Ulinzi na kamatakamata UDSM leo

Askari mmoja ana gharimu kiasi gani kwa kazi maalumu? Posho yake na gharama za mabomu ya machozi

Gharama za utawala ni kiasi gani,ikiwemo vikao vya kupanga jinsi ya askari hao kugawanyika na kufanya kazi yao?

Watu wa usalama nao hulipwa bei gani kwa ajili ya kukaa vijiweni kunywa pombe kwa siku kwa lengo la kupeleleza?

Tukipiga mahesabu hayo tunaweza kujua ni askari wangapi wanahitajika ili kutumia milioni 100 na tunaweza kukadiria pana askari wangapi huko hivi sasa na hatimaye tutapata jibu kama habari hii ni ya kweli au imeongezewa chumvi

Kule kwetu Zanzibar waliwahi kumwagwa kwa maelfu, nadhani walitumia vijisenti vingi


Asha

Bi Asha posho za vikao ni nyingi hasa kwa wahadhiri. Katika kikao chochote kilicho chini ya Halmashauri ya Chuo (University Council) posho kwa wajumbe ni sh 150,000/= kila mmoja. Vikao vya Kamati ni kuanzia sh 60,000/= sijui kama zimebadilika hizi ni rate za mwaka 2000.
 
kwa weli wenye kufikiri kuwa kuna ushabiki wafuatilie watagundua kuwa ''operation mlimani'' imetengewa shilingi ngapi na tutafurahi kama wataleta takwimu tofauti. Gharama hizo ni pamoja na magari ya kukodisha ambayo yako kama sita na huipiwa laki tano kwa siku. Mimi nimefuatilia nikashangaa na kutoamini sasa badala ya kusema kuwa ni ushabiki tu tuleteeni taarifa tofauti.
 
kwa weli wenye kufikiri kuwa kuna ushabiki wafuatilie watagundua kuwa ''operation mlimani'' imetengewa shilingi ngapi na tutafurahi kama wataleta takwimu tofauti. Gharama hizo ni pamoja na magari ya kukodisha ambayo yako kama sita na huipiwa laki tano kwa siku. Mimi nimefuatilia nikashangaa na kutoamini sasa badala ya kusema kuwa ni ushabiki tu tuleteeni taarifa tofauti.

Habari zipi tena mkuu wakati wewe ndo umefuatilia na umeleta habari hapa JF?
 
Inanikumbusha public school za nchi moja carribean, bila polisi mwalimu hafundishi darasani. maana mitoto imekuwa kama minyangáu, ina siraha zote. pamoja na ulinzi wa getini kuwapekuwa lakini bado inakuwa na silaha na yanauana tu hata yakinyimana popcorn. huenda mkuu mmoja alitembea haka ka nchi ndo maana ameamua aige hii staili hapo chuoni. Lakini mi naona kama unatumia bunduki kuua inzi!!! nyie mnaonaje??
 
Inanikumbusha public school za nchi moja carribean, bila polisi mwalimu hafundishi darasani. maana mitoto imekuwa kama minyangáu, ina siraha zote. pamoja na ulinzi wa getini kuwapekuwa lakini bado inakuwa na silaha na yanauana tu hata yakinyimana popcorn. huenda mkuu mmoja alitembea haka ka nchi ndo maana ameamua aige hii staili hapo chuoni. Lakini mi naona kama unatumia bunduki kuua inzi!!! nyie mnaonaje??

Mkuu CMM nimekupata
Kuna moja iko UK watoto wadogo (teens) wamewekewa kituo cha polisi. Unaambiwa vurumai yao, hakuna wa kuwaamua zaidi ya polisi. Ila ndio hivyo ina wa Jamaica wengi na inawezekana ni njia ya kuwadhibiti kimtindo
 
Siamini 100M inaweza kutumika kwa ajili hiyo lakini siwezi sema, mimi si kiongozi wala policy maker; Ila sipendelei Tanzania kuwa maarufu kwa Haya Ya kutumia excessive force sehemu isiyostahili... watoto wa shule wafikiriwe kama wanetu na si majambaziKuna siku viongozi
Sarafu ina pande mbili. Angalia na upande wa pili pia. hao watu wa shule nao waache kujifanya kama wanasiasa au wadau wa wanasiasa. Upo hapo?
 
Hao FFU na bunduki zao wanalinda nini hasa ?
Kuna mgodi wa MADINI hapo UDSM?
Anayeleta fujo ni binaadamu. siyo mgofi wa madini. Hapo Uni. kuna vichwa-ngumu wanaotaka kuchafua aman, kwa nini wasishughulikiwe? tukanusuru hali ya utulivu waliyonayo mamilioni ya Watanzania wakiwemo watoto wetu wadogo.
 
Wanachuo watano Mlimani mbaroni
Waandishi Wetu
Daily News; Monday,January 19, 2009 @20:00​


UDSM%20POLISI.jpg

ONE of the students of the University of Dar es Salaam being questioned by police before registration for the re-admission exercise which began in the city yesterday. (Photo by Bernard Rwebangira)​

MCHAKATO wa kuwarejesha chuoni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, umeanza rasmi chini ya ulinzi mkali huku wanafunzi watano wakishikiliwa na Polisi, wakidaiwa kutaka kusababisha uchochezi.

Gazeti hili lilishuhudia jana zaidi ya wanafunzi 200 wakiwa wamejipanga kwenye mstari wa usajili ambako walitakiwa kuhakiki majina yao na kupewa fomu za udahili upya na vitambulisho vipya.

Hata hivyo, hali ya usalama katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, haikuwa shwari asubuhi kutokana na baadhi ya wanafunzi wanaoaminika kutokamilisha masharti ya kurudi chuoni, kuonekana wakiwa wamebeba mabango huku wakiimba.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, polisi waliwakamata wanafunzi wanne waliobeba mabango hayo yenye maneno yanayoweza kuleta uchochezi kwa wanafunzi wengine.

"Tumewakamata wanafunzi wanne na wapo kituo cha Polisi Oysterbay, kwa kuwa walibeba mabango tunayodhani yana ujumbe ambao ungeleta uchochezi na ushawishi kwa wenzao waweze kuandamana na kusababisha fujo," alisema Kalunguyeye.

Wanafunzi waliokamatwa ni Issa Paul, Sabinius Respicius, Bahati Alone na Titus Ndulla, wote wa mwaka wa tatu na mwanafunzi wa tano ambaye hakufahamika alikamatwa akidaiwa kutumia lugha chafu katika eneo la chuo.

Baada ya kukamatwa kwa wanafunzi hao, gazeti hili lilishuhudia ulinzi ukiimarishwa eneo hilo kwa magari ya Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), moja likiwa na namba PT 0158 yakiwa na askari wenye silaha na karandinga namba STH 2568 likiegeshwa katika eneo la usajili.

Awali akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema utaratibu wa usajili unakwenda vizuri kwa kuwa wanafunzi wengi wamejitokeza pamoja na ulinzi na usalama kuimarika.

Aliwasihi wanafunzi walioshindwa kutimiza masharti kukata rufaa kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ili rufaa zao zifanyiwe tathmini upya na ikithibitika hawana uwezo watarudishwa vyuoni.

Aidha, alisisitiza kuwa wanafunzi ambao wamejaza fomu lakini hawakutimiza masharti, wakamilishe masharti hayo, kwa kuwa chuo hicho kimeongeza muda wa udahili hadi Januari 29 mwaka huu.

Gazeti hili liliona moja ya fomu za masharti mapya kwa wanafunzi waliotimiza masharti ya kurudi chuoni ambapo wanatakiwa wawapo chuoni wasiingize mwanafunzi yeyote ambaye hajaruhusiwa kuingia hapo pia hakuna kufanya mkutano wowote katika eneo la chuo bila kibali.Masharti mengine ni kutogoma kuingia darasani wala kufanya maandamano yoyote katika eneo la chuo.

Baadhi ya wanafunzi waliotimiza masharti walipongeza mchakato huo wa kuwarudisha vyuoni ila waliiomba Serikali kuwafikiria zaidi wale wanafunzi ambao hawana uwezo na kuwarejesha ili waendelee na masomo.

Leyla Omary ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu alisema pamoja na kwamba masharti yaliyomo kwenye fomu za kudahiliwa upya ni magumu, wanafunzi wengine hawana budi kujitahidi kuyatimiza ili kuokoa muda wa masomo uliopotea.

HabariLeo ilishuhudia katika eneo la Utawala, wanafunzi wote waliotimiza masharti na kuruhusiwa kuingia chuoni hapo pamoja na wafanyakazi wakiwa wamevaa vitambulisho vipya.

Nao viongozi waliovuliwa madaraka wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho cha Mlimani (DARUSO), walitoa wiki moja kwa Serikali iwarudishe wanafunzi wote waliosimamishwa masomo vyuoni, la sivyo wataandamana na kufanya kitu ambacho kitawashangaza Watanzania.

‘Rais wa DARUSO', Anthony Machibya, alisema kinachoendelea kwa sasa ni kuwarejesha watoto wa matajiri vyuoni na kuwatekeleza watoto wa masikini, hali ambayo Serikali hiyo haitakubaliana nayo kwani pamoja na kuvuliwa madaraka, wataendelea kutetea haki za wanafunzi wanyonge waliowaweka madarakani.

"Hatuogopi vitisho, tuko tayari kufa, kufukuzwa chuo na hata kwenda jela, tutaendelea kutetea watoto wa masikini, kwani kinachoendelea sasa ni kutengenezwa kwa matabaka kati ya masikini na matajiri, tunaomba Serikali iwarudishe wanafunzi wote vyuoni, vinginevyo Tanzania haitakalika," alisema Machibya.

Naye Katibu wa Umoja wa Vyuo vya Elimu ya Juu vya Umma Tanzania (UVEJUTA), Silinda David, aliwataka wanafunzi wote kurejea vyuoni pindi vyuo vitakapofunguliwa. "Na kwa taarifa tulizonazo wahadhiri nao wamegoma kuwafundisha wachache waliopo vyuoni hadi tutakaporejea."

Aidha, gazeti hili lilitembelea Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) ambako lilishuhudia wanafunzi wakidahiliwa upya wakiwa chini ya ulinzi mkali lakini hali ikiwa shwari. Nacho, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliitaka Serikali kuacha hujuma dhidi ya wanavyuo masikini.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama hicho, Erasto Tumbo, alisema anashangaa kuona Rais akikaa kimya bila kutoa tamko kuhusu wanafunzi masikini wanaoshindwa kurudi vyuoni kwa kukosa kutimiza masharti yakiwamo ya ulipaji wa gharama zote za mwisho.
 
Date::1/19/2009
Chuo Kikuu vurugu tupu
Hussein Issa
Mwananchi​

JESHI la Polisi jana lililazimika kuvunja maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyokuwa yameandaliwa na serikali ya wanafunzi iliyoripotiwa kuvunjwa, lakini zoezi la udahili likafanyika huku likisababisha adha kubwa kwa wasafiri na wakazi wa maeneo yanayopakana na chuo hicho.

Wanafunzi walitakiwa kufanyiwa udahili kwenye lango la chuo linalotazamana na Chuo cha Maji cha Rwegalulila, lakini nje ya lango hilo ndiko baadhi ya wanafunzi waliona sehemu nzuri ya kuanzia maandamano yao.

Wanafunzi hao waliamua kuandaa maandamano kupinga utaratibu wa udahili ulioanza jana wa kuwapokea wanafunzi ambao wamekamilisha malipo yao yote kulingana na makundi waliyopangiwa na Bodi ya Mikopo.

Mwananchi ilishuhudia wanafunzi wakiwa nje ya uzio wa chuo wakijiandaa kuandamana wakiwa wameshika mabango yanayochochea maandamano, huku wengine wakiwa wanaendelea na udahili.

"Tumeamua kuandamana leo (jana), ili uongozi uone kwamba unachokifanya si halali kwa sababu kumrudisha mwanafunzi mwenye uwezo kuendelea na masomo na kumwacha asiye na uwezo ni sawa na ukandamizaji," alisema mmoja wa wanafunzi waliokuwa wamebeba mabango ya vitambaa kabla ya kuanza maandamano yao.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi lilivunja maandamano hayo na kuwakamata wanafunzi wanne, ambao ilisemekana kwamba walikuwa wakiongoza maandamano hayo.

Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma waliamua kugoma kuingia darasani mwishoni mwa mwaka jana wakipinga sera ya uchangiaji elimu. Wanadai kuwa mfumo unaotumiwa kuchambua uwezo wa kiuchumi wa mwanafunzi na familia yake (means testing), unawabagua na hivyo kutaka sera hiyo isitishwe ama wanafunzi wote wapewe mkopo kamili ili wamudu kusoma bila ya matatizo.

Migomo hiyo iliisha kwa serikali kufunga vyuo vikuu saba. Vyuo hivyo ni UDSM, Chuo Kikuu cha Elimu (Duce), Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Kilimo, Morogoro (SUA), Chuo cha Ualimu Mkwawa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara, Moshi (Mucobs).

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo hilo, kamanda mkuu wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Mark Karunguyeye, alisema polisi ililazimika kuvunja maandamano ya wanafunzi hao kutokana na kwenda kinyume na sheria.

Alisema Jeshi la Polisi limewakamata wanafunzi wanne ambao walikuwa vinara wa maandamo hayo jana; na kuwataja majina kuwa ni pamoja na Bahati Arone, Issa Paul, Titus Ndula na Sabinian Priuspius.

''Nyie mtakaa polisi mpaka wazazi wenu waje kuwachukua... leo mnaenda moja kwa moja Kituo cha Oysterbay. Hakuna mzaha hapa," alisema Karunguyeye.

Mara baada ya kuzuiwa kufanya maandamano chuoni hapo, uongozi wa Daruso ulienda katika baa moja iliyo jirani na mlango wa kuingilia chuoni hapo na kuzungumza na waandishi wa habari. Viongozi hao walisema kuwa, pamoja na kuzuiwa kwa maandamano hayo, wanapanga mikakati mingine ya maandamano yatakayofanyika muda wowote kuanzia leo.

"Wametuzuia leo, lakini aluta continua, tunapanga mipango ya kuandamana vyuo vyote vya umma kwa mara nyingine tena. Kama wanataka watumalize kwa kutuua, sisi hatuogopi kwani tunatetea haki za wanyonge," alisema rais wa Daruso, Antony Machibya.

Naye katibu wa mtandao wa wanafunzi nchini, TSNP, Owawa Steven alisema wakishapangilia namna ya kuandamana nchini kote, watawafahamisha wanafunzi wote ili wajumuike katika kudai haki zao.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala alisema hali inaendelea vizuri ya kudahili wanafunzi na akasisitiza kuwa muda wa kudahili unaongezwa. Awali, ilitangazwa kuwa udahili ungefanyika hadi Januari 22, lakini sasa utaisha Januari 29. Pia alipotakiwa kuelezea wanafunzi waliokamatwa alisema, hana taarifa ya kukamatwa kwao.

"Imebidi muda uongezeke kwani idadi ya wanafunzi ni kubwa na kuna wale watakaokata rufaa, pia mlango wa waziri uko wazi kwa wale wasio na uwezo wa kukamilisha malipo yote," alisema.

Masharti waliyowekewa wanafunzi ya kuingia chuoni hapo hayakuwa kero kwao tu, bali wakazi wa maeneo jirani kama Changanyikeni na Makongo na wanajamii wa chuo hicho ambao walilazimika kutumia vitambulisho maalum kuweza kuingia ndani ya uzio.

Hakuna mabasi ya usafiri (daladala) yaliyoruhusiwa kuingia eneo la chuo kama ilivyo kawaida yao ya kubeba abiria kutoka Mwenge kwenda Ubungo kupitia Chuo Kikuu na mengine kuelekea Changanyikeni.

Hata wamiliki wa magari madogo walilazimika kusimama langoni kukaguliwa na kuonyesha vitambulisho kabla ya kuingia.

Mwananchi ilishuhudia wanafunzi wakilalamikia fomu za kujiunga upya na chuo hicho na kudai kwamba wanatakiwa kulipia gharama ambazo zilikuwa zinalipwa na bodi ya mikopo, miongoni mwa gharama hizo ni pamoja na hela ya mitihani, matibabu na udahili.

"Tunalipia fedha za mitihani Sh12,000, kulipia matibabu Sh50,000 na udahili tunalipia Sh5,000, hela ambazo huwa zinalipwa kupitia bodi," alisema mwanafunzi Mary Lucas.

Nao Ellen Manyangu na Winfrida Mtoi wanaripoti kuwa, baadhi ya wahadhiri wa Udsm wamelaani kitendo cha uongozi wa chuo kufunga baadhi ya njia na kusema kitendo hicho ni kutengeneza bomu ambalo hawajui litalipukia upande gani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti kwa sharti la kutotajwa majina, wahadhiri hao walisema kitendo hicho kimewafanya wajione kama wakazi wa Ukanda wa Gaza, eneo la Mashariki ya Kati ambalo limetenganishwa na Israel kwa ukuta na ambalo haliishi kuwa na mapambano.

Walisema wanashangazwa na uongozi wa chuo kufanya maamuzi bila ya kuwashirikisha wakiwa ni wafanyakazi wa sehemu hiyo muhimu kielimu.

"Nashangazwa na uongozi huu kwani mambo mengi yahusuyo chuo tumekuwa tukiyasikia mtaani na baadaye kuyasoma katika vyombo vya habari... na kweli baada ya taarifa hizo zisizo rasmi tunauona ukweli wa taarifa hizo," alisema mmoja wa wahadhiri hao.

Aliongeza kuwa, kipo chama cha wahadhiri cha Udasa, lakini mara nyingi maoni ya chama hicho hayapewi uzito wowote na uongozi wa Chuo na badala yake huchukuliwa kama ushauri ambao unaweza kutumika au kutotumika.

Aidha, kwa upande mwingine wahadhiri hao walisema wanashangazwa na kauli ya uongozi huo wa Chuo kuwataka kuanza kufundisha mara tu wanafunzi watakapofungua chuo licha ya wanafunzi wengi kutoripoti kwa siku hiyo.

"Mimi nina darasa la wanafunzi 200 na walioruhusiwa ni 45 kati ya hao walioripoti kwa siku ya leo ni watano unategemea niwafundishe hao kisha nifanyeje juu wengine watakaoripoti baada ya hapo? Huku ni kuwekana katika wakati mgumu," alisema mhadhiri huyo.


Wakati huo huo, wakazi wa Changanyikeni wamelaani kitendo cha kufungiwa njia na kusema kuwa, huo ni ukiukwaji wa haki za binadamu, kwa kuwa njia hiyo ndiyo njia kuu waliyokuwa wakitumia hata kabla ya chuo hicho kuwepo.

Wakitoa maoni yao kuhusiana na suala hilo, wakazi hao walisema kitendo cha mtu au uongozi fulani kuamua kufunga njia kwa sababu ya matatizo waliyoyatengeneza bila kujali njia hiyo inayotegemewa na jamii kwa mahitaji mbalimbali ni unyanyasaji wa hali ya juu.

"Ni kitendo cha kusikitisha watu wasomi kama hao kuchukua maamuzi bila kuangalia madhara ya pande zote, hii njia ndiyo njia kuu kwetu kwani huduma za afya, maji, benki na kituo cha polisi, vyote viko hapo chuoni na ndivyo vinatoa huduma kwa wakazi wa Changanyikeni," alisema mkazi wa Changanyikeni, Agnes Moshi.

Aliongeza kuwa, "niko hapa tangu saa 2 asubuhi nimezuiwa kupita na kama uonavyo hali yangu dakika yoyote naweza kujifungua, unategemea nikizidiwa hapa na kupata matatizo yoyote nani atalaumiwa kama sio uongozi huo mbovu wa chuo?"


Aidha, alieleza kuwa jana (juzi) wanakijiji waliandaa maandamano kupinga suala hilo la kufungiwa njia, lakini uongozi wa wilaya ulisitisha maandamano hayo na kuahidi kutoa suluhu ya tatizo hilo jana.
 
Du! pamekuwa kama gaza strip kama attachment hapo chini inavyoonyesha.
Inasikitisha kwa kweli.
 

Attachments

  • UDSM LEO.doc
    621 KB · Views: 123
Ujinga mtupu.

Uongozi wa chuo ni wa kijinga (viongozi wa aina ya Profesa Geoffrey Mmari ni adimu sana). Ndiyo maana ninaposikia watu wanasema kuwa tumchague kiongozi fulani ati kwa vile yeye ni msomi mimi huguna sana. Mtu anatakaiwa awe na sifa ya uongozi, halafu usomi utamsaidia kuongoza viziri. Usomi pekee haumfanyi mtu awe kiongozi mzuri, ndiyo maana wasomi wale akina Mukandala wanashindwa kuongoza.

Uongozi wa serikali ni wa kijinga. Gharama wanazotumia kudahiri wanafunzi upya, kudeploy polisi na kuwalipa walimu na wafanya kazi wa chuo wakati hakuna wanafunzi chuoni zingetosha kuwalipia wanafunzi hao karo na kuepusha mazigira ya unyanyasaji kama haya.
 
Ujinga mtupu.

Uongozi wa chuo ni wa kijinga (viongozi wa aina ya Profesa Geoffrey Mmari ni adimu sana). Ndiyo maana ninaposikia watu wanasema kuwa tumchague kiongozi fulani ati kwa vile yeye ni masomi mimi huguna sana. Mtu anatakaiwa awe na sifa ya uongozi, halafu usomi utamasaidia kuongoza viziri. Usomi pekee haumfanyi mtu awe kiongozi mzuri, ndiyo maana wasomi wale akina Mkandala wanashindwa kuongoza.

Uongozi wa serikali ni wa kijinga. Gharama wanazotumia kudahiri wanafunzi upya, kudeploy polisi na kuwalipa walimu na wafanya kazi wa chuo wakati hakuna wanafunzi chuoni zingetosha kuwalipia wanafunzi hao karo na kuepusha mazigira ya unyanyasaji kama haya.
w

Hao tuliowaweka madarakani siku zote huwa tayari kutumia vyombo vya dola ili kulinda maslahi yao badala ya yale ya nchi. Wangeweza kabisa kutatua matatizo ya vijana hawa na kuwapa mikopo ya 100% ili kuwawezesha kumaliza masomo yao bila matatizo. Hawa viongozi maamuzi yao siku zote ni ya kutaka kukomoa badala ya kujenga ili kuhakikisha matatizo hayo yasijirudie tena.

Hili tatizo la mikopo kuhusiana na wanafunzi wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo wa kifedha itaendelea kuwepo miaka nenda miaka rudi maana 20% wanayotakiwa wajilipie wenyewe kwa wengine hawawezi kabisa kumudu kiwango hicho.

Hivyo UDSM na vyuo vingine na vitafungwa kila mwaka na kupoteza miezi chungu nzima na hata miaka kutokana na viongozi wa serikali kutokuwa tayari kutatua matatizo yaliyopo kwa njia za kudumu.

Mungu inusuru nchi yetu.
 
...upuuzi mtupu,kuanzia wanafunzi waliogoma mpaka UD administration wote hawana akili na kama hivi ndio namna ya kumaliza matatizo basi solution hakuna na kitakachofuata ni makonde zaidi,wengine watafukuzwa chuo for good na chuo kufungwa tena,hivi kwanini wanachuo wanagomea uongozi wa chuo wakati tatizo hapa ni kati yao na sponsor wao,chuo kinawajibika kufundisha wanafunzi waliolipa fees zao na wengine wengi tuu ni private na have nothing to do na pesa za serikali,wako pale kusoma na wamelipa pesa zao sasa kwanini hawa wanaleta fujo campus badala ya kwenda kupambana na sponsor wao ambaye sio UD admin,na Chuo kikubwa kama UD kwanini wanashindwa kutumia technology to solve this BS,mtoni semister likianza hakuna kuongea na mtu,unakutana na limachine/computer tuu katika registration na kama unadaiwa chochote computer linagoma mpaka ulipe,sasa kama una nguvu pigana nalo uone cha moto...kweli nimechok na hii migomo ya kugomea uongozi wa chuo ambao ukweli hawahusiki kabisa na hiyo mikopo,waende huko Bodi/serikalini sio chuoni ambako watu kibao karibu 50% wanajilipia pesa zao siku hizi.
 
Ujinga mtupu.

Uongozi wa chuo ni wa kijinga (viongozi wa aina ya Profesa Geoffrey Mmari ni adimu sana). Ndiyo maana ninaposikia watu wanasema kuwa tumchague kiongozi fulani ati kwa vile yeye ni masomi mimi huguna sana. Mtu anatakaiwa awe na sifa ya uongozi, halafu usomi utamasaidia kuongoza viziri. Usomi pekee haumfanyi mtu awe kiongozi mzuri, ndiyo maana wasomi wale akina Mkandala wanashindwa kuongoza.

Uongozi wa serikali ni wa kijinga. Gharama wanazotumia kudahiri wanafunzi upya, kudeploy polisi na kuwalipa walimu na wafanya kazi wa chuo wakati hakuna wanafunzi chuoni zingetosha kuwalipia wanafunzi hao karo na kuepusha mazigira ya unyanyasaji kama haya.
w

...uongozi wa chuo sio bodi ya mikopo/serikali na wala hawana maamuzi yeyote na hiyo mikopo,sioni sababu ya kulaumu uongozi wa chuo kwa hii migomo,kwanini wafundishe wanafunzi wasiolipa ada? nawalaumu tuu kwa kuendekeza maneno na matumizi makubwa ya kutumia security wakati wana uwezo wa kukaa kimya na technology ikafanya kazi yote with accuracy kwa gharama ndogo sana
 
...hii serikali ndio ya kulaumu na kwa nini wanajua watu maskini kiasi kile na ukweli hawana any source of credit bado unalazimisha wachangie? watazipata wapi? kama kweli serikali wako sincere na hawana pesa bora kuchukua wanafunzi wachache na wawalipie 100% kuliko kuwafikisha chuoni then unawafukuza kwa sababu wameshindwa kuchangia,wanatia huruma sana hao vijana,i know it practically/from experience watanzania wengi sana ni maskini mpaka huwezi amini...nakumbuka kuna wanafunzi wana akili sana wakija kuanza form one basi kurudi likizo kao ni baada ya miaka miwili au kumaliza form four,walikuwa wanabaki shule wakati wa likizo kuchunga ng'ombe na kulima then shule inawasamehe school fees,then leo unawaambia wachangie,wazitoe wapi? lakini tusisahau kuna wengi vile vile wana uwezo wa kuchangia!
 
Kuna mchango niliweka leo kwenye mada ya "Chuo Kikuu Vurugu Tupu" kabla haijaunganishwa na hii. Nilicheki kuwa ilikuwepo, maana niliisoma. Lakini naona sasa imefutwa.

Moderator, umeifuta makusudi au ni bahati mbaya? Tafadhali irudishe.

Augustine Moshi
 
Anayeleta fujo ni binaadamu. siyo mgofi wa madini. Hapo Uni. kuna vichwa-ngumu wanaotaka kuchafua aman, kwa nini wasishughulikiwe? tukanusuru hali ya utulivu waliyonayo mamilioni ya Watanzania wakiwemo watoto wetu wadogo.

Nadhani ni vema wachangiaji wa-balance michango yao kwa kuongelea hali ya wale ambao wanahitaji kuwa madarasani hawapendi vurugu, watiifu na wanapenda kutatua matatizo yaliyokuwepo kwa njia ya majadiliano zaidi.
Ni vema eneo la chuo likaachwa liendelee kutoa huduma ambazo zimekusudiwa yaani kutoa elimu. Kwa wale ambao bado wanaona kuwa wanahitaji kutatua matatizo ya kwa njia vurugu nk basi waendelee kufanya hivyo lakini siyo ndani ya eneo la chuo.
nafikiri hapa tutakuwa tumetenda haki kwa maana wanaotaka kutatua kwa njia ya majadiliano huku masomo yakiendelea watapata nafasi na wale wanaotaka kwa njia ya vurugu nao watakuwa wanaendelea kufanya hivyo pia.
 
Waliokamatwa ni Issah Paul, Titus Ndullah, Sabinian Prinspius na Bahati Alone. Kamanda wa Kinodnoni, Kalunguyeye (nadhani ndio jina lake) amesema watafikishwa mahakamani kwa uchochezi

kwenye zile vurugu za mwaka jana, wanafunzi walipelekwa mahakamani na wakaonekana walipelekwa kimakosa. ikabidi warudishwe ili wahukumie kwa by laws za chuo. sijui safari hii.
Management inakurupuka sana wakati wa migomo (hawa jamaa huwa wanakuwa na hasira sana mpaka wanaharibu). hebu fikiria barua ya DVC-ARC kuhusu kudailiwa kwa wanafunzi ilitangaza kufutwa kwa DARUSO lakini VC akaandika barua nyingine kuipinga ile ya kwanza kwamba DARUSO haijafutwa ila viongozi ndiyo hawana chao. inaonyesha kuna weakness kubwa kwenye maamuzi. pia chuo kina PRO (msemaji wa chuo) ambaye huwa hana kazi, kwani hii mizee inapenda kila wakati kuzungumza kwenye press, why kwanini wizi mtupu.
 
Kuna mchango niliweka leo kwenye mada ya "Chuo Kikuu Vurugu Tupu" kabla haijaunganishwa na hii. Nilicheki kuwa ilikuwepo, maana niliisoma. Lakini naona sasa imefutwa.

Moderator, umeifuta makusudi au ni bahati mbaya? Tafadhali irudishe.

Augustine Moshi

Augustine hata yangu imefutwa/potea tena nilikuwa nime ku quote wewe!!! what a coincidence?
 
Back
Top Bottom