Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

mkuu embu endelea basi na hili somo kwa utaratibu mzuri basi maana na mimi dish langu ft6 lipo kama pambo tu, hamna linachoonyesha, nimehangaika wee wapi..kila fundi nnayemtafuta ananipiga kalenda tu..nipo mkoani!! hapo uliposema pima cm30 kutoka nguzo inapoishia embu elezea vizuri basi kivipi??
 
Dish langu ni la futi 6, LNBF ni C-Band, Receiver ni media Com MFT 910+New. Nilifanikiwa ku-install local channels ITV(na ndugu zake), Star TV,TBC1. Tatizo radio zake sizipati? Pili, nimenunua LNB ya pili C-Band, naomba kanuni za kuifunga na frequency zilizo upande mmoja na aljazeera. Tatu, ninashindwa kupata channel ten. Ahsante.

kuna mediacom ambazo hazina progam ya radio ambayo ina taa nyekundu bila shka ya kwako ipo hivyo
 
Nilishawahi kutumia tumia mediacom 910 new receiver, yenyewe ina sapoti radios.chagua channel mfano tbc1 na bonyeza kitufe cha audio,chagua audios zinazoonekana.
 
Nilishawahi kutumia tumia mediacom 910 new receiver, yenyewe ina sapoti radios.chagua channel mfano tbc1 na bonyeza kitufe cha audio,chagua audios zinazoonekana.

Ninashukuru sana mkuu, nimefanikiwa. Nilikuwa ninapitia sehemu isiyosahihi.
 
Arselona

Bila shaka mmekusanya vitu vyote nilivyoainisha hapo juu, sasa twende kazi.Unganisha ungo wako vizuri na hakikisha pale utakapoliweka pako level, umewaka kisabuni (neflon) kwenye cband lnb na uifunge kwenye dish vizuri, weka pins kwenye cable na ncha moja iungwe kwenye lnb na nyingine kwenye receiver.

Fungua receiver yako na uweke tp hizi 3642 H 8545(kama cable imeungwa vizuri utaona mstari mwekundu kwenye screen yako).Elekeza ungo wako kuelekea mashariki (angalia ungo wa jirani yako).

Kwa kutumia rula yako pima nguzo ya nyuma ya ungo 25-30cm weka alana fix kwa kutumia screw inayoonekana hapo.Tuanze kuzungusha ungo,anza kwa kuzungusha kitako cha ungo na wakati unafanya hivyo hakikisha unaangalia kwenye screen yako, utaona ule mstari mwekundu unaongezeka asilimia na acha kuzungusha pale utakapojiridhisha kuwa mstari mwekundu hauongezeki tena.

Sasa rudi kwenye ile screew nyuma ya dish ifungue na elevate or lower dish lako, utafika pointi ambayo utaona kuna mstari mwingine wa kijani umetokea.hapo utakuwa umeipata satellite ya intelsat906 scan kupata channels zako za IPP Media. Ukiona haijatokea mistari hiyo toa H na weka V na urudie zoezi lako.Nakaribisha mijadala.
 
Last edited by a moderator:
Bila shaka mmekusanya vitu vyote nilivyoainisha hapo juu, sasa twende kazi.Unganisha ungo wako vizuri na hakikisha pale utakapoliweka pako level,umewaka kisabuni (neflon) kwenye cband lnb na uifunge kwenye dish vizuri, weka pins kwenye cable na ncha moja iungwe kwenye lnb na nyingine kwenye receiver.

Fungua receiver yako na uweke tp hizi 3642 H 8545(kama cable imeungwa vizuri utaona mstari mwekundu kwenye screen yako).Elekeza ungo wako kuelekea mashariki (angalia ungo wa jirani yako).Kwa kutumia rula yako pima nguzo ya nyuma ya ungo 25-30cm weka alana fix kwa kutumia screw inayoonekana hapo.

Tuanze kuzungusha ungo,anza kwa kuzungusha kitako cha ungo na wakati unafanya hivyo hakikisha unaangalia kwenye screen yako,utaona ule mstari mwekundu unaongezeka asilimia na acha kuzungusha pale utakapojiridhisha kuwa mstari mwekundu hauongezeki tena.

Sasa rudi kwenye ile screew nyuma ya dish ifungue na elevate or lower dish lako, utafika pointi ambayo utaona kuna mstari mwingine wa kijani umetokea.hapo utakuwa umeipata satellite ya intelsat906 scan kupata channels zako za IPP Media. ukiona haijatokea mistari hiyo toa H na weka V na urudie zoezi lako.Nakaribisha mijadala.

mkuu mi nimekupata vizuri , sasa hapo unapopima cm 30 kwenye nguzo ya nyuma...ni ipi? ile inayotoka juu kuingia ndani au ile ya chini na unapimia kutoka juu kwenda chini au chini kwenda juu?? msaada pliiiz mkuu kwa hilo!!

mi nimeshajaribu sana hivyo ila (ingawa hapo kwenye kupima tu ndo bado kunanitatiza)..na nilifanay kama hivi: baada ya kuunga kila kitu sawa nikafungua receiver kama ulivyosema na kweli nikaona huo mstari mwekundu na nimejaribu kuzungushazungusha dish mpaka ikafika ukawa unafika hadi 75%, kutokea hapo kila ninavyojaribu kupandisha a kushusha dish (elevation) ili nipate kuona huo wa kijani hamna kitu..!!

satellite nimeselect hiyo ya intelsat 906 na kile kipande nimeweka kwenye lnb na kimekaa vizuri tu... ila kuna sehem moja tu ambayo nikitoa hiki kipande kwnye lnb na nikiselect satellite ya asia (105) sijui afu nikizungusha dish kuna mahali napata huo wa kijani na nikiscan napata aljazeera na chanel 2 za kihindi tu na nyingine za kihindi pia ila scrambled, na nikirudshia kile kipande zinapotea zote(no signal) ...

sijui nakosea wapi??
 
sijui nini

Kaka naona umeanza kunielewa. Naomba u2mie hiyo asiasat105 kupata chaneli za bongo.Ikamate kwanza hiyo aljazeera, halafu kiweke kile kisabuni kwenye lnb, weka tp hizi 3642 H/V 8545 fungua ile screw iliyoko nyuma ya ungo na lower dish lako kidogo sana kwa angalau 4cm kupata signal. Unaweza substitute H for V.

(unapopima cm 30 kwenye nguzo ya nyuma...ni ipi?) Ni ile ya juu na upime kutoka juu na ufungie screew pale utakapowekea alama
 
Last edited by a moderator:
Hiyo sat ya w3c 16 e bem yake inafika hapa bongo ? Je dish saizi gani ?
upo lacation gani kaka? W3C inapatikana vizuri sana kwa offset dish la angalau 75cms. Sijui jinsi ya kuposti pics tu ningekupostia beam hapa na pics mbalimbali za aligments za nyungo(naomba mnipe somo)
 
Kaka naona umeanza kunielewa.

Naomba u2mie hiyo asiasat105 kupata chaneli za bongo.Ikamate kwanza hiyo aljazeera, halafu kiweke kile kisabuni kwenye lnb, weka tp hizi 3642 H/V 8545 fungua ile screw iliyoko nyuma ya ungo na lower dish lako kidogo sana kwa angalau 4cm kupata signal.

Unaweza substitute H for V.
(unapopima cm 30 kwenye nguzo ya nyuma...ni ipi?) Ni ile ya juu na upime kutoka juu na ufungie screew pale utakapowekea alama

Shukrani sana kaka, umeniokoa sana..hivi nikitoka tu kwa ofisi nikifika kitu cha kwanza ndo hiyo kazi...hopefully nitaleta majibu kesho!! i hope it will work...thank u sana!
 
upo lacation gani kaka? W3C inapatikana vizuri sana kwa offset dish la angalau 75cms. Sijui jinsi ya kuposti pics tu ningekupostia beam hapa na pics mbalimbali za aligments za nyungo(naomba mnipe somo)

Morogoro.
 
shukrani sana kaka, umeniokoa sana..hivi nikitoka tu kwa ofisi nikifika kitu cha kwanza ndo hiyo kazi...hopefully nitaleta majibu kesho!! i hope it will work...thank u sana!

kaka lakini ujue kupata chanel za ipp sio kazi. Shuhuli ipo kwenye star na ch.ten
 
Mi hizo startv, nmezkosa bana, almanusra nivunje kiuno juu ya bati!
Hivi upande wa kulia au kushoto wa Cband nikiweka lnb tapata channel zipi kwa position hii ya locol tvs?
 
Mi hizo startv, nmezkosa bana, almanusra nivunje kiuno juu ya bati!
Hivi upande wa kulia au kushoto wa Cband nikiweka lnb tapata channel zipi kwa position hii ya locol tvs?

kaka alafu ujue receiver za cku hizi ni kimeo mfano mimi natumia media com 910plus haina shida kabisa ni za zamani cku hizi hakuna.na nikiitoa nikifunga 910new ni shida kwenye star na zingine pia 930 ni tabu mwanzo mwisho
 
Je kuna channel zozote za fta zinazoonyesha mechi za mpira wa ngazi yoyote kutoka South America? Kama zipo ni kwenye satellite gani na frequency zipi?
 
Je kuna channel zozote za fta zinazoonyesha mechi za mpira wa ngazi yoyote kutoka South America? Kama zipo ni kwenye satellite gani na frequency zipi?

Mimi sijui kutengeneza ila kitu kipo mtaani na watu wanafanya dishi la kawaida unaingiza software katika receiver (media com). Unaingiza na cable chungulia nyuma ya receiver utaona hio sehemu. Ukishaingiza hio software chanel za aljazeera zitaongezeka utapata aljazeera sport zote.

Aljazeera sport inaonesha mipira yote ya south america na pia kuna tetesi mwakani wakaonesha ligi ya uingereza kwa kuwapokonya licence abudhabi sport
 
Back
Top Bottom