Ulianza ukabila, ukaja udini, baadaye tukaambiwa wataleta fujo, baadaye uhaini, itafuata nini??

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Safari hii CCM wamenasa pabaya, wanajaribu bila mafanikio kuziba sauti zinazowaonyesha rangi zao halisi. Mwanzoni tuliambiwa CHADEMA ni chama cha Wachaga, wakashangaa kuona inaungwa mkono zaidi kanda ya ziwa wakajua wakisema ya wasukuma wamekwisha maana hawa ni kipenzi cha wengi, wakaja na CHADEMA ni chama kinachoeneza udini wananchi wakatafakari wakagundua ni uzushi, wakaleta habari za uhaini wakaambiwa waende mahakamani kwani uhaini ni kosa la jinai wakachemsha, sasa wametoka na Chama kinachopewa fedha na mataifa ya nje ili kiiondoe serikali madarakani.

Vyote ni vichekesho maana CCM ndio mabingwa wa kupokea misaada kutoka nje, tuliambiwa 2000 Mugabe alimwaga midollar ya kutosha, tukaambiwa 2005 Ali Hadaiwi naye alimwaga $$$ za kutosha, inawezekana kweli kuna chama kimepokea msaada kutoka kwa wasamaria wanaotaka maendeleo ya nchi hii kama ambavyo wanatoa misaada mingine kuwakomboa masikini wa nchi hii, kama wamevunja sheria yoyote si muwafungulie mashitaka???

Hii serikali inayokubali sheria za nchi zivunjwe ni serikali gani hiii, haifai na inatakiwa kujiondoa yenyewe kabla hatujaiondoa
 
Nyerere alisema UKILA NYAMA YA MTU HUWEZIKUACHA UTAENDELEA TUU

Hapo umenena lakini pia Shabaan Roberts aliwahi kuandika hivi kwenye mashairi yake: Ukweli huvunja milima. Kama Chadema wanasema kweli tupu basi watashinda hizi propaganda za uongo za CCM
 
Ccm akil zao wanazjua wao, wanadhan tu wapumbav kama wanavyofikir, ukwel hauwez kufchka kamwe
 
Back
Top Bottom