Ulie kwenye ndoa na mahusiano imara jipime hapa!!..

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,709
Jibu hayo maswali halafu uangalie nafasi yako hapo ulipo!....Naweza kuorodhesha matamanio ya mafanikio ya mwenzangu kimaisha..YES/NO? Najua mambo anayohofia mwenzi wangu kwa nyakati tofauti.......YES/NO? Najua kuhusu nyakati muhimu kwenye maisha ya mwenzi wangu,naweza kuzitaja kama ikihitajika wakati wowote.,..YES/NO? Naweza kuorodhesha mambo matatu anayoyapenda mwenzi wangu,nitayataja kirahisi..YES/NO? Huwa ninamgusa mpenzi wangu kwa upendo mara kwa mara.....................YES/NO? Maisha yetu kuhusu tendo la ndoa ni ya kuridhisha na ninayafurahia.......YES/NO? Hua napenda kuwa karibu nae nikiwa sina majukumu mengi..................YES/NO? Mwenzi wangu ni miongoni mwa marafiki wangu wakubwa sana...........YES/NO? Mwenzi wangu ananieleza kila anapopata jambo linalomsumbua..............YES/NO? Huwa nafurahia kutoka moyoni ushauri wake.YES/NO? Huwa najifunza mengi kutoka kwake pale ambapo hatujafikia muafaka kwenye mambo mbalimbali....YES/NO? Najihisi mwenye kauli yenye nguvu au muhimu kila tukifanya maamuzi..YES/NO? Huwa nakiri kwa upendo kila nikikosea....YES/NO? Hatununiani tunaposhindwa kuelewana...........YES/NO? Ni mzuri sana katika kuniliwaza pale ninapokereka au kuvunjika moyo,...YES/NO? Huwa tunashirikiana kwenye kila jambo tuklenga kuimarisha uhusiano wetu udumu sana.....YES/NO? Tunapobishana lengo sio kushinda bali muafaka na maelewano tu........YES/NO? Kuna mambo hatuwezi kuyapatia suluhu....YES/NO? Tunashiriki kwenye majukumu yetu kwa usawa....YES/NO? Tunashiriki kumbukumbu zetu nzuri kwa furaha.,...YES/NO? Kama majibu yako ya YES yanakaribia robo tatu,jua uhusiano wenu ni imara,kama ni chini ya hapo kuna kasoro kidogo,zirekebisheni.Kama YES ni chini ya robo,mnakaribiana kutengana!
 
Gud 4u,kama unasema kweli!
Thanks, mimi katika maisha yangu sipendi kusema sema uwongo...Unless kama kuna sehemu nikisema ukweli utanidhuru, hapo ndo nakuwa muongo kichizi aisay :biggrin:
 
Hapo mm ni no karibia zote.ukiniuliza kwa nini hata sielewi utanisaidiaje?
 
Naona YES zimezidi. Huu uzi umetulia, watu wasiuchukulie juu juu.
 
What is the sensitivity and specificity of this test? Maana sio suala la mtu kuuliza maswali tu bila kupewa nguvu na tafiti za ubora wa hicho kipimo.
 
What is the sensitivity and specificity of this test? Maana sio suala la mtu kuuliza maswali tu bila kupewa nguvu na tafiti za ubora wa hicho kipimo.

Uhusiano wako ndo kipimo!Au uhusiano ni kitu cha kawaida kwako?
 
Back
Top Bottom