Uliomba kazi,ukapewa kazi. Husione kazi,kufanya kazi.

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,314
10,775
Salaam wana JF.

Huo ni ujumbe kwa wafanyakazi wote,popote pale walipo. Kuanzia wasaidizi wa ndani,wafigizi wa barabara,makondakta na madereva wa mabasi,hadi kwa rais wa JMT.

Watanzania tumezidi kuona kazi,kufanya kazi,wakati hakuna aliyetulazimisha kuomba na kutafuta kazi. Kazi tunazitafuta kwa gharama zozote zile (wengine hadi kwa kuuza utu wao!),lakini linapokuja suala la kutimiza yale uliyosema unayaweza (kama ulivyosema kwenye barua ya ombi la kazi na CV),inakuwa tabu na nongwa.

Unaweza kuingia ofisi ya umma ama binafsi na kukutana na katibu muhutasi aliyenuna na anayetoa majibu kama hana ndugu ama wazazi! Mbaya zaidi ukifanikiwa kusikilizwa na kumuona bosi,unakutana na bosi aliyebusy na simu na wavuti,kisha shida yako itapigwa tarehe mpaka soli za viatu zitazomea.

Ukienda kwenye taasisi za elimu,unakutana na wahadhiri ambao wao kumsimamia mwanafunzi wa uzamili au uzamivu wanaona kazi. Unakuta mwanafunzi badala ya kusoma kwa miezi 18,anasoma kwa miezi 36 au zaidi (hii ni kwa upande wa shahada ya uzamili). Ingawa kuna sababu jingine zinazoweza kusababisha,ukweli unabaki kuwa wahadhiri wengi wanaona kazi kutimiza wajibu wao katika kusimamia wanafunzi;wanatumia muda mwingi katika consultancies,tafiti na biashara zao binafsi.

Wandugu, tufanye kazi kwa bidii; tusione kazi,kufanya kazi,kwa vile tuliomba kazi tukapewa kazi.
 
chezea mshahara na sio kazi
unakuta file zina kaa mpaka vumbi mezani kwa mtu mwenye shida anambiwa file halionekani
 
chezea mshahara na sio kazi
unakuta file zina kaa mpaka vumbi mezani kwa mtu mwenye shida anambiwa file halionekani

Umenikumbusha lile tangazo la Twaweza,ambapo katuni ya Masoud Kipanya inaonyesha jinsi watu walioomba kazi na kupata kazi,wanavyoona kazi kufanya kazi zao.
 
Ukiona kazi kufanya kazi
Acha kazi
Uone kazi kutafuta kazi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom