Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,227
- 113,582
hivi kuna mtaa kule uswahili enzi zile ambao ulikosa jumba bovu? ila bahati mbaya jumba bovu la mtaani kwetu lilikuwa na mashetani....lol
Enzi zile hasa kwa sisi tuliozaliwa na kukulia Dar sidhani kama Uswazini kulikuwa kuna mtaa uliokuwa hauna jumba bovu. Unajua watu walikuwa wanaanza kujenga halafu sijui nini kinatokea ujenzi unaishia njiani. Basi hiyo ilisababisha kuwepo na majumba mabovu kibao. Nadhani wengi wa wamiliki wa hayo majumba walikuwa ni wale wahujumu uchumi na kilipowaungulia basi wakashindwa kuendelea na ujenzi wao.
Mijumba mibovu mingi ya mtaani kwetu ilikuwa na kenge kibao na mimbwa koko.