Ulinzi mkali kama wa rais kwa faru hautoshi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
LEO katika gazeti hili tumechapisha habari inayomkariri Rais Jakaya Kikwete akipokea faru watano weusi kutoka Afrika Kusini akikiri kuwa ujangili na imani za wanaume wajinga kuwa unga wa pembe za ndovu huongeza nguvu za kiume ni chanzo cha kutoweka wanyama hao hapa nchini.

Faru hao watano kati ya 32 kutoka Afrika Kusini waliotolewa msaada na Kampuni ya Singita Grumeti Reserve kupitia mmiliki wake Paulo Tuddor Jones raia wa Marekani.

Rais Kikwete kutokana na ujangili faru hao watapewa ulinzi unaofanana na ule ambao anapewa yeye kama rais wa nchi ili kuhakikisha hakuna mtu ambaye anagusa wanyama hao.

Alisema miaka ya 1960 wanyama hao walikuwa wanafikia 1,000 na serikali ilitoa kibali cha kuwinda na kuuza, lakini ujangili uliibuka na kuwapunguza hadi kufikia miaka ya 1990 idadi yao ilikuwa chini ya mia moja.

Rais alisema majangili walitumia mwanya huo huku imani za watu wajinga wakiamini kuwa unga wa pembe hizo unaongeza nguvu za kiume, hali ambayo serikali imejipanga kukabiliana nayo ili kuhakikisha faru hao wanaongezeka.

Tunachukua nafasi hii kuipogeza serikali kwa kufanya jitihada za kuomba msaada wa faru hao kutoka Afrika Kusini ili Tanzania iwezekuwa na faru hao tena.

Hata hivyo, tunapenda kueleza kwamba uamuzi wa kuomba msaada wa faru kutoka Afrika Kusini wakati miaka ya nyuma Tanzania ilikuwa moja ya nchi ambazo zilikuwa na idadi kubwa ya wanyama ulikuwa nao ni ya aibu.

Tunasema ni jambo la aibu kwa serikali kwa sababu hatuna sababu za msingi zilizotufanya tushindwe kuwalida wanyama hao hadi wakaisha na matokeo yake leo tunageuka ombaomba.

Ni kutokana na uzembe huo wa kushindwa kulinda raslimali zetu ikiwamo faru leo kila mara tunasikia makontena ya pembe za ndovu kutoka Tanzania yanakamatwa nje ya nchi. Lakini tunajiuliza ni akina nani wanaohusika na vitendo hivi vya ujangili kiasi kwamba waue tembo wasafirishe katika makontena kupitia barabara na bandarini zetu bila ya kuonekana?

Ni wazi kwamba ni watu waliopo karibu na baadhi ya viongozi wa juu wa serikali au ambao wanatumia fedha kuwafumba macho watendaji wa serikali ambao wamepewa jukumu la kulinda rasmali zetu.

Kutokana na hali hiyo tunachukua nafisi hii kuitahadharisha serikali kwamba pamoja na kuwapa ulinzi mkali kama wa rais faru, lakini kama haitadhibiti watendaji wake kujihusisha na biashara hii haramu ni wazi hakuna jambo ambalo litatendeka.

Kama serikali inataka kulinda wanyamapori wake ambao wako katika hatari ya kutoweka, basi ni vyema ianze kuwakamata watu ambao wanajihusisha biashara hii ambao wengi wanatumia mwavuli wa ukaribu wao na vigogo wa serikali au kujiingiza katika siasa kufanikisha azima yao

Ulinzi mkali kama wa rais kwa faru hautoshi
 
Back
Top Bottom