Ulishawahi kukumbana na vitimbi vya kichawi? Soma hapa

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,363
11,147
Mwaka 2003 niliwahi kuishi kwa muda wa kama miezi 7 katika kijiji kimoja pembezoni mwa wliaya ya Biharamulo nikiwa mimi na rafiki yangu.Kabla ya kwenda huko tulihadithiwa na mmoja wa watu walioshi huko namna kulivyokuwa na vitimbi vya kishirikina...Lakini tukapiga moyo konde na kwenda (kama mnavyojua harakati za kusaka shilingi).

Tulifika na kuishi vyema na wenyeji.kadri siku zivyokuwa zinakwenda baadhi ya watu ambao tulikuwa tumejenga urafiki nao walikuwa kila mara wanatuuliza kama tumeshuhudia chochote toka tuishi hapo,nasi tuliwajibu hakuna chochote kipya,kumbuka walikuwa wanatuuliza kwa namna ya mafumbo lakini lengo lao ni kujua kama tumekumbana na vitimbi vyovyote vya kishirikina.

Tulikuwa tumepanga vyumba viwili tofauti mimi na huyo rafiki yangu lakini katika nyumba yenye compound moja.Vitimbi vikaanza kwa rafiki yangu,akiwa amelala akasikia vishindo kwenye bati..kusikiliza vizuri ailikuwa ni paka aliyekuwa analia na kukanyaga kwa vishindo ambavyo sauti yake ilikuwa mithili ya jiwe kubwa lillokuwa linapondwa kwenye bati - akatulia -lakini kwa hofu kidogo.Baadae usingizi ukampitia.Alipoamka yupo pembeni mwa geti la mlango..hana hamu.

Baada ya siku 2 ikawa zamu yangu.Wakati nipo usingizini nikahisi kama kiu-baridi,kustuka mlango upo wazi...nikatoka kitandani nikaufunga kwa kujipa moyo kwamba pengine nilisahau.Nikarudi usingizini.Usingizi mtamu,ghafla nikasikia honi za magari na mwanga mkali wa taa..kuamka siwezi lakini nahisi kabisa sio ndoto.Daah....nilipiga kelele Yesuuu (me ni mkristo).Nikastuka tena na kukuta mlango upo wazi kabisa huku mwili ukiwa karibu kabisa ya mlango.Nikamwta mwenzangu tukapiga story mpaka kukakucha.

Kifupi baada ya mwezi 1 tuliondoka huku wenyeji wakishangaa namna tulivyoishi bila kuonyesha wala kuhadithia vitimbi vyovyote,na kubwa zaidi kwamba tumeaga badala ya kuondoka kimyakimya!!
 
Muheshimiwa mlihakiki vilikua ni real vituko,? Na si Cellebral Maleria ?
 
Hata huku kwetu(sweeden) wamo wengi tu!
ila wanakuja kama warewolves.
 
Yalitukuta aisee by the way baada ya tukio la kwanza tukawa tunasali kabla ya kulala

maombi kwa mkristo ni LAZIMA,yaani ni kama chakula msisubiri yawakute ya kuwakuta ndo msali
nice experience though,mtakuwa mnawahakikishia wale wanaosema hakuna uchawi.
uchawi upo tena with grades,na ni tofauti kulingana na maeneo.
 
Aisee mna moyo!
Mie nadhani kesho yake ningetoweka eneo hilo bla hata ya kuaga lol!
 
Aisee mna moyo!
Mie nadhani kesho yake ningetoweka eneo hilo bla hata ya kuaga lol!

Ilibidi tuvumilie, kwanza ngawira tunataka,pili tulishapata story nyingi kabla kuhusu hilo eneo kwa hiyo tukapata ka-ujasiri kidogo ka kuishi.Wenyewe wanasema wakikushindwa hapo wanaenda visiwani kufuata mizinga mipya!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom