Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

im not sure but mwaka jana nliipata tbc , then naskia na mozambique pia
ku inakuwa upande wa emmanuel tv? Au kbc.. Na frequency pamoja na symbol rate zinazotumika ni zipi? Hata nikipata mozambique itanifaa
 
mkuu eti kwenye kU band unaweza pata chanel za itv, eatv,channel 10, capital,tbc na star tv?

unaweza kupata. Kupitia dekoda ya ting mkuu. Za bure kwa sasa hakuna. labda startv na tbc tena kwa muda mchache tu kupita nss 12 pale kwenye kbc
 
Chaneli za bongo unapata kwa ku muelekeo wa dstv ila ni za kulipia kwenye pakegi ya ting iliyo fta ni chan ten tu.
 
Vipi MBC1,2,3,4 na DUBAI SPORTS zinapatikana kama FTA? Na kwa dish size gani? Na Aina gana ya RECEIVER?
 
ku inakuwa upande wa emmanuel tv? Au kbc.. Na frequency pamoja na symbol rate zinazotumika ni zipi? Hata nikipata mozambique itanifaa

upande wa emanuel tv... But hat hyo kbc n ku but inawekwa upande wa mbele... Ilikua hapa 11855 H 4444
 
Habari jf. Baada ya tathmini ya muda mrefu kuhusu masuala ya sat tvs na jinsi wa2 wanavyohangaika kutwa kucha kutafuta elimu hiyo, nimeona mimi nami kuanzisha mada hii ili niweze kuwafahamisheni kidogo ninachoelewa kuhusu masuala ya sat tv. Kwa uzi huu utajishughulisha zaidi na sattelites gani zinapatikana maeneo ye2, jinsi ya kuweka sat dishes na sizes zake. Aidha nategemea kupata maswali kutoka kwenu ili niweze kutoa majibu. Mijadala imefunguliwa rasmi.

mkuu tupo wengi tunaopenda kuyajua haya mambo,unaonaje ukajiandaa na kuendesha somo lote kuanzia maana ya setlite na zinavyofanya kazi mpaka jinsi ya ku connect kwenye hizo satlite?
 
Vipi MBC1,2,3,4 na DUBAI SPORTS zinapatikana kama FTA? Na kwa dish size gani? Na Aina gana ya RECEIVER?

chanel hizo zinapatikana fta at 7WA magharibi ukiwa na ungo wa ku band angalau wa ft 5 na ricva hata ya mpeg2.
 
Combining 2LNBs on 90cm Offset Dish Intelsat 7 10 and Nss12 ku.jpg Niko nafanya majaribio kama naweza kuposti pics:eyebrows::eyebrows::eyebrows::eyebrows:
 
Mkuu leo nafikiri nianze na receivers/decoders.Hicho ni kifaa kinachopokea mawimbi ya matangazo kutoka kwenye satellite husika kupitia ungo.

Kwa sasa receivers zote ziuzwazo duniani kote ni DIGITAL.Ndio maana zimeandikwa mbele DVB[ Digital Video Broadcasting] Zinaitwa decoders kwa sababu zikisha pokea mawimbi zina uwezo wa kukuambia zimepokea nini[picha na sauti unayopata ndio decoding ability ya receiver yako]

Kwa hiyo sio kila receiver ina uwezo wa kudecode [kukuambia nini kimepokea]mawimbi yaliopokea.Kwa sababu hiyo ndio maana kuna reiceiver inanasa mawimbi ya tv channels ambazo zinapatikana bure hewani [FTA TVs] na zingine tvs za kulipia tu.

Tunaendelea.Nimesema receivers/decoders zote ni digital ok? Ndiyo, ingawa ni digital bado zina uwezo wa kupokea(to receive)mawimbi ya anologia na kutupa picha/sauti (to decode).Receivers/decoders hizo ziko za aina anuai, nazo ni; DVB-S, DVB-T na DVB-T
DVB-S :
Hizi ni vile zenye uwezo wa kupokea mawimbi kwa njia ya satellite, nazo ziko za aina kuu mbili Dvb-s1(digital video broadcasting-satelite 1st generation) na Dvb-s2(..................2nd generation).Receivers/decoders nyingi tulizo nazo majumbani mwe2 ni Dvb-s1 mfano mediacom zote,gulf star,baadhi ya strong n.k. zote hizo mpeg2.Ricva hizo hazina uwezo wa kupokea mawimbi ya satellite 2nd generation(dvb-s2)

Dvb-s2
ni technology ya kisasa. Mfano wa ricva zake ni strong srt 4669,4930, humax ir1020,2000,2020, Ting aal-003, zuku decoder,dstv hd decoder n.k. Ricva/Decoders hizo zote ni mpeg4 compatible na nyingine ni HD compatible.

Tunasema receivers tulizonazo hazifai sana kwa sababu si tu kwamba tvs zinahamia digital bali nyingi zinahamia dvb-s2.Hebu tembelea FlySat Yahsat-1A @ 52.5° East
utaona ninachomaanisha.Utaona kuna baadhi ya tvs unahitaji revceiver ya dvb-s2 ili uikamate.Kwa ufupi kwenye dvb-s unahitaji dish kupata mawimbi ya tvs

DVB-T: hizi ni zile zinazokamata mawimbi kwa njia ya antenna( digital video broadcasting-terrestrial) nazo ziko za aina mbili, dvb-t1 na dvb-t2.Ving'amuzi vya startimes na ting aal-001 na al-002 viko hapo.

DVB-C: hivi hukamata na kutoa matangazo kwa njia ya cable.Aina hii ya ving'amuzi c mashuhuri sana Africa hususani Tanzania. Kulingana na Jina la Thread hii mijadala yote itahusiana sana na DVB-S receivers/decoders na fta tv stations.
 
Hili si dish tunalomaanisha hapa. Hiki ni kibonzo za dishi.Ni pm contacts zako nikupeleka kwa akina masele wa mizengwe. Fanya fasta usije ukakosa nafasi
 
Arselona

ivi mkuu arselona hawa jamaa wa ting wamehama eutelsat 36A au wamebadili frequency nina mda mrefu signal yao siipati.
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa kwenye satellite ya eutelsat 7A at 7e nimeamua kuhamia eutelsat 16A at 16e kuifuata hasa RDV senegal ambayo inaonyesha EPL hata mechi 2 kwa wiki ambayo nilikuwa naipata eutel 36A at 36e na ikapotea, lakini nimebahatisha kuipata TV madagaska tu chaneli zingine nimehangaika nimezikosa natumia reciever ya eurostar HD DVB-S2 wakuu kuna mwenye maujanja na satellite hii anipe.
 
Inasemekana wanadaiwa na wamiliki wa eutelsat 36A.Tumshukuru Mungu tu kwamba decoda zao zinatumika vile mtu apendavyo tofauti na zile za iliyokuwa GTV.
 
Viper, MBC package ipo fta ila kutokana na geographical location itakuwa vigumu sana kupatikana, ukiwa arusha unahitaji angalau dishi la 3m. Dubai sports ok ila haionyeshi epl, inaonyesha bundesliga. Free epl inapatikana @ Amos 5 na W3c.
 
Back
Top Bottom