Ulta sound ilionesha mapacha, kazaliwa mmoja inawezekana?

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Wana jamvi naomba mnisaidie, mke wangu alikuwa mjamzito. Alianzia kliniki Temeke hospital, akaambiwa atajifungua watoto mapacha baada ya vipimo vya ultra sound. Akahamishiwa hospitali ya Muhimbili ambako pia akaambiwa atajifungua watoto mapacha. Na alijifungua kwa oparesheni mtoto mmoja. Je hapa hakuna uchakachuaji au inawezekana vipimo vikakosea katika hospitali mbili tofauti?
 
mtoto mmoja kauzwa wakati mama bado amelala kwa dawa ya usingizi. ashukuru kupewa huyo mmoja, la sivyo angeweza kuambiwa wote wamekufa!

macinkus
 
Hapana usiogope, wakati mwingine mtoto anakuwa ametanguliza ****** sasa kwa kuangalia tu wanaona kama ni watoto wawili, na ndo maana kafanyiwa upasuaji.
 
Wana jamvi naomba mnisaidie, mke wangu alikuwa mjamzito. Alianzia kliniki Temeke hospital, akaambiwa atajifungua watoto mapacha baada ya vipimo vya ultra sound. Akahamishiwa hospitali ya Muhimbili ambako pia akaambiwa atajifungua watoto mapacha. Na alijifungua kwa oparesheni mtoto mmoja. Je hapa hakuna uchakachuaji au inawezekana vipimo vikakosea katika hospitali mbili tofauti?

Umejaribu kuwauliza wahusika (waliofanya operation) wanasemaje? Kama hata mapigo ya moyo yaliashiria kuwapo kwa viumbe wawili tumboni na baadae akatolewa mmoja, naamini kuna maelezo zaidi yanahitajika.
 
Chukua picha ndugu yangu peleka kwa wataalamu wakusomee. Inawezekana wamecheza mchezo. Ila inabidi jamani muwepo pembeni ya wake zenu pale wanapofanyiwa operation.
 
Hapo tafuta maelezo ya kina. Kwanza nadhani watoto mapacha in most case wanazaliwa na kilo chache. Sasa mtoto wako alikuwa na kilo ngapi? Kama ni kweli walikosea kusoma utrasound basi huyo mtoto lazima atakuwa ni mkubwa maana mimba ya mapacha kutoka mtoto mmoja lazima baby alikuwa mkubwa. Otherwise kilo zake kama zilikuwa chache umepigwa changa la macho.
 
Back
Top Bottom