Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

Mavella, kama ungo wako upo tayari kwenye eutelsat 16a basi jaribu kuzungusha lnb yako clockwise/anticlockwise na blindscan receiver yako.Aidha check decoder yako kama ni mpeg4 na inasapoti dvb-s2 8psk kwani freq 10804 h 30000 ni dvb-s2 8psk. Hiyo freq 11024 h 3333 uliyoipata ni dvb-s1 mpeg2.Hata hivyo ninapata mshangao kwa vile frequence hii iko mbali sana na Tanzania,nihakikishie kama huishi Tanzania.Kwenye sat eutelsat 16a ni beams mbili tu ambayo Tanzania tunaweza kupata, Eutelsat 16A South East Africa na Eutelsat 16A Saharan Africa,ukitembelea hapa flysat.com/e16a-beam.php utaelewa nn namaanisha.

frequency hii ya tv madagaska ni subsaharan africa beam ukitembelea HAPA mimi niko songea na reciver yangu ni mpeg4 dvb-s1/2 labda size ya dish cm 60 kama inadhuru.
 
haya kwa wale waliofunga KU na wanshindwa kuzipata radio zilizopo bonyeza batani hii kwenye rimoti yako TV/R utapata radio zote hakikisha chneli uliyoweka ipo upande wa ku mfano kbc.
 
Mavella, uko sahihi ,nilikuwa naangalia flysat ambako tvm haionekana. kupata channels unahitaji ungo wenye ukubwa 40dBW=120CM hii ni kwa mujibu wa [flysat.com], lakini we jaribu tu na ungo wa 3ft unaweza ukashika kwani 120cm ni estimation tu. Good luck
 
haya kwa wale waliofunga KU na wanshindwa kuzipata radio zilizopo bonyeza batani hii kwenye rimoti yako TV/R utapata radio zote hakikisha chneli uliyoweka ipo upande wa ku mfano kbc.

Kama stations 20 hv znafunguka...kîss fm,metro fm,jambo etc..
 
ATN iko wazi kwa sasa kwa kupitia king'amuzi chao AAL-003,faidi kabla hawajaifunga
 
kwanini baadhi za channels ikifika muda flani huwa ina scratch scrath au hayoneshi kabsia.
 
ATN iko wazi kwa sasa kwa kupitia king'amuzi chao AAL-003,faidi kabla hawajaifunga

Mkuu salute!
Ninatanguliza hukurani kwa elimu unayoileta hapa.
Ninaomba utuelimishe jinsi ya kutumia hiki king'amuzi ili "kung'amua channels nyingine" kama ulivyowahi kudokezea.
 
Mkuu salute!
Ninatanguliza hukurani kwa elimu unayoileta hapa.
Ninaomba utuelimishe jinsi ya kutumia hiki king'amuzi ili "kung'amua channels nyingine" kama ulivyowahi kudokezea.

nimekupata mkuu.nitafanya kama unavyotaka
 
unaweza kupata fta chaneli nyingi kutokana na uwezo wa kuwa na satdish 2 au 3,
(1)uwe na c band satdish futi 6 au 8 pamoja na lnb 3 moja iwe c band lnb na 2 ku band,
lnb ya kwanza ambayo ni c band utapata chanel 9 ambazo ni
1.itv
2.eatv
3.capital
4.tbc
5.star tv
6.channel 10 (kwa shida)
7.mtv1
8.mtv2
9.tim
lnb ya pili ni ku ambayo utaifunga juu ya ile c band ya katikati na utapata chanelli kama,
btv, sabc 1,2 na 3, f24, nollywood plus, nollywood moves, ctl, press tv, channel 44, afrika unite tv, citezen tv, emanuel tv ziko nyingi zaidi ya 70.
Lnb ya tatu ni ku utaifunga upande wa chini na hii umapata chaneli kama kbc, k24, familly tv, sayare tv (sauti ya rehema), na wbs.
Kama utakuwa na dish dogo la ku lifunge liangalie kaskazini muelekeo wa dstv utapata chaneli kama,
lcf, golfe tv, rdv, ortb, drtv internatinal, love world, ebru tv, tpa (feed) kama una hd reciever unapata na channel ten. To be cont...

mkuu kama nimekuelewa vizuri unamaana uwe na dish tatu! .. Duh! ...
 
Mkuu leo nafikiri nianze na receivers/decoders.Hicho ni kifaa kinachopokea mawimbi ya matangazo kutoka kwenye satellite husika kupitia ungo.Kwa sasa receivers zote ziuzwazo duniani kote ni DIGITAL.Ndio maana zimeandikwa mbele DVB[ Digital Video Broadcasting] Zinaitwa decoders kwa sababu zikisha pokea mawimbi zina uwezo wa kukuambia zimepokea nini[picha na sauti unayopata ndio decoding ability ya receiver yako]Kwa hiyo sio kila receiver ina uwezo wa kudecode [kukuambia nini kimepokea]mawimbi yaliopokea.Kwa sababu hiyo ndio maana kuna reiceiver inanasa mawimbi ya tv channels ambazo zinapatikana bure hewani [FTA TVs] na zingine tvs za kulipia tu.

Tunaendelea.Nimesema receivers/decoders zote ni digital ok? Ndiyo, ingawa ni digital bado zina uwezo wa kupokea(to receive)mawimbi ya anologia na kutupa picha/sauti (to decode).Receivers/decoders hizo ziko za aina anuai, nazo ni; DVB-S, DVB-T na DVB-T
DVB-S :
Hizi ni vile zenye uwezo wa kupokea mawimbi kwa njia ya satellite, nazo ziko za aina kuu mbili Dvb-s1(digital video broadcasting-satelite 1st generation) na Dvb-s2(..................2nd generation).Receivers/decoders nyingi tulizo nazo majumbani mwe2 ni Dvb-s1 mfano mediacom zote,gulf star,baadhi ya strong n.k. zote hizo mpeg2.Ricva hizo hazina uwezo wa kupokea mawimbi ya satellite 2nd generation(dvb-s2)
Dvb-s2
ni technology ya kisasa. Mfano wa ricva zake ni strong srt 4669,4930, humax ir1020,2000,2020, Ting aal-003, zuku decoder,dstv hd decoder n.k. Ricva/Decoders hizo zote ni mpeg4 compatible na nyingine ni HD compatible.
Tunasema receivers tulizonazo hazifai sana kwa sababu si tu kwamba tvs zinahamia digital bali nyingi zinahamia dvb-s2.Hebu tembelea FlySat Yahsat-1A @ 52.5° East
utaona ninachomaanisha.Utaona kuna baadhi ya tvs unahitaji revceiver ya dvb-s2 ili uikamate.Kwa ufupi kwenye dvb-s unahitaji dish kupata mawimbi ya tvs
DVB-T: hizi ni zile zinazokamata mawimbi kwa njia ya antenna( digital video broadcasting-terrestrial) nazo ziko za aina mbili, dvb-t1 na dvb-t2.Ving'amuzi vya startimes na ting aal-001 na al-002 viko hapo.
DVB-C: hivi hukamata na kutoa matangazo kwa njia ya cable.Aina hii ya ving'amuzi c mashuhuri sana Africa hususani Tanzania. Kulingana na Jina la Thread hii mijadala yote itahusiana sana na DVB-S receivers/decoders na fta tv stations.


mkuu yangu ni hii hapa... sun ray 4 HD 800 se ni Dream box 800se clone everything dream box 800se does this machine do better plus access ya wifi .... nipo nje ya bongo nakusanya hivi vifaa nikirudi tanzania likizo nikamfungie bimkubwa ungo home pale (DAR) wazee angalau wapate kuburudika sitaki kusikia stations za kulipia sasa hii thread yako muhimu sana ila kama stations za kibongo ni C band only mpaka sasa naona kuna umuhimu wa wa dish mbili sababu channels toka bara arab kule muhimu kidogo kwa bimkubwa na zinapatikana nyingi kwa KU band mzEe naye agalau za sports kama epl mzee ni mnazi wa Newcastle united sasa EPL kwake pia itakuwa safi akiona match hata mbili tatu FTA ... nadhani umeelewa tatizo langu! channel za bongo zinatakiwa na za watu mbelembele zinatakiwa ... Na pia dish size gani unaushuri..?
vipi kuhusu bei za madish huko bongo ni bei sana..??! kama ni cheap ntabeba receiver tu


kwa nyuma

DSC00046.jpg




kwa mbele





 
Mavella, uko sahihi ,nilikuwa naangalia flysat ambako tvm haionekana. kupata channels unahitaji ungo wenye ukubwa 40dBW=120CM hii ni kwa mujibu wa [flysat.com], lakini we jaribu tu na ungo wa 3ft unaweza ukashika kwani 120cm ni estimation tu. Good luck

nimepata chaneli 2 za bay TV na 1kzn TV kutoka south afrika ambazo ziko amos 5 at 17e ktk mwelekeo huohuo wa eutelsat 16A at 16e bila kusogeza dish
 
Hongera Mavella kwa kazi nzuri unazoendelea kuzifanya humu ndani. Ni dhahili kuwa ungo wako upo kwenye sats Amos/ Eutelsat 16a na pengine hupati frequences zingine ni kwa 7bu ya size ya dish.
 
Hongera Mavella kwa kazi nzuri unazoendelea kuzifanya humu ndani. Ni dhahili kuwa ungo wako upo kwenye sats Amos/ Eutelsat 16a na pengine hupati frequences zingine ni kwa 7bu ya size ya dish.

Natumia dish dogo(ku band) Intelsat7/10(68E) hapa napata KBC,K24,family tu...Bwana arselona naomba unisaidie kupata chnls nyngnezo hasa KISS TV hawa wanaonesha mpira EPL na UEAFA!..Natumia media com receiver!..nsaidie hata frequencies zake itakuwa mzuka zaidi!...
 
Leo niendelee na kifaa kingine kiitwacho satallite dish(ungo). Kabla sijaendelea na somo la leo naomba niwarudishe nyumba kidogo kwenye somo lilopita lililohusu receicers/decoders kwamba kuna baadhi ya ricva/decoders zina uwezo wa kutumika kama dvb-s, dvb-c na dvb-t. Mfano wa decoders hizo ni strong srt 4902 na sun ray 4 HD 800se ambacho Viper anacho.

kuna aina kuu mbili za nyungo nazo ni; prime focus dishes(maarufu kama c-band dishes) na offset/parabolic dishes(maarufu kama ku-band dishes).Kwa aina ya kwanza kuna ambazo ni za bati na za wavu zenye ukubwa unaoanzia 6ft na kuendelea.Ni madishi ambayo ni ya duara.Madishi hayo ndiyo mengi sana majumbani mwetu. Kati ya bati na ya wavu, ningependa watu waelewe kuwa yabati ni bora zaidi kwani yana uwezo wa kukamata frikwensi dhaifu kuliko za wavu.Aidha zinaweza kutumika kukamata frikwensi za ku.
mesh-c-band dish.jpeg c-band dish.jpeg Aina ya pili ni madishi, ni yale yenye umbo la yai Ambayo dstv, zuku na Ting wanayatumia.Madishi hayo yana ukubwa kati ya 2ft -6ft.Kama ilivyo kwa madishi ya aina ya kwanza watu wengi tunafikiri kwamba aina hayo ya madishi yanatumika tu kwa kupokea mawimbi ya ku pekee,si kweli bali yanaweza pia kupokea mawimbi ya c-band pia kutegemea na ukubwa wake. DSC01226.jpg ku- band dish.jpeg haya ni madishi ya ku.
Kuna aina kuu mbili za LNBs(Low Noise Blockers), nazo ni Ku/universal LNBs na C-band/standard LNBs.Tazama picha hii ya ku-lnbs
ku- band lnbs.jpeg na nyingine ya c-band lnbs mwisho ya makala hii.
Ingawa kuna aina kuu mbili tu ya lnbs lakini kuna aina ya tatu ya lnb nayo ni muunganiko wa aina kuu hizo mbili nayo ni Ku/C- band lnbs kama inavyoonekana katika picha hii
ku-c band lnb.jpg Aidha kuna kifaa kingine kinachopatikana ndani ya C-band lnbs kinaitwa Dielectric fiber( kitu kama kisabuni vile). ukiangalia picha zifuatazo utaweza kufahamu vizuri c-bandlnb_ilist_2.jpg solar_ring_cband.jpg Nilisema inawezekana kutumia offset dish kupata mawimbi ya c-band. Tizama picha ifuatayo scalar.jpeg nitarudi tena kuendelea na somo hili hili kesho Mungu akipenda.
 

Attachments

  • c-band lnbs.jpeg
    c-band lnbs.jpeg
    7.6 KB · Views: 313
Leo niendelee na kifaa kingine kiitwacho satallite dish(ungo). Kabla sijaendelea na somo la leo naomba niwarudishe nyumba kidogo kwenye somo lilopita lililohusu receicers/decoders kwamba kuna baadhi ya ricva/decoders zina uwezo wa kutumika kama dvb-s, dvb-c na dvb-t. Mfano wa decoders hizo ni strong srt 4902 na sun ray 4 HD 800 se ambayo Viper anayo.
kuna aina kuu mbili za nyungo nazo ni; prime focus dishes(maarufu kama c-band dishes) na offset/parabolic dishes(maarufu kama ku-band dishes).Kwa aina ya kwanza kuna ambazo ni za bati na za wavu zenye ukubwa unaoanzia 6ft na kuendelea.Ni madishi ambayo ni ya duara.Madishi hayo ndiyo mengi sana majumbani mwetu. Kati ya bati na ya wavu, ningependa watu waelewe kuwa yabati ni bora zaidi kwani yana uwezo wa kukamata frikwensi dhaifu kuliko za wavu.Aidha zinaweza kutumika kukamata frikwensi za ku. View attachment 68884View attachment 68884View attachment 68884

Aina ya pili ni madishi, ni yale yenye umbo la yai Ambayo dstv, zuku na Ting wanayatumia.Madishi hayo yana ukubwa kati ya 2ft -6ft.Kama ilivyo kwa madishi ya aina ya kwanza watu wengi tunafikiri kwamba aina hayo ya madishi yanatumika tu kwa kupokea mawimbi ya ku pekee,si kweli bali yanaweza pia kupokea mawimbi ya c-band pia kutegemea na ukubwa wake.

Mkuu tunakusoma vizuri ... Tunasubiri urudi uendelee na hili darasa... Nishaelewa c band na hicho kisabuni... Nasubiri darasa la ku band
 
Bila shaka somo ililopita limeeleweka vizuri kwani mpaka sasa hakuna maswali. Mwenzenu leo nilikuwa nafanya utafiti kujua ni kwa namna gani nitanunua receiver nzuri kwa mahitaji yangu. Nimeona kuna aina moja ya receiver ambayo kwa mtazamo wangu ni box nzuri sana si tu kwa unafuu wa gharama ya ununuzi bali pia kwa uwezo wake.

Hii Skybox F3 ambayo ni dvb-s2 HD decoder,ina modulation ya qpsk,8psk na 16psk(Ting AAL-003 ina pia qpsk na 16spk na 8spk) Ina usb port moja, Rj45 port, 0ne smartcard reader port inasapoti irdeto2, sharp tuner, inasapoti pia wifi. Pia inamfanya mtumiaji kuweka codes kufungua en*****ed tv channel. Decoder hiyo inauzwa china kwa gharama ya usd87 pamoja na gharama za usafiri kwa HDL.
Sasa nikilinganisha na strong srt 4669 ambayo inauzwa kati ya tsh 180000-200000, bado ni cha mtoto.Srt 4669 ina modulations za qspk na 8spk tu, sio Hd,ina weak tuner na haina wifi.
Aidha naendelea kutafiti kuona kama ninaweza kuinstall firmware ya decoder nyingine ya kichina kwenye decoder ya ting(aal-003).Ili kuweza kufanya hivyo nitalazimika kwanza kufanya backup ya ting.

.
 
Mavella " nimepata chaneli 2 za bay TV na 1kzn TV kutoka south afrika ambazo ziko amos 5 at 17e ktk mwelekeo huohuo wa eutelsat 16A at 16e bila kusogeza dish "

Bro Mavella naomba ujaribu kuzungusha LNB @ 3:00pm ( namaanisha pale kwenye fitting ya cable panakuwa at 3:00pm ukiwa mbele ya dish lako )
 
"Natumia dish dogo(ku band) Intelsat7/10(68E) hapa napata KBC,K24,family tu...Bwana arselona naomba unisaidie kupata chnls nyngnezo hasa KISS TV hawa wanaonesha mpira EPL na UEAFA!..Natumia media com receiver!..nsaidie hata frequencies zake itakuwa mzuka zaidi"..Mchakatoh

Kaka mchakatoh sijaweza kuona sat yoyote inayorusha kiss tv fta, kwa vile haja yako ni ucl na epl una njia mbili mbadala, ya kwanza ni kuuelekeza ungo wako mwelekeo wa dstv itakuwezesha kupata ORTB tv ya benin ambayo pia inaonyesha mpira(rdv na drtv kwa sasa hazipatikani tena hapo)
Njia ya pili ni kununua dvb-s2 decoder na offset dish la >3ft ili kukufanya unase sats eutelsat/amos ambapo utapata channels nyingi za sports zikiwemo rdv, drtv,rst1 ortb setanta africa na crtv
 
Nina srt 4996 naweza pata chanel gani ? . Kwa dish ya ft 6 c band au ku cm 90. Nina dongle avatar 2. Je unayo software mpya mkuu ?
 
Back
Top Bottom