Ulimtambua vipi kuwa huyu ndiye mwenyewe?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,463
911,172
ULIMTAMBUA VIPI KUWA HUYU NDIYE MWENYEWE…..
(Getting to know her/him)

Hivi mwandani wako ulimtambuaje kuwa ndiye yeye?
Hivi ni maujanja yepi wewe uliyatumia kumpima yeye?
Ni vigezo vipi vilikutongoza hadi kujua umelamba dume?
Hivi ni vichocheo vipi vilikufanya uone ya kuwa umewasili?
Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu

Kauli yake mwenyewe huitia kitanzini na kuishibisha azma zake!
Aongeacho mara nyingi sicho kilichopo moyoni kwake wala!
Tabasamu lake lalenga kuijenga kauli ambayo si lazima iwe na kweli!
Kamwe kauli au hata tabasamu lake kuwa kioo cha moyo wake!
Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu

Kauli na taswira yake huoana na moyo wake masijala ya kukataa…
Pindi moyo wake umekuasi kata katu basi shabaha wewe hulengwa…
Bila haya au huruma jipu kukupasulia kuwa hakuhitaji nawe kulia..
Na kwa kufanya hivyo huwa kajitendea mwenyewe ubinadamu..
Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu

Ni mitihani ipi uliitumia kuupima moyo wake?
Hata kuridhia yeye ndiye na hakuna mwingineo?
Kama ulienda mkichamkichwa basi ilikula kwako!
Kama uliserereka na kauli au taswira basi wewe teja!

Dah to me it is a long story !!Kwakuwa nilikuwa naye kama rafiki lakini nikakuta tumekuwa marafiki kwani siku yakwanza tulienda Casablanca ilikuwa kinondoni........then ndo ukawa mwanzowetu na sasa ni Mama watoto na ni family yenye furaha!!kwa kujivunia uwepo wa Baba na mama!!
 
Mimi nimeangukia kwenye utenzi wa mwisho.............lol
 
Dah to me it is a long story !!Kwakuwa nilikuwa naye kama rafiki lakini nikakuta tumekuwa marafiki kwani siku yakwanza tulienda Casablanca ilikuwa kinondoni........then ndo ukawa mwanzowetu na sasa ni Mama watoto na ni family yenye furaha!!kwa kujivunia uwepo wa Baba na mama!!

KakaKiiza..long story is yet to be told.......................ulimtambuaje? kwenda Casablanca pekee yake hakutoshi kamwe........kukufanya ukamtambua kuwa she is the one for you and forever and evermore for you safe kkeeping........there must be other reasons..............
 
Last edited by a moderator:
huwezi amini alipenda vidole vyangu vya mkononi, aliniona napanda kwenye daladala ya mwenge posta akaona nimeshika mlango ili kupanda, akaadmire vidole kabla hajaona sura wala umbile langu! hakuwa anakuja posta alikuwa amemsindikiza rafikye kupanda daladala ilibidi apande! aliponiongelesha kunisalimia baada ya kushuka posta, i said what a sweet voice, a manish voice! the rest is history, kha umenikumbusha mbali!
 
Taswira mwayego...........heri ingekuwa kauli

Taswira bila ya kauli.........hii ni kali nifhamuvyo........................kauli njema humtoa nyoka pangoni.......................lakini wewe Elizabeth Dominic hata neno tu hukulihitaji...........hapo u were more than teja...........
 
Last edited by a moderator:
huwezi amini alipenda vidole vyangu vya mkononi, aliniona napanda kwenye daladala ya mwenge posta akaona nimeshika mlango ili kupanda, akaadmire vidole kabla hajaona sura wala umbile langu! hakuwa anakuja posta alikuwa amemsindikiza rafikye kupanda daladala ilibidi apande! aliponiongelesha kunisalimia baada ya kushuka posta, i said what a sweet voice, a manish voice! the rest is history, kha umenikumbusha mbali!

cacico.......yeye vidole naye akakugwaya bila ya chenga ,.....................na wewe je what really happended....just a mnly voice?................there ought to be more...................a gentle aura......................that was least threatening to you made you feel safe in his ably hands? Or what was it that made you say I do...........
 
Last edited by a moderator:
Taswira bila ya kauli.........hii ni kali nifhamuvyo........................kauli njema humtoa nyoka pangoni.......................lakini wewe Elizabeth Dominic hata neno tu hukulihitaji...........hapo u were more than teja...........

Teja si kidogo, lakini nimejifunza.................suluba nilizozipata si kidogo, mpaka rafiki yangu moja uwa aliniambia ulimtaka mzuri kwani ulitaka kumpika umle...........lol
 
huwezi amini alipenda vidole vyangu vya mkononi, aliniona napanda kwenye daladala ya mwenge posta akaona nimeshika mlango ili kupanda, akaadmire vidole kabla hajaona sura wala umbile langu! hakuwa anakuja posta alikuwa amemsindikiza rafikye kupanda daladala ilibidi apande! aliponiongelesha kunisalimia baada ya kushuka posta, i said what a sweet voice, a manish voice! the rest is history, kha umenikumbusha mbali!

Dah kuna mtu/watu bwana wana vidole, akikuwekea vidole say amekushika mkono au begani raha sana....
 
Back
Top Bottom