Ulimboka adakwa kwa kutaka kumhonga Kado

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
Waandishi Wetu, Dar na Morogoro

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe amekamatwa na polisi mkoani Morogoro akihusishwa na njama za kuhujumu mchezo wa Ligi Kuu baina ya Simba na Mtibwa uliopangwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri.Mshambuliaji huyo aliyetemwa na mabingwa hao wa soka wa Tanzania Bara msimu uliopita alikamatwa juzi na kuachiwa kwa dhamana jana asubuhi baada ya kuhojiwa na polisi wa kituo cha Manungu.

Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa Ulimboka alikamatwa akiwa na Sh400,000 na alipohojiwa alidai kuwa alikuwa akienda kumlipa deni kipa wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kado.

Polisi walithibitisha kukamatwa kwa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa, lakini wakasema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo unaendelea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye aliliambia Mwananchi jana kuwa uongozi wa Mtibwa wilayani Mvomero ulimfikisha Ulimboka kituo cha polisi kwa tuhuma za kutaka kutoa hongo ya Sh400,000 kwa Kado ili acheze chini ya kiwango kwenye mechi ya leo.

"Ni Kweli tumepokea taarifa hizo kuwa Ulimboka alifikishwa kituoni Mtibwa baada ya kujaribu kumpa Kado fedha kiasi hicho ili aachie mabao katika mchezo wao wa kesho [leo] dhidi ya Simba," alisema Kamanda Andingenye.

‘’Hata hivyo, Ulimboka amekana kuwa hakutaka kumrubuni kipa huyo na kusema ni kweli alikwenda Mtibwa akiwa na kiasi hicho cha fedha kwa lengo la kumlipa deni mchezaji huyo kwa sababu (Kado) ni rafiki yake ndani na nje ya mpira.

"Alitwambia kwamba anachofahamu katika siku za nyuma yeye alimwazima Kado kiasi hicho cha fedha na alifika Mtibwa kwa kuwa wakati huo ulikuwa muda sahihi wa kwenda kumlipa kwa kuhofia kuwa kama angechelewa, angeweza kumuudhi."

Kado amekuwa mmoja wa wachezaji nyota walioibukia katika siku za karibuni na alionyesha kiwango cha juu wakati Taifa Stars ilipolazimisha sare ya bao 1-1 na Algeria mjini Blida.

Kipa huyo anatarajiwa kusimama langoni Oktoba 9 wakati Stars itakapoikaribisha Morocco kwenye mechi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2012.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Mtibwa Sugar ziliarifu Mwananchi jana kuwa walipokea taarifa kutoka kwa Kado akieleza kuwa Ulimboka alikuwa akitaka kumpatia fedha ili aiachie Simba katika mchezo wa leo na ndipo wao wakamshauri ampe muda ili wafike mahali (Manungu) wakiwa na polisi na ndivyo alivyofanya.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, afisa habari wa klabu ya Simba, Clifford Ndimbo alikana klabu yake kuhusika na tuhuma hizo na kudai kuwa kuna watu wanataka kuwavuruga ili wafanye vibaya katika mchezo huo.

''Sisi hatuhusiki na tuhuma hizo... kwanza Ulimboka aliondoka Simba kwa ugomvi, iweje leo uongozi wetu umtume atoe rushwa? Habari si za kweli,'' alisema Ndimbo.

Lakini tangu habari hizo zilipofumuka jana asubuhi wadau mbalimbali wa Simba, wakiwemo waandishi watano wa habari za michezo walikuwa wakipiga simu kujaribu kushawishi habari hiyo isichapishwe na Mwananchi kwa madai kuwa itashusha heshima ya klabu hiyo.

Tukio hilo limetokea wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiwa limetangaza kuwafungia waamuzi wanne kwa makosa ya kuvurunda mechi walizochezesha za Ligi Kuu Bara zinazoihusisha Simba, Yanga, Azam na Kagera. Klabu za Azam na Arusha FC ziliwahi kulalamikia uamuzi wa mechi zao dhidi ya Simba na Yanga zikidai uamuzi ulilenga kuzibeba timu hizo kongwe nchini.

Ulimboka adakwa kwa kutaka kumhonga kipa
 
Dah hii imeishushia hadhi Simba mwaka jana gemu nyingi walikuwa wanafanya hivi
 
Hii habari imekaa ki-majungu-majungu na kuichafulia hadhi klabu yetu...mkuu unaanzisha thread na kuwa wa kwanza kuichangia huku ukuwa na muelekeo wa ki-komandoo wa jangwani...anyway..SIAMINI KAMA TIMU YA SIMBA INAWEZA KWENDA KUMUHONGA MTU KAMA KADO NA KWA KUPITIA ULIMBOKA AMBAYE ALIKUWA MCHEZAJI WA SIMBA....katika dunia ya utandawazi ya leo ni kazi ndogo sana kumpa mtu pesa..kuna ZAP, M-PESA, TIGO PESA NA BANK ACCOUNTS...kwa hiyo ilikuwa ni suala la mtu kuongea na kado na kumtumia pesa kwa njia hizo walla haihitaji mtu kusafiri kilomita 1000 kumpelekea tshs 400,000/=...HAYA NI MAJUNGU NA UPUUZI...kwa hiyo tuamini kila timu inayoshindwa na simba wamehongwa?...therefore hata polisi dodoma walimuhonga kipa wa simba??.... na azam wanavyofungwa nao kipa wao anakuwa amehongwa??....BUSARA ZICHUKUE MKONDO WAKE
 
Unamsakama bure Fidel80! Hajaanzisha yeye thread hii bali ame-quote Mwananchi. Kwa hiyo ana haki ya kuijadili. Usitetee uozo, hata kama ww ni simba. Nyie ndiyo mnadumaza mpira wa tz
 
unamsakama bure fidel80! Hajaanzisha yeye thread hii bali ame-quote mwananchi. Kwa hiyo ana haki ya kuijadili. Usitetee uozo, hata kama ww ni simba. Nyie ndiyo mnadumaza mpira wa tz

nadhani huelewi hata mpira..kwa taarifa yako duniani kote rushwa zimejaa michezoni...ila cha msingi ni kuwa habarii hii ni "fabrications" za kipuuzi na u-simba na yanga usiokuwa na msingi....

Je ulimboka anasema ametumwa na simba??...je simba hawana jinsi nyingine ya kumpatia kado pesa mpaka wamtume ulimboka?...je kila mechi waliyofungwa mtibwa alihongwa kado?...je kila mechi waloshinda simba walihonga magolikipa wa timu pinzani?....baada ya hayo..je mechi zote wanazoshinda yanga tuamini walitoa hongo??...

Tuache upuuzi tuangalie mambo yanayorudisha nyuma soka letu ...na rushwa sio moja ya vitu vinavyorudisha nyuma mpira...ingekuwa ndivyo basi juventus ya italy ingekuwa marehemu kaburini na soka la italy lingekuwa limekufilia mbali...lets tok senses now we r big boys n girlz here

ndiyo maana mpira wa tz hauendelei!!

ofcuz haundelei kwa sababu wachezaji hawalipwi vizuri na wanakopeshana viji-pesa na kulipana kabla ya mechi...ila kama unamaanisha rushwa michezoni...naomba kupingana na wewe...rushwa ilikuwapo, ipo na itaendelea kuwapo popote pale duniani penye ushabiki na ushindani katika michezo yote... rushwa zipo hadi kwenye boxing, basketball, etc...ila uendelevu wa michezo unatokana na "proper training" na "personal/individual talent development"...chini ya hapo michezo itakufa na kutoendelea duniani kote... ni maoni tuu wadau
 
hapa hatujadili "watu"..tunajadili issues... jaribu kuonyesha "UKOMAVU WA AKILI YAKO" atlest ujipatie heshima kwa jamii
Kwa watu waelewa kama sisi, tumeshakuelewa sana mheshimiwa....Thibitisha kwa hapa chini:

The Following User Says Thank You to Who Cares? For This Useful Post:

Asprin (Today)​
 
nadhani huelewi hata mpira..kwa taarifa yako duniani kote rushwa zimejaa michezoni...ila cha msingi ni kuwa habarii hii ni "fabrications" za kipuuzi na u-simba na yanga usiokuwa na msingi....

Ni kweli rushwa michezoni iko duniani kote, lakini haitetewi kama ufanyavyo. Watoa rushwa huadhibiwa
 
unajua kaka sio kwamba natetea rushwa..siipendi hata kuisikia maana inawanyima watu haki yao stahili...ila umekuwa ni utamaduni wa wanadamu wengi kujitahidi kushinda "by any means necessary" inapotokea pande mbili zinashindana...

lakini mie nachojaribu kuelewesha umma kuhusu hii mada ni kuwa ufike wakati tuelewe kuwa u-shabiki wa simba na yanga isiwe ndio chanzo cha kuandika habari hata zisokuwa na kichwa wala mkia...justifications za matokeo ya mpira kuwa timu fulani ikishinda ni rushwa zimepitwa na wakati....tuwe na justifications za kitaalamu.. na pia hoja kuwa mpira wetu haukui kwa ajili ya rushwa nayo naipinga nachoamini ni kuwa mpira unakuzwa kwa mazoezi na jitihada binafsi za wachezaji wetu na waalimu bora... nawasilisha hoja
 
nadhani huelewi hata mpira..kwa taarifa yako duniani kote rushwa zimejaa michezoni...ila cha msingi ni kuwa habarii hii ni "fabrications" za kipuuzi na u-simba na yanga usiokuwa na msingi....

Je ulimboka anasema ametumwa na simba??...je simba hawana jinsi nyingine ya kumpatia kado pesa mpaka wamtume ulimboka?...je kila mechi waliyofungwa mtibwa alihongwa kado?...je kila mechi waloshinda simba walihonga magolikipa wa timu pinzani?....baada ya hayo..je mechi zote wanazoshinda yanga tuamini walitoa hongo??...

Tuache upuuzi tuangalie mambo yanayorudisha nyuma soka letu ...na rushwa sio moja ya vitu vinavyorudisha nyuma mpira...ingekuwa ndivyo basi juventus ya italy ingekuwa marehemu kaburini na soka la italy lingekuwa limekufilia mbali...lets tok senses now we r big boys n girlz here

WRONG. Rushwa ni moja ya vitu vinavyorudisha mpira nyuma na miongoni mwa culprit wakubwa kwa mpira wetu wa hapa nchini ni hivi vilabu vinasemekana kuwa 'vilabu vikubwa vya soka nchini' vikishirikiana na Marefa kutaka ushindi hata pale wasipokuwa na uwezo. Ndio maana wanapokwenda nje hawafiki mbali kwa sababu hapa nyumbani ushindi waomara nyingi unatokana na fitna za soka na sio uwezo wao wakutandaza kandanda.
Afadhali ungesema tuwe wavumilivu na tusubiri 'gemu' hili litakavyoendelea. Kado amedai kuwa Mwakingwe alikuwa anamletea Laki 400,000/= ili acheze chini ya kiwango watakapocheza na Simba. Mwakingwe amedai kuwa Kado ni rafiki yake alikuwa anamrudishia hela aliyomkopa!! Hivirafiki yako asijue kuwa unamrejeshea hela yake nabadala yake akurupuke kudai kuwa unampelekea rushwa???
Ingekuwa vyema sana kama Mwananchi ingetaja majina ya hao waandishi watano wanaodaiwa kulipigia simu gazeti hilo ili kuomba story hiyo isitoke kwa sababu 'itaidhalilisha Simba'! Wawataje. Sio vizuri kuficha ugonjwa.
 
hii habari imekaa ki-majungu-majungu na kuichafulia hadhi klabu yetu...mkuu unaanzisha thread na kuwa wa kwanza kuichangia huku ukuwa na muelekeo wa ki-komandoo wa jangwani...anyway..siamini kama timu ya simba inaweza kwenda kumuhonga mtu kama kado na kwa kupitia ulimboka ambaye alikuwa mchezaji wa simba....katika dunia ya utandawazi ya leo ni kazi ndogo sana kumpa mtu pesa..kuna zap, m-pesa, tigo pesa na bank accounts...kwa hiyo ilikuwa ni suala la mtu kuongea na kado na kumtumia pesa kwa njia hizo walla haihitaji mtu kusafiri kilomita 1000 kumpelekea tshs 400,000/=...haya ni majungu na upuuzi...kwa hiyo tuamini kila timu inayoshindwa na simba wamehongwa?...therefore hata polisi dodoma walimuhonga kipa wa simba??.... Na azam wanavyofungwa nao kipa wao anakuwa amehongwa??....busara zichukue mkondo wake

kama ushachana passport chungulia basi hata kwenye website za magazeti ya nyumban usikimbilie kulaumu
 
Waandishi Wetu, Dar na Morogoro

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe amekamatwa na polisi mkoani Morogoro akihusishwa na njama za kuhujumu mchezo wa Ligi Kuu baina ya Simba na Mtibwa uliopangwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri.Mshambuliaji huyo aliyetemwa na mabingwa hao wa soka wa Tanzania Bara msimu uliopita alikamatwa juzi na kuachiwa kwa dhamana jana asubuhi baada ya kuhojiwa na polisi wa kituo cha Manungu.

Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa Ulimboka alikamatwa akiwa na Sh400,000 na alipohojiwa alidai kuwa alikuwa akienda kumlipa deni kipa wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kado.

Polisi walithibitisha kukamatwa kwa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa, lakini wakasema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo unaendelea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye aliliambia Mwananchi jana kuwa uongozi wa Mtibwa wilayani Mvomero ulimfikisha Ulimboka kituo cha polisi kwa tuhuma za kutaka kutoa hongo ya Sh400,000 kwa Kado ili acheze chini ya kiwango kwenye mechi ya leo.

"Ni Kweli tumepokea taarifa hizo kuwa Ulimboka alifikishwa kituoni Mtibwa baada ya kujaribu kumpa Kado fedha kiasi hicho ili aachie mabao katika mchezo wao wa kesho [leo] dhidi ya Simba," alisema Kamanda Andingenye.

''Hata hivyo, Ulimboka amekana kuwa hakutaka kumrubuni kipa huyo na kusema ni kweli alikwenda Mtibwa akiwa na kiasi hicho cha fedha kwa lengo la kumlipa deni mchezaji huyo kwa sababu (Kado) ni rafiki yake ndani na nje ya mpira.

"Alitwambia kwamba anachofahamu katika siku za nyuma yeye alimwazima Kado kiasi hicho cha fedha na alifika Mtibwa kwa kuwa wakati huo ulikuwa muda sahihi wa kwenda kumlipa kwa kuhofia kuwa kama angechelewa, angeweza kumuudhi."

Kado amekuwa mmoja wa wachezaji nyota walioibukia katika siku za karibuni na alionyesha kiwango cha juu wakati Taifa Stars ilipolazimisha sare ya bao 1-1 na Algeria mjini Blida.

Kipa huyo anatarajiwa kusimama langoni Oktoba 9 wakati Stars itakapoikaribisha Morocco kwenye mechi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2012.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Mtibwa Sugar ziliarifu Mwananchi jana kuwa walipokea taarifa kutoka kwa Kado akieleza kuwa Ulimboka alikuwa akitaka kumpatia fedha ili aiachie Simba katika mchezo wa leo na ndipo wao wakamshauri ampe muda ili wafike mahali (Manungu) wakiwa na polisi na ndivyo alivyofanya.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, afisa habari wa klabu ya Simba, Clifford Ndimbo alikana klabu yake kuhusika na tuhuma hizo na kudai kuwa kuna watu wanataka kuwavuruga ili wafanye vibaya katika mchezo huo.

''Sisi hatuhusiki na tuhuma hizo... kwanza Ulimboka aliondoka Simba kwa ugomvi, iweje leo uongozi wetu umtume atoe rushwa? Habari si za kweli,'' alisema Ndimbo.

Lakini tangu habari hizo zilipofumuka jana asubuhi wadau mbalimbali wa Simba, wakiwemo waandishi watano wa habari za michezo walikuwa wakipiga simu kujaribu kushawishi habari hiyo isichapishwe na Mwananchi kwa madai kuwa itashusha heshima ya klabu hiyo.

Tukio hilo limetokea wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiwa limetangaza kuwafungia waamuzi wanne kwa makosa ya kuvurunda mechi walizochezesha za Ligi Kuu Bara zinazoihusisha Simba, Yanga, Azam na Kagera. Klabu za Azam na Arusha FC ziliwahi kulalamikia uamuzi wa mechi zao dhidi ya Simba na Yanga zikidai uamuzi ulilenga kuzibeba timu hizo kongwe nchini.

Ulimboka adakwa kwa kutaka kumhonga kipa

Duh kweli siku za mwizi arobaini....kila siku kuhonga leo wamebambwa kazi kweli kweli....
 
nadhani huelewi hata mpira..kwa taarifa yako duniani kote rushwa zimejaa michezoni...ila cha msingi ni kuwa habarii hii ni "fabrications" za kipuuzi na u-simba na yanga usiokuwa na msingi....

Je ulimboka anasema ametumwa na simba??...je simba hawana jinsi nyingine ya kumpatia kado pesa mpaka wamtume ulimboka?...je kila mechi waliyofungwa mtibwa alihongwa kado?...je kila mechi waloshinda simba walihonga magolikipa wa timu pinzani?....baada ya hayo..je mechi zote wanazoshinda yanga tuamini walitoa hongo??...

Tuache upuuzi tuangalie mambo yanayorudisha nyuma soka letu ...na rushwa sio moja ya vitu vinavyorudisha nyuma mpira...ingekuwa ndivyo basi juventus ya italy ingekuwa marehemu kaburini na soka la italy lingekuwa limekufilia mbali...lets tok senses now we r big boys n girlz here

kama unakubali rushwa zimejaa michezoni mbona hii unataka kuikataa..?????
 
kumbe ngebe zoote zile ndani yake kuna rushwa?
sasa hizo hela si mngetumia kuzibua vyoo vya jengo lenu kariakoo ambalo kwa sasa watu wamekuwa wakinya kwenye mifuko na kutupa hovyo kutokana na uchakavu wa vyoo vya jengo?
 
Back
Top Bottom