Ulimwengu wa mapenzi

Kwanini ujipe tabu, kama yeye hakupendi,
Tafuta sahihi jibu, nenda baa kaspendi,
Jipatie kaulabu, kuchangamsha maindi,
Baada ya bia tano, kila kitu kiopo shwari.

Kila kitu kipo shwari, baada ya bia tano,
Akijipitisha Amri, omba nae mkutano,
Mpashe hii habari, wahitaji pumziko,
Kwa Amri yake tabia, lazima ingie kingi.

Akishaingia kingi, siibane nyama yao,
Mwonjeshe mipango mingi, hata ile ya wayao,
Ukishajenga msingi, huzuni yaenda kwao
Ulimwengu wa mapenzi, lazima utarejea!
 
Wasalaamu salamuni, waungwana nawajia
Mababu wa mizimuni, walokwisha tangulia
Najongea kwa huzuni, najizuia kulia
ulimwengu wa mapenzi, buriani aagia

Ulimwengu wa mapenzi, buriani naagia
naondoka kwa majonzi, mlango najifungia
Si wangu nimemaizi, moyo nafungulia
Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka

Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka
Umeyataka mabawa, meupe yaso na taka
Nimechoka kupagawa, na penzi lenye mashaka
Ulimwengu wa mapenzi, nawaachia wenye bahati.

KUTOKA KWA NYOTA NDOGO-NATAFUTA

CHORUS
Natafuta wa kunipenda mimi
nimechoka na penzi la uongo
na sijui kama nitapenda tena
niliyempenda ameniponza
nasubiri pengine Mungu ataleta
atakae nipenda atakae nipenda

Maumivu nimeyapata
sasa naishi na mengi fikira
mazoea yana tabu,umpendae yeye atakuponza
mambo mengi utokea,sikujua yangenifikia
visa vingi utendeka,sikujua kama yangenitokea
fikiria kama umpendae kama akupenda hivyo hivyo

CHORUS

Binadamu hatuna wema
mambo mazuri uwa yakitokea
twageuza,twayapika,twayafanya mabaya yaonekane
penzi langu nilitoa bila choyo wala dukuduku
lakini penzi likageuka,likawa chungu mithili ya shubiri
MIKONO YANGU NINAIFUNGA,NA SIJUI NANI WA KUMNYOOSHEA

Kwa anaeweza kuuweka hapa,tafadhali kwa ajili ya dada yetu.
 
MTM

Uamuzi nimetoa, nachelea urejea
wangu moyo nilitoa, yeye akauchezea
kitambo ningelitoa, subira nikarejea
ningeyajua ya moyo, katu singeliumia

Natizama pembe kona, faraja kuitafuta
Ili nipate kunona, mwili upate mafuta
nimekonda kila kona, kama mche wa ufuta
laiti ningeyajua, katu singeliumia

Kweli nimekuelewa, kipi umenadhiri
hiyari yashinda utumwa, hili sasa ni dhahiri
Ila epuka tumwa, ibilisi ni jahiri
Pia usije fumwa, ukijuta kwa hadhiri
 
Mwana jamii namba moja,Zako salamu nimezipata
Kwa ulizotoa zako hoja ,na mizimuni wamekupata
Nimepitia zote zako hoja,kwa uhakika nimekupata
Swali langu kwako moja,umeacha au wapumzika?

Wahenga walisema,mvumilivu daima hula mbivu
Umevumilia na kumsoma,mwishowe ukala mbovu
Ulimpenda pasi lawama,baadaye kakupa maumivu
Swali langu kwako moja,umeacha au wapumzika?

Kipindi hiki kigumu sana,cha upweke na majonzi
Ulompenda mmeachana,arukaruka sana kama inzi
Tabia yake si ya maana,naona nawe pia umeimaizi
Swali langu kwako moja,umeacha au wapumzika?

Ulimwengu wa mapenzi,hatuuachi twapumzika
Ndani ya mwaka au miezi,utampata unayemtaka
Mojawapo ya wanaokuenzi,Fidel80 aso na mipaka
Swali langu kwako moja,umeacha au wapumzika?

Tulia ewe dada tulia,wa dhati mpenzi utampata
Endelea kuvumilia,wako wa ukweli atakufuata
Hakika nakufagilia,Kwa uamuzi wako usio tata
Swali langu kwako moja,umeacha au wapumzika?
 
Ulimwengu wa mapenzi,hatuuachi twapumzika
Ndani ya mwaka au miezi,utampata unayemtaka
Mojawapo ya wanaokuenzi,Fidel80 aso na mipaka
Swali langu kwako moja,umeacha au wapumzika?

Kudadekiiii.......... wewe wamtakia mema kweli?
 
Wasalaamu salamuni, waungwana nawajia
Mababu wa mizimuni, walokwisha tangulia
Najongea kwa huzuni, najizuia kulia
ulimwengu wa mapenzi, buriani aagia

Ulimwengu wa mapenzi, buriani naagia
naondoka kwa majonzi, mlango najifungia
Si wangu nimemaizi, moyo nafungulia
Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka

Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka
Umeyataka mabawa, meupe yaso na taka
Nimechoka kupagawa, na penzi lenye mashaka
Ulimwengu wa mapenzi, nawaachia wenye bahati.

Shosti unaniangusha, kujiliza hadharani
Chati unampandisha, kakufanya hayawani
Bure unajikondesha, nakujishusha thamani
Amekufanya wa nini, mfanye wa kazi gani.

Mfanye wa kazi gani, amekufanya wa nini
Akipita mtaani, mvalie na miwani
Mmekutana ukubwani, majonzi sasa ya nini
Ulimwengu wa mapenzi, na wewe bado ni memba.

Na wewe bado ni memba, ulimwengu wa mapenzi
Hutakiwi kwenda Pemba, kuyatafuta mapenzi
Wanamuziki waimba, yalianza toka enzi
Aliye na niya hasa, penzi usimbanie.

Penzi usimbanie, aliye na niya hasa
Ila usikimbilie, Fidel Chrispin Masa
Hapana watamkie, usije wapa hamasa
Mbili zero moja mbili, ndoa zao watangaza.

Ndoa zao watangaza, mbili zero moja mbili
Hawajaenda angaza, wameahirisha mara mbili
Hapa nakupa mwangaza, silazimishi ukubali
Ukitala alosoma, jiulize pia why?

Jiulize pia why, ukitaka alosoma
Ningeshauri Bluray, ila kingereza chake noma
Anaongea in a way, tafsiri zinagoma
Pedejee sishauri, unless wahusudu.
 
Wenye bahati tunasonga
wewe safiri songasonga
Sisi raha tunalonga
umevamia kabla hujalonga
Kwaheri tuachie tunatesa.
 
Shosti unaniangusha, kujiliza hadharani
Chati unampandisha, kakufanya hayawani
Bure unajikondesha, nakujishusha thamani
Amekufanya wa nini, mfanye wa kazi gani.

Mfanye wa kazi gani, amekufanya wa nini
Akipita mtaani, mvalie na miwani
Mmekutana ukubwani, majonzi sasa ya nini
Ulimwengu wa mapenzi, na wewe bado ni memba.

Na wewe bado ni memba, ulimwengu wa mapenzi
Hutakiwi kwenda Pemba, kuyatafuta mapenzi
Wanamuziki waimba, yalianza toka enzi
Aliye na niya hasa, penzi usimbanie.

Penzi usimbanie, aliye na niya hasa
Ila usikimbilie, Fidel Chrispin Masa
Hapana watamkie, usije wapa hamasa
Mbili zero moja mbili, ndoa zao watangaza.

Ndoa zao watangaza, mbili zero moja mbili
Hawajaenda angaza, wameahirisha mara mbili
Hapa nakupa mwangaza, silazimishi ukubali
Ukitala alosoma, jiulize pia why?

Jiulize pia why, ukitaka alosoma
Ningeshauri Bluray, ila kingereza chake noma
Anaongea in a way, tafsiri zinagoma
Pedejee sishauri, unless wahusudu.

Swadaktaaaaaaaaaa... Hili ndio jukwaa laa Lugha haswaa
 
Shosti unaniangusha, kujiliza hadharani

Penzi usimbanie, aliye na niya hasa
Ila usikimbilie, Fidel Chrispin Masa
Hapana watamkie, usije wapa hamasa
Mbili zero moja mbili, ndoa zao watangaza.

Lizy big up,nimeipenda sana hii,nimekugongea thanks kule.
 
Afwezeli, manake ulivokuwa mchoyo wa thanks kweli Lizy kakukuna.

Wewe salimia kwanza,ha ha ha mimi sio mchoyo wa thanks angalia kwenye details zangu idadi ya thanks nilizogongea watu halafu linganisha na za kwako hapo ndo tutajua nani mchoyo wa thanks.
 
Wewe salimia kwanza,ha ha ha mimi sio mchoyo wa thanks angalia kwenye details zangu idadi ya thanks nilizogongea watu halafu linganisha na za kwako hapo ndo tutajua nani mchoyo wa thanks.

Hahaha! Nilijua tu lazima uchungulie manake hupitwi. Salama lakini? Shemeji hajambo?
 
Hahaha! Nilijua tu lazima uchungulie manake hupitwi. Salama lakini? Shemeji hajambo?

Si unajua unapoleta mada lazima uwe na full info sasa nilipoona umeniita mchoyo nikaanza uchunguzi,nikagundua kuwa umeleta mada bila kuifanyia uchunguzi,Sisi tu wazima,mimi na familia yangu na shemeji yako pia mzima kabisa.
 
Poa msalimu shemeji. Akikuletea za kuleta usisahau kuniPM. Hahahaha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom