MUNGU apishie mbali maana naona statement kama za akina Bull zinaonyesha tayari wanajiandaa kwa jihad. Mabomu ya Mbagala na kwingineko inabidi yahifadhiwe vizuri maana hawa jamaa hawachelewi kwenda kuyachukua na kuanza kujilipua.

kwa statement hizo, nadhani mungu hakustahili hata kutajwa hapo, anyway, mungu atakulipa kwa kauli zako ewe mwenye akili zisizo nahitilafu, mwingi wa uelewa,

Asante kwa niaba ya waliobunguliwa akili

 
Kwakweli hata mimi sielewi kwanini bwana mkubwa yuko kimya kwenye issue sensitive kama hii. It is so dangerous kwa kweli.


issue inakuzwa, Sidhani kama mkuu anatakiwa a-react kwa kufuata media, muda ukifika atatoa tamko lake,

jazba tunazo sisi, kila siku tunatoa habari mpya, angalia tu thread ngapi zimebandikwa hapa JF kuhusu habari hii, nyingine hata kuitwa tetesi hazifai, mtu akiona keyboard tu anafikiria aanze vipi iliapate supporta mtu ana andika atakapojisikia,

 
Je hii mahakama ya kadhi ni sawa na zile islamic courts za Somalia?
Asiyejua matatizo ya mahakama za namna hii aangalie somalia wanavyouana na kuikimbia nchi.
Asiyejua matatizo ya kukaribisha udini katika serikali aangalie huko.
Waislamu tusidanganyane; katika sheria za kiislamu dini ni serikali na serikali ni dini, je hili litafanyaje kazi Tanzania? Je wakristo nao wakiamua kuanzisha mahakama zao, si inamaana serikali itabaki na mahakama za wasio na dini (wenye dini za asili)? Lakini nao hao wana sheria zao ambazo nao wanaweza kuanzisha mahakama zao!
Ebu mtueleze ni wapi katika Quran tukufu palipoandikwa kuwa mahakama ya kadhi ni sehemu ya ibada; au palipoandikwa kuwa mahakama ya kadhi ni nguzo ya uislamu?
Tuwe makini na vitu hivi maana migongano ya kidini ikianza hakuna atakayekaa kwa amani, si muislamu wala mkristu wala wa dini za asili!

Hao wanaoturubuni tuanze migongano hiyo watakuwa kwao wamekaa wanapata sharbati baridi sisi tunakimbizana juani na kulala njaa.
Hivi CCM ikitupatia hizo mahakama basi tuichague kwa sababu hiyo tu? maovu mengine tuyaache? Lets be reasonable.
 
[/LEFT]

Unajua CCM walidhani ni lelemama, sasa subili yanayo kuja! Yaani mungu atunusuru. Kama sasa ni amri za siku za kuhesabika, Sijui, sijui tunako enda!
mkuu unajuaa serikali hii inafanya mambo kimzaha mzaha.kwenye mambo ya msingi wanaleta mzaha.yaleyale ya wauwaji wa albino wauwawe kumbana mzee anamwaga machozi sasa hili la mahakama ya kadhi wao wenyewe waliweka kwenye ilani sasa watajuutaa kuwafahamu waislam
 
Sasa kamauelewi kajifunze kwenza acha kuleta blablaa, kwanza takasha kiswahili chako? alfu ndo ujekuuliza maswali ako> vibalagashia ndio walioleta UHuru na pia Julius aliva kibalagashia wakati huo Pork eater wanafubaishwa akili na wakoloni. Jufunze history ya nchii hii.

Sasa hivi umeletwa mjini na serikali ya CCM vitabu vingi tu vya kiswahili na vya Historia ya nchi. Nyerere kavalishwa balaghasia hakuvaa msalaba wakati tunagombania uhuru na Swaumu pia tulimfungisha! Kelbu we!!


Lugha gani unaandika wewe? Halafu hizo za kusema dini fulani ilileta uhuru ni propaganda zisizo na maana, Nyerere kaanza vuguvugu la kudai uhuru toka akiwa mwanafunzi Tabora na Makerere. Alipokija mjini Dar ndio akashirikiana na wananchi wengine wa wa huku. Uhuru ni zao la juhudi na umoja wa wananchi sio dini. Na kwa taarifa yako, mapambano dhidi ya ukolono yalikuwepo tangu kina Mkwawa, Mirambo, Kimweri, Nyngu ya Mawe na Kinjekitile. Weka historia vizuri, usitumie mtukutio(emotion) kujadili vitu sensitive, wananchi wote kwa nafasi zao mbalimbali walishiriki na kama kusingekuwa na umoja wa wananchi basi uhuru ingekuwa ndoto
 
Wako mahakimu wangapi kwa ajili ya mahakama hii????
Au wakipewa ruksa ndo watawatafuta?
nieleweshwe tafaaaaaaaaaaaaaadhali
 
[/I][/SIZE]

Lugha gani unaandika wewe? Halafu hizo za kusema dini fulani ilileta uhuru ni propaganda zisizo na maana, Nyerere kaanza vuguvugu la kudai uhuru toka akiwa mwanafunzi Tabora na Makerere. Alipokija mjini Dar ndio akashirikiana na wananchi wengine wa wa huku. Uhuru ni zao la juhudi na umoja wa wananchi sio dini. Na kwa taarifa yako, mapambano dhidi ya ukolono yalikuwepo tangu kina Mkwawa, Mirambo, Kimweri, Nyngu ya Mawe na Kinjekitile. Weka historia vizuri, usitumie mtukutio(emotion) kujadili vitu sensitive, wananchi wote kwa nafasi zao mbalimbali walishiriki na kama kusingekuwa na umoja wa wananchi basi uhuru ingekuwa ndoto

Mkuu Bunduki kumbuka unajibizana na , 'Bull'
sorry am out!
 
Hao ni wababaishaji tu,wasome katiba ya nchi.OIC na KADHI havipo,labda wanapewa kiburi na magaidi.
 
Swali: Kama BAKWATA ni chombo kama chombo kingine cha Waislamu na hivyo hakiwezi kuzungumza kwa niaba ya Waislamu wote je Jumuiya ya Wahadhiri inazungumza kwa niaba ya Waislamu wote au nayo ni chombo kingine cha Waislamu na hivyo hakiwezi kuzungumza kama sauti moja ya Waislamu?

a. Kama JWK (Jumuiya Wahadhiri wa Kiislamu) siyo chombo cha Waislamu wote basi hakina uwezo wa kuipa serikali siku 14 kwa niaba ya Waislamu wote

b. Kama JWK ni chombo cha kuwawakilisha Waislamu wote basi BAKWATA iseme kama inaunga mkono mkwara huo. Kama walioko BAKWATA hawaungu mkono basi JWK haiwakilishi Waislamu wote.

c. Kama (a) na (b) ni kweli, basi ultimatum ya siku 14 haina msingi katika Waislamu na haiwezi kuilazimisha serikali kufanya jambo lolote.

d. Kama (a) ni kweli, na (b) ni kweli na (c) ni kweli; basi Waislamu wakae chini na kuunda chombo kimoja ambacho kitazungumza kwa sauti moja ya Waislamu. Chombo hicho kinaweza kuwa muamvuli wa vyombo vingine vya Waislamu. Chombo hicho kitakachoundwa ndicho kitatakiwa kiwakilishe misimamo rasmi ya Waislamu kama Kundi. Hii itafanana na TEC ambayo inazungumza kwa niaba ya Wakatoliki wote (siyo Wakristu wote); TCC inayozungumza kwa niaba ya makanisa ya Kiprotestant na TPC inayozungumza kwa niaba ya makanisa ya Kipentekoste.

Hii ina maana hata kama haiwezekani kuunganisha Waislamu wote basi wanaweza kujipanga kwa kufuata madhehebu yao. Kuwe na chombo cha kuwakilisha Sunni, Shia na Ahmaddiya n.k Pasipo Waislamu kuunda umoja wa aina hiyo watajikuta mara nyingi wanagawanyika katika misimamo yao.

Kwa sababu hata Mahakama ya Kadhi ikiundwa haina maana itakuwa imewaunganisha Waislamu kwani katika applications za sheria hizo itabidi bado wataalamu/wanazuoni wa ilimu mbalimbali kutoka madhehebu mbalimbali kuweza kukubaliana katika masuala kadha wa kadha.
 
Last edited:
Huku kijijini kwetu hakuna muislamu hata mumoja:). Je tuwashawishi wapigie chama gani wasio waislamu kwetu:D
CCM kazi mnayo maana very soon tutaona ccm MYK na ccm kanisa. Kwa kosa mlilofanya lazima, narudia lazima mkatike mara mbili. Njia ya muongo ni fupi. Hata wakristo hawadanganywi tena kirahisi ili mpate kura zao:(.

Nakauka kucheka ndipo watajaza na uongo wao,CCm mwaka huu watalijua jiji
 
Wengi tunafuatilia mijadala ndani ya Bunge, hivi karibuni tulimsikia Mh slaa akisema ataikwamisha bajeti ikiwa mashirika ya dini hayatafutiwa msmaha, lkn tunajua waliokuwa wanapiga kelele ni Dini Fulani. Kuhusu MAHAKAMA ya kadhi Mzee huyu na Kijana Huyu Kimya , Kuhusu Mkataba kati ya kanisa na Serekali kimya haibani serekeli na kutafuta nyaraka ili aibane govt, Kuhusu tamko la maaskofu kimya ? Kuhusu Vertican Kimya hata kutaka hayo majibu ya Ovyo ovyo hamyataki
 
Jamani,

Mimi sielewi kitu kimoja; naomba msaada - mahakama ya kadhi itakuwa ya waislamu, na siyo ya serikali; sasa ni kwa nini waislamu wanataka serikali ndiyo iwaanzishie hiyo mahakama? Kwa nini wasianzishe wao wenyewe huko misikitini or wherever?


Kwasababu itakuwa haina nguvu kisheria za nchi nchini.

Umeelewa?

FP
 
Kwasababu itakuwa haina nguvu kisheria za nchi nchini.

Umeelewa?

FP

FP:

Kanisa Katoliki lina Mahakama za Kanisa Katoliki ambazo zinasimamia na kila Jimbo. Mahakama hizo zinahusu mambo ya ndoa na ibada vile vile. Mahakama hizo zinaongozwa na Canon Law (Sheria ya Kanisa). Sheria ya Kanisa siyo sawa na Sheria ya Nchi (Civil Law).

Mahakama za Kanisa zina mawakili, na majaji na waendesha mashtaka. As a matter of fact neno tunalolitumia la diabolis advocatum (Wakili wa Shetani) msingi wake ni kwenye mahakama za Kanisa ambapo mtu anayetarajiwa kutangazwa mtakatifu anakuwa na wakili wa kumtetea na wakili ambaye atayaonesha mabaya yake (hence Wakili wa Shetani).

Mahakama hizo za Kanisa maamuzi yake yanatambulika kisheria za nchi kwani ni sehemu ya Kanisa Katoliki. Hivyo, Kanisa Katoliki likiamua kufuta ndoa (annulment) basi hiyo ndoa inafutwa hata kwenye sheria za nchi ( baada ya kufuata taratibu). Kanisa Katoliki likimfungia Askofu (kama ilivyofanya Same) askofu huyo ana haki ya kukata rufaa hadi kwa Papa (ambaye ndiye Jaji Mkuu na wa Pekee wa Rufaa). Maamuzi hayo hayawezi kuingiliwa na Mahakama za ndani.

Mahakama hizi Katoliki huendeshwa kwa sadaka za Wakatoliki wenyewe na michango kutoka kwa nchi nyingine.

Hata leo ukienda Jimbo la Dar kwa mfano na ukiuliza muundo wa Mahakama ya Kanisa jimbo la Dar utaambiwa na kesi mbalimbali ambazo zimewahi kufikishwa kwenye mahakama hizo na kutolewa maamuzi.

Kwa hiyo:

a. Mahakama za kidini Tanzania tayari zipo
b. Zinafanya kazi
c. Zinaendeshwa na waumini wenyewe
d. Maamuzi yake yanatambuliwa na nchi
e. Hazikuanzishwa na serikali, kufadhiliwa au kwa namna yoyote ile kujadiliwa bungeni. Zimeanzishwa by the very fact kwamba ni sehemu ya dini hizo.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom