Elections 2010 Ulinzi kura za rais

NATA

JF-Expert Member
May 10, 2007
4,492
1,311
Kura za udiwani ubunge ni rahisi sana kuzilinda kuliko za urais.

Diwani akisha tangazwa mshindi basi husahau ulinzi wa kura za ubunge. Naye mbunge akisha tangazwa mbunge husahau ulinzi wa kura za rais
hapo ndipo chakachu .........aaaa inapokuwa kubwa .
 
Kura za udiwani ubunge ni rahisi sana kuzilinda kuliko za urais.

Diwani akisha tangazwa mshindi basi husahau ulinzi wa kura za ubunge. Naye mbunge akisha tangazwa mbunge husahau ulinzi wa kura za rais
hapo ndipo chakachu .........aaaa inapokuwa kubwa .

ndio maana tunatakiwa kujiunga na chadema sasa na kukifanya kiwe na wanachama makini kila mtaa ili kuzuia hujuma hizi. baada ya diwani kutangazwa kuwe na mwangalizi mkuu wa chama....na baada ya ubunge kuwe na mwangalizi mkuu wa jimbo kwa ajili ya kura za rais.....
yatawezekana tu next time....mimi najiunga very soon
 
hata hivyo kura toka kila kituo zaweza thibitisha nani kashinda bila kutegemea za Tume CCM.
 
hata hivyo kura toka kila kituo zaweza thibitisha nani kashinda bila kutegemea za tume ccm.
si rahisi hivyo, kwa kutegemea mawakala tu ni pamoja na ulinzi shirikishi wa watu wa diwani na wambunge. Kama wanavyo ng`ang`ania kura za mbunge sisomwe ndivyo wahakikishe kura za rais kira kituo kabkla ya kushangilia ushindi wa diwani na kusambaa!
 
kura za udiwani ubunge ni rahisi sana kuzilinda kuliko za urais.

Diwani akisha tangazwa mshindi basi husahau ulinzi wa kura za ubunge. Naye mbunge akisha tangazwa mbunge husahau ulinzi wa kura za rais
hapo ndipo chakachu .........aaaa inapokuwa kubwa .

kwa kweli ndugu yangu umesema kitu ambacho nimekiona live katika kusimamia kura za chama nilichokuwa nasimamia. Kama mnakumbuka vyema uchaguzi ulipokaribia tulihamasishana humu kuwa wapenda mabadiliko tukashiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi ikwemo kupiga kura, kuwa mawakala, kusimamia maslahi ya vyama vyetu katika uchaguzi n.k mwenzenu mlikuwa hamnioni nilifanya hivyo.

Nilichojifunza kuwa uchaguzi sio lelemama. Unahitaji experience, manpower na resources za kutosha. Kwa kuwa ccm wana mtandao kutoka taifa hadi vijijini wanasaidiana kubeba huo mzigo. Ni lazima tukubali kuwa kura zimeibiwa, lakini yapo maeneo inexperience, uzembe ndivyo vilichangia sana kufanikisha wizi huo. Wengi wetu tulimtegemea dr slaa na chadema wafanye kila kitu. Tulishau ule msemo "what will you do for america"

mgombea ubunge wangu alikwishaibiwa kura zake 2005, safari hii alijipanga kweli kweli, nakuhakikishia kama sio yeye mwenyewe kutengeneza timu ya uhakika kukusanya fomu za matokeo ya ubunge na urais, hata yeye angechakachuliwa tuu!!!!.

Nilichokiona mgombea udiwani wake alishindwa hata kuchukua summary ya kura alizopata kama mgombea udiwani kutoka vituoni,tulipofika makao makuu ya kata alikuwa hajui kura zake ni ngapi ilihali matokeo katika vituo yalikuwa yamebandikwa. Hivyo alikuwa akitegemea kauli ya msimamizi kuwa kapata kura ngapi kama mgombea udiwani. Kama ilishindwa kuwa na summary yake mwenyewe unatarajia ni kwa vipi awe na summary ya mbunge na rais?

Safari hii ccm ,tume na wasimamizi walitumia style ya kuchelewesha matokeo ili kuwatenga wanachadema na kura za dr slaa. Dalili za kuchelewesha matokeo ya udiwani na ubunge zilipojitokeza kila mtu akamsahau mgombea urais; shughuli ikawa ni kupigania na kulinda kura za madiwani na wabunge. Hiyo ikatoa mwanya kwa tume ya uchaguzi kuchakachua matokeo ya urais wanavyotaka.

Hapo ndio ninapokuja kukubaliana na mwanakijiji hofu ya wizi wa kura imetuathiri sana kwanza kwa kufanya wappiga kura wengi wasijitokeze kupiga kura. Pili hofu hiyo ikatumiwa vizuri na ccm ,tume uwt kuwatenga wancahdema na kura za kura za dr slaa. Sikumbuki kusikia katika mkusanyiko wowote wa people's power kudai matokeo ya udiwani au ubunge mtu yoyote akikumbusha kudai pia kura za urais.

Tunaweza kuanzisha fujo, vurugu na hata vita lakini ukweli utabaki pale pale tulichopata ndio saizi yetu kutokana na inexperience,manpower na resources at our disposal.linapokuja suala la uchaguzi wenzetu wanaccm wanakuwa makini na wanakuwa tayari kujitolea zaidi hata kutembea nyumba kwa nyumba usiku kushawishi wapiga kura.

Kwa mimi niliyekuwa front katika kampeni, nikakesha usiku kucha hadi asubuhi siku ya upigaji kura, na matokeo ya udiwani yalipotoka tukashinikiza kutangazwa kwa kura za mgombea ubunge wetu, ambaye alikuwa na data kamili kura zake ni ngapi. Nawaona wale ambao hawakutimiza wajibu wao wa kushiriki mchakato wa uchaguzi huu wa kihistoria kama vile hawana haki ya kulalamika kuibiwa kwa kura zetu.

Nitatoa mfano hai mmoja kuonyesha vile upungufu wa watenda kazi ulivyosababisha chama changu kukosa idadi ya kutosha ya kata kuwa chama tawala katika manispaa husika. Katika kata niliyosimamia, ccm walishinda udiwani kwa kwa kura chache. Kura zilizoipa ccm ushindi zilizopigwa katika vituo vitatu vilivyoko ndani ndani baada ya mawakala wenyeji wa maeneo hayo kurubuniwa.

Baadhi ya mawakala waliotarajiwa kuongeza nguvu huko walikataa kusimamia vituo hovyo kwa madai kuwa ni ndani nsdani sana. Walitaka kupangiwa kituo kilivyopo town. Hali hii ikasababisha mtu mmoja wa ccm kupiga kura tatu na hata nne katika vituo vya vijijini kutokana na mawakala wenyeji wa kurubuniwa.




 
Back
Top Bottom