Ulinzi wa kizamani huu siasa za Tanzania zimekosa wabunifu?

Rais George Bush wa Marekani alipotembelea Tanzania alichopoka toka kwenye kundi kubwa lililomzingira nyuma yake na kwenda kumkumbatia mama mmoja aliyekuwa anamshangilia. Tendo lile naweza kulitafsiri kama alikimbia wimbi la kundi lililokuwa linamfuata bora aende kwa kwa yule mama pembeni atapata hewa zaidi.
:pound:
 
_44865683_-6.jpg
India.jpg

Tunachoongelea hapa ni update ya system katika masuala ya ulinzi wa viongozi. Mtindo huu tulio nao ni ule tulioachiwa na wakoloni wa kiingereza nusu karne iliyopita, hakuna jitihada zilizofanyika kuboresha au to update system.
Rais analindwa na mlinzi aliyevaa magwanda kama ya polisi magereza, je ni mfungwa? Kwa nini asiwe na walinzi smart ambao hawaonikani tofauti na mvao wa viongozi anaoambatana nao?
Pia mfumo wa ulinzi ambao raiz huzingirwa na kundi kubwa ni wa kizamani mno, kwani leo kuna teknology ambayo huhitaji kundi kubwa hivi. Utaona hata ndani ya chumba nyuma ya rais ambako kuna ukuta yupo bodigadi, hata haiingii akiiini kabisa analinda nini mgongoni kwa rais.

Rais akiwa uwanja wa ndege unaona walinzi wanamfuata kwa nyumba na wengine wamefunga njia mbele, anashindwa rais hata kupata fresh air ndio maana mara kadhaa amaangaka jukwaani sababu ya kuwamliziwa hewa kutokana na afya yake kudumaa kidogo.
Nani alikwambia huyo ni mlinzi, au kwa kuwa kasimama nyuma ya rais basi ukaconclude kuwa ni mlinzi? Well huyo anaitwa Aide de camp au kwa kiswahili mpambe. Unless uko kwenye PPU ndio unaweza kujua kama wameboresha au la, kuna documentary moja Us Secret Service jamaa alisema "kuna mengi yanayotokea na kuendelea nyuma pazia ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyaona".

Tumejadili sana walinzi wa Kikwete na viongozi wengine kwenye ile thread ya Walinzi wa viongozi, inapatikana hapa.

Bush alivyokuja Tanzania alikuwa na aide de camp
BushTZ7.jpg
Bush%2Bin%2BTanzania%2B%2B2.16.08%2B%2B%2B2.jpg
 
Hapo nawakatalia wakuu,walinzi wa rais sio hao mapolisi!....na walinzi wengi wa rais wamekopeshwa sana na marais wengine kama kabila.....so,I disagree.
 
Huyu mwenye uniform si mlinzi wa raisi ila ni msaidizi wa raisi anaitwa ADC (aide-de-camp) Kazi yake ni kubeba mafaili ya hotuba ya raisi na vitu vidogo kama raisi atahitaji papo kwa papo. So kabla ya kuanza kuponda elimika kwanza.

kama ni porter wa rais na si mlinzi kwa madai yako kwa nini anakuwa kanali wa jeshi? mimi naamini naye ni sehemu ya walinzi wa mkulu
 
India.jpg
Nilishawali post kitu kama hiki siku chache zilizopita. Mlinzi wa Rais alivyo ni sawa na mpambe tu. Angalieni tofauti ya mlinzi wa Waziri Mkuu wa India alivyo smart na asivyoweza kugundulika kirahisi kama mlinzi, na kisha oanisha na mlinzi wa Rais wa Tanzania alivyopambwa na nguo za polisi magereza na kofia inayoonekana toka mbali kama mashua baharini. Uzamani huu utaisha lini?

Ukiona polisi wanavyotembea na magobole yao mitaani atamfukuzaje mhalifu wakati gobole lile linazidi urefu wake. Kununua bastola ni gharama ndogo sana ukilinganisha na pesa wanazolipishana posho wajanja tokana na kodi zetu.

Mbona kama mfupi kuliko JK,atawezaje kuona mbele kama kuna kitu kinatokea..
 
Rais analindwa zaidi ya unavyofikiria. Katika eneo ambao Rais yupo kuna walinzi ambao hata ukiambiwa hutaamini. Kama unataka kuamini nenda jaribu kumgusa uone watakaokushulikia, huyo anayemwona huenda hatakugusa. Acha kudharau kila kitu chako, kipende chako. Usipokipenda nani atakipenda?
 
Hakuna asiyejua hilo, tunalojadili hapa ni je, hatuweze update hii system tuliyoachiwa na mkoloni Mwingereza? Enzi hizo huko uingereza walikuwa wanafanya hivyo, lakini leo ni utaratibu unaoendana na wakati
 
Why change kama inafanya kazi inayotakiwa?
 
Hakuna asiyejua hilo, tunalojadili hapa ni je, hatuweze update hii system tuliyoachiwa na mkoloni Mwingereza? Enzi hizo huko uingereza walikuwa wanafanya hivyo, lakini leo ni utaratibu unaoendana na wakati
Wewe unafanya kazi PSU mpaka ujie hawaja update system?
 
Kama inafanya kazi bado mbona wanammalizia hewa Rais hadi anaanguka jukwaani, fikiri kama atazungukwa hivyo kwa masaa kadhaa ni dhahiri hewa safi hapati.
Kati ya Kikwete na say Obama nani ambaye anazungukwa na walinzi wengi? Mind you popote anapoenda Obama (nje ya white house) anakuwa na walinzi si chini ya 250.
 
Kati ya Kikwete na say Obama nani ambaye anazungukwa na walinzi wengi? Mind you popote anapoenda Obama (nje ya white house) anakuwa na walinzi si chini ya 250.

Mjadala si idadi ya walinzi ila namna na uboreshaji wa ulinzi wa kisasa. System yetu bado ile ya mwaka 47 ambapo ulinzi wa Magavana wa Tanganyika Trustship ilivyobuniwa na Wakoloni waingereza. Huu mtindo ni wa magavana Donald Cameroon na Sr. Edward Twining mwaka 1947 bado tunautumia Tanzania ya leo mwaka 2011.
 
Wahenga walisema jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Huwezi kujua kila kitu. Kujifanya unajua kila kitu ni sawa na kuingilia fani za wengine huku ukionekana kama unababaisha baisha tu. stick to ur professional na walio na professional zao waache sio kujifanya mjuaji kumbe upo mweupe. Mtu hajui hata role ya huyo askari anasimama kama symbol gani unakimbilia tu kubwatuka. Kam hujui kitu utapungukiwa nini kwa kunyamaza kimya. Kile ambacho si cha fani yako kiachee usidandie tu treni kwa mbele
 
kuna thread moja ilikuja hapa kama mwezi umepita, ilikuwa inauliza yule mzee anasimama nyuma ya raisi ni nani,nimeitafuta siipati,nilicheka sana siku ile,naomba ileteni tena il;e thread!pls
 
Ulisema hivi
Kama inafanya kazi bado mbona wanammalizia hewa Rais hadi anaanguka jukwaani, fikiri kama atazungukwa hivyo kwa masaa kadhaa ni dhahiri hewa safi hapati.
Nilivyokuuliza kati ya Obama na Kikwete nani aliyezungukwa na walinzi wengi ukajibu,
Mjadala si idadi ya walinzi ila namna na uboreshaji wa ulinzi wa kisasa. System yetu bado ile ya mwaka 47 ambapo ulinzi wa Magavana wa Tanganyika Trustship ilivyobuniwa na Wakoloni waingereza. Huu mtindo ni wa magavana Donald Cameroon na Sr. Edward Twining mwaka 1947 bado tunautumia Tanzania ya leo mwaka 2011.
Mkuu sijui lini umeanza kufuatilia walinzi wa rais, heck for all I know unaweza kuwa mmoja wao lakini naweza kukuambia kuanzia 2005 mpaka leo kumekuwa na tofauti kubwa sana na improvement nyingi tuwape credits. Kwa Tanzania threat level ya usalama wa maisha ya rais iko chini sana.
 
Wahenga walisema jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Huwezi kujua kila kitu. Kujifanya unajua kila kitu ni sawa na kuingilia fani za wengine huku ukionekana kama unababaisha baisha tu. stick to ur professional na walio na professional zao waache sio kujifanya mjuaji kumbe upo mweupe. Mtu hajui hata role ya huyo askari anasimama kama symbol gani unakimbilia tu kubwatuka. Kam hujui kitu utapungukiwa nini kwa kunyamaza kimya. Kile ambacho si cha fani yako kiachee usidandie tu treni kwa mbele

Hapa ni uwanja wa great thinkers, na tunajali hoja, kama unatoa hoja tunakupongeza kwa uungwana wako, lakini hii resistance unayofanya haitusaidii wengine wenye kutaka kupanuana fikra katika majadiliano yetu. Kama majadiliano yetu yanakuudhi ukiwa mmoja wapo katika system hiyo just quit, au donoa mazuri tunayopendekeza na ukiwa na moyo wa subira unaweza kujifunza kitu kutokana na haya tunayoongolea. Wengi wa wachangiaji hapa ni watu pengine wenye uzoefu katika masuala hayo si kwa tanzania tu ila wanajaribu kuoanisha na mataifa mengine walivyojaribu to update system. Ukiona inakuumiza ndugu yangu waachie wenyewe waendelee we nenda thread nyingine ambayo wajisiki comfortable.
 
Ulisema hivi

Nilivyokuuliza kati ya Obama na Kikwete nani aliyezungukwa na walinzi wengi ukajibu,

Mkuu sijui lini umeanza kufuatilia walinzi wa rais, heck for all I know unaweza kuwa mmoja wao lakini naweza kukuambia kuanzia 2005 mpaka leo kumekuwa na tofauti kubwa sana na improvement nyingi tuwape credits. Kwa Tanzania threat level ya usalama wa maisha ya rais iko chini sana.

Nakubaliana nawe, ila ukiangalia utaratibu wa kumlinda rais si salama sana kutokana na uwingi wa watu wanafuatana naye, na pamoja na kwamba wanafahamiana, lakini kwa usalama wingi ule ni kasoro ambayo wenzetu wamejaribu kurekebisha. Mauaji ya marais wa Marekani kwa mfano Kennedy yalitokea katika mfumo wa wingi huo. Karume wa Zanzibar halikadhalika. Pope John Paull alipopigwa risasi ni katika wingi kama huo.

_44865683_-6.jpg

Kuwepo distance fulani kutoka alipo Rais na wasaidizi wake hasa wanapotembea ni muhimu kwa sababu ni rahisi kuona kitu kutoka mbali kabla ya madhara kutokea. Lakini katika wingi ule unatia kiwingu na uwezekano wa mtu mwenye dhamira mbaya kujitokeza papo kwa papo huwa ni vigumu kuthibiti kwa kuwa anayekusudia kufanya hivyo huwa amejianda vyakutosha kutimiza dhamira yake.

Usindikizaji wa Rais Tanzania nao unatakiwa uangaliwe upya, maana utakuta Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri kadhaa, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Makatibu wakuu, wakurugenzi, wote hao wanaenda kumpokea au kuandamana na rais, na hapo bado kuna hao wenye magwanda ya polisi magereza, polisi na usalama wa taifa, na bado umoja wa wanawake bila kuwasahau wa kumpigia vigelegele. Ni maandamano yasiyo ya lazima kiuchumi, na ni hatari kwa usalama pia. Tujaribu kupunguza wingi huu unaoongeza kiwingu katika msafara wa rais.
 
Back
Top Bottom