Ulinganifu wa Usafi Dar na Finland

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Mimi ni Mtanzania, nilifanikiwa kupata safari ya kuja Finland kwa ajili ya masomo ya muda mfupi toka tarehe 01/09/2009 na niatrudi Tanzania mwezi ujao. Nimebahatika kutembelea maeneo mengi ya katika nchi ya Finland kama Turku, Tampere, Helsinki na kadhalika. Pia nilipata bahati ya kutembela Norway and Capenhagen. Jambo lililonifurahisha ni usafi wa nchi hizi. Ni ngumu sana kuona rundo la taka kama ilivyo katika jiji la Dar es Salaam. Mtu anatembea na uchafu masafa marefu mpaka aone sehemu ya kutupa taka.

Mapipa ya kutupia taka yapo kila mahali, hata kwenye misitu. Nikajiuliza ingekuwa ni Dar, wauza vyuma chakavu wangekuwa walishayabeba. Mapipa yenyewe hayajatobolewa kama tunavyofanya Tanzania. Mara ya kwanza nilifikiri ni mapipa ya maji safi, kumbe ni kwa ajili ya taka. Mimi mwenyewe nilikuwa naona aibu kimoyo moyo. Sijui tufanye nini ili jiji la Dar liwe safi. Ukiwa nchi za Ulaya utafikiri hakuna kufa, jinsi watu wanavyojali.
 
kuifanya Finland au Norway kuwa role model ya mji wetu ni kupasuka msamba, twende hata Nairobi tukajifunze ....
Kilichopo ni kuwa sheria zetu ni legelege sana, tunatunga hakuna msimamizi, naweza kukojolea ukuta hapa jirani tu, hakuna hata anae stuka akinikuta, tumezoea, watu wanatupa chupa za maji mbele ya police au mgambo, hakuna anae jali, kafanye hivyo Nairobi.
 
Kwanini kuandikia mate wakati wino upo, tupeleke milonjo yetu Kigali...ila Miafrika ndivyo tulivyo NN
 
tusiende mbali tuende moshi mjini, jaribu kutupa taka hovyo au ukojolee ukuta uone matokeo yake. Tuanze kubadilika na kuweka mazingira yetu katika hali ya usafi, kwanza kabisa jiji liweke mapipa ya taka kila sehemu na taratibu watu watabadilika!
 
tusiende mbali tuende moshi mjini, jaribu kutupa taka hovyo au ukojolee ukuta uone matokeo yake. Tuanze kubadilika na kuweka mazingira yetu katika hali ya usafi, kwanza kabisa jiji liweke mapipa ya taka kila sehemu na taratibu watu watabadilika!
Nadhani hayo mapipa yasiwekwe kabisa, maana yakikosekana watu hupata kisingizio - watatupa popote.

Ukizalisha taka, beba nenda nazo nyumbani. Ukinunua embe, kula na utupe hapo hapo uliponunua. Vivyo hivyo kwa maji ya kunywa au voucher.
Ukinunua chips nyama choma na unasafiri kwa basi, tupa humo ndani ya basi, sio dirishani. Yes, ndani ya basi; hata kama mnapita mbugani.

Kule Moshi mtu akikuona unanunua voucher anakufuata nyuma. Anasuburi aone utatupa wapi akulime!
 
Back
Top Bottom