Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulimwengu wa mapenzi

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by MwanajamiiOne, Oct 13, 2009.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,470
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 48
  Wasalaamu salamuni, waungwana nawajia
  Mababu wa mizimuni, walokwisha tangulia
  Najongea kwa huzuni, najizuia kulia
  ulimwengu wa mapenzi, buriani aagia

  Ulimwengu wa mapenzi, buriani naagia
  naondoka kwa majonzi, mlango najifungia
  Si wangu nimemaizi, moyo nafungulia
  Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka

  Ninakupa zako mbawa, uruke unakotaka
  Umeyataka mabawa, meupe yaso na taka
  Nimechoka kupagawa, na penzi lenye mashaka
  Ulimwengu wa mapenzi, nawaachia wenye bahati.
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 39,810
  Likes Received: 1,025
  Trophy Points: 113
  Ndo umeshamwaga jamaa mpwa aanze kusarandia?
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,975
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nipo tayari kukupokea haney karibu tulifufue upya.
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 39,810
  Likes Received: 1,025
  Trophy Points: 113
  Mpwa usisahau kumleta Nyama Chabez ale mishikaki ya samaki.
   
 5. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 183
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 18
  Fidel ebu mwache binti wa watu mbona unamkosesha raha jamani? MJ1 endelea kujifariji bwana achana na kaka zako bwana, 'haweshi' mambo ati!
   
 6. M

  Msindima JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,021
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MJ1,vipi tena? umeamua kum-mwaga jamaa?
   
 7. M

  Msindima JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,021
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Crispin mwache kwanza MJ1 atulie.
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 39,810
  Likes Received: 1,025
  Trophy Points: 113
  Atulie kivipi mamii, anahitaji kuchangamshwa, si kuachwa. Ebo!
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,975
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Huyu analipenda limtu lisilo mpenda na kumjali sasa mm nampenda yeye hanipendi umeona sasa ni vice versa mtu umpendae yeye hakupendi na unae mpenda nae hakupendi.
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 39,810
  Likes Received: 1,025
  Trophy Points: 113
  Au mpwa nijaribu bahati yangu? Huwezi jua mipango ya Mungu bana.
   
 11. M

  Msindima JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,021
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli anahitaji kuchangamshwa ila haya mambo ya kumwambia sijui nani amsarandie bado ni mapema ujue bado ana maumivu,cha muhimu tuwe naye karibu,tumtie moyo.
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 39,810
  Likes Received: 1,025
  Trophy Points: 113
  Kusarandiwa ni sehemu ya kuchangamshwa mamii. Msindima acha kumwekea mpwa wangu kauzibe.
   
 13. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,941
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 38
  Ndio maana wengine wameamua kuwa matowashi-masista na mapadri,lakini mnawabeza wakati ulimwengu wa mapenzi nao maumivu.
  Bravo masista na mapadri!
   
 14. M

  Msindima JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,021
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Simwekei kauzibe,ye ajichangaye tu,ila kwa sasa tumfariji mwenzetu.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,975
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ndo tatizo letu si wabongo kuwekeana kauzibe yaani.
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,975
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Haya mfariji huku ukinipigia pande basi. Kama una mdogo wako yupo yupo mm naoa 2012 fanya mchakato basi Msindima.
   
 17. M

  Msindima JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,021
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmhh wewe Fidel80,kweli mdogo ninaye lakini mmhh wewe tena jamani,mchakato unatakiwa ufanye mwenyewe.
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,846
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 48
  Pole dada pole, pole mwana jamii
  mapenzi polepole, ndani ya yetu jamii
  ulianza hisi polepole, ukadhani huumii
  sasa yamegonga kole, watutangazia jamii


  nimekusoma kwa kitambo, kwenye forum ya jamii
  unalalama kimtindo, ewe mwanajamii
  wengi tuliona kombo, kama wana jamii
  tukasema mweke kando, akuumizaye mwanajamii

  Vera na nyamayao, walikupa zao bidii
  wote jinsia yao, walijituma kwa bidii
  vidume ni kama zao, wakaanza kwa bidii
  wakakaa kimkao, wakusherehe kibidii

  lakini hadi sasa, ewe mwana jamii
  sipati hata msasa, na kuelewa hii jamii
  ni vipi twatakasa, tena kwa zetu bidii
  kutoa ndoa takasa, ya Muumba kwa bidii?
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 39,810
  Likes Received: 1,025
  Trophy Points: 113
  Kama ulikuwa hujui, hakuna watu wanaomegana kama hao binadamu. Lol! Nikimwona padre karibu na shori wangu patakuwa hapatoshi.
   
 20. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,941
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 38
  hahahahahaaaa.Haya Bwana .Pengine ushawahi kulizwa na mapadri,Aisifuye mvua..........
   

Share This Page