Ulemavu na Ombaomba

Rikab Mikail

Member
Jun 7, 2009
16
0
Naomba kuuliza. Je, Mlemavu lazima awe ombaomba?

Kila ninaposimama kwenye mataa za kuongozea magari kwenye barabara za Dar ninakuta walemavu wana omba wakigongagonga madirisha za magari na kunyosha mikono. Je, hii hali inawezekana kubadilishwa/kubadilika? :confused:
 
so long as the national cake is not distributed equally this will go on year in year out and strange enough there is a constitutional guarantee for all citizens of tanzania to get a better life and no one seems to care about them
 
Kuwa mlemavu sio excuse ya kutofanya kazi. Labda tuseme ni ulemavu gani ambao mtu anao. Ni kweli kuna walemavu ambao hata wewe ukiwaangalia unashindwa kujua ni kazi gani hapa duniani anaweza kufanya akapata kipato kama wengine.

Ila kwa tamaa ya pesa, watu wengi wameona ulemavu ni ajira. Hata wale wazima wamekua wanajitia kilema ili nao pia waombe mpaka unashindwa kujua nani wa kusaidiwa na nani anaigiza!

Kwa kiasi fulani, hawa watu wanawadhalilisha walemavu na nashangaa serikali imefumba macho kwenye hili. Pale Ubungo, kuna wakina mama ambao sio hata walemavu, wazima wa afya na wana watoto wao mgongoni wanaomba, ukiwauliza wanasema wana shida - kwani kuwa omba omba ndio solution pekee ya kuondokana na shinda?

Serikali yetu ipo wapi?
 
Huku ni kudhalilisha walemavu.

lakini mimi nasema wengi wao ni wazee na ni tabia ya wagogo toka Dodoma
 
Back
Top Bottom