Ulinzi wa Kikwete Balaa! Ma DC wote wavuliwa viatu Bukoba Airport

ukiona ulinzi wa raisi unaongezeka kuliko ilivyokuwa awali, hususan kwa raisi 'popular' kama wa kwetu hiyo ni dalili yake na wasaidizi wake kutambua kuwa mtu huyo sio popular tena na maadui wamezidi kuliko wampendao. ndio kisa cha JK kuongezewa ulinzi maradufu
 
Nijuavyo mimi, na kwa mujibu wa miongozo ya Usalama viwanjani hakuna mtu mwenye excuse katika kukaguliwa Airport, ispokuwa Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar na Waziri Mkuu!

PJ, hawa ma DC walikuwa wanaenda kumpokea airport, hawakuwa wanasafiri.

Ina maana akiwakaribisha ikulu ndugo kwa chakula cha jioni nako watavuliwa viatu na kukaguliwa, kama hata MADC hawaaminiki nani ataaminika?
 
Kama kafikia hatua hiyo kweli atathubutu kupita mikoani
kwa mikutano ya kushukuru kwa kuchakachuliwa.....?????
 
Ni kawaida sana kuvuliwa viatu kwa ukaguzi, Kuepuka bughudha vaa raba simple na suruali isiyohitaji mkanda.
 
Jamani kuvuliwa viatu Airport ni jambo la kawaida tena linafanyika siku zote.

Hakuna ubaguzi wa cheo pale wote wanapaswa kuvua viatu ili vipitishwa kwenye x-ray kama ilivyo kwa mikoba, makoti nk.

Hapa mimi sielewi!!!!!!! wanaovua viatu ni wasafiri na siyo wapokeaji wa wasafiri si ndiyo? Wapokeaji hawavuki x-ray, wanasubiria abiria watoke nje?????!!!!!!!
 
Ukiwa na rais anayeamini zaidi nguvu za giza,mambo haya ni kawaida katika ziara zake.Wakazi wa Bukoba walimkataa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.Alizidiwa kwa mbali na Dk wa ukweli.
 
Back
Top Bottom