Ulaji wa Asali na Maumivu ya Tumbo

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Asali inaaminika kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali. Hata hivyi kuna wakati unakula asali halafu unaanza kusikia maumivu. Mathalan, leo asubuhi nimekunywa chai ya rangi ambayo imeungwa na asali badala ya sukari; kitafunio changu kikawa mahindi ya kuchemsha (mindi moja tu. Baada ya muda nikaanza kusikia tumbo linanisumbua. Nakumbuka hali kama hii ilikuwa inawatokea watu kule nyumbani kwetu Kondoa Irangi kwa baadhi ya watu walipokula asali hata bila kula na kitu kingine.

Je hii inaweza kuwa inasababishwa na nini?

Mwenye maelezo tafadhal.
 
Mimi sio mtaalamu ila nakumbuka hata mini kabla sijazoea kula asali mara ya kwanza kula nilisikia tumbo linaniuma ila baada ya kuzoea na siku hizi ndio kama kilaji changu cha kila siku najisikia niko vizuri.

Wataalamu wanashauri kwa kuwa asali ni dawa ya vitu vingi ni vyema mtu akajizoesha kula asali kila siku asubuhi vijiko viwili na maji ya kunywa ya moto kabla hujala kitu chochote hii inasaidi tumbo lako kufanya(digestion) kazi vizuri. Kitu ambacho hata mimi nakubaliana nacho.

Hivyo nafikiria mtu kama hujazoea kula asali na mara unapoanza kula ukasikia maumivu ya tumbo pengine inaweza ikawa ni viashiria kuwa tumbo lako haliko safi kutokana na kula vitu vingi hivyo unaweza ukawa una uchafu tumboni, minyoo n.k. hivyo ile asali inavyoshuka kwa kuwa ni dawa inaenda kutibua hivyo vilivyokuwa vimelala kwa sababu kama mtu unajifuatilia mwenye yale maumivu ya tumbo huwa yanachukua muda mfupi then yanaacha ila utakapoendelea kula asali kila siku hiyo hali ya maumivu utakuta imetoweka ndio kusema kama ni uchafu umesafishwa. na then utajikuta unakuwa ni rafiki mkubwa wa asali hutamani siku ipite hujaonja hata kijiko kimoja.

Jamani haya ni mafikirio yangu tu ila pengine kuna sababu nyingine wajuzi watujuvye.
 
Nashawishika kukubaliana na wewe kwamba maumivu yale ni sehemu ya mchakato wa matibabu kwa sababu jana na leo nimetumia asali ileile asubuhi lakini sijasikia maumivu tena.
 
Natumia asali badala ya sukari ya kwaida kwa sehemu kubwa ya mika 4 iliyopita; napenda kuwashuhudia kuwa nimepunguza matatizo mengi sana niliyokuwa nayapata to the extent naweza kudiriki kusema afya yangu iko stable sana kwa sasa!

Namshukuru aliyenishauri kuitumia na ninawashaurini tujizoeze kuitumia mara kwa mara ikibidi!

Nilifurahi siku moja nilipita mjini Morogoro nikaamua kujipatia chai pale kwa Mama ntilie 1 wa msamvu stand nikakuta kaweka option ya asali kwa wateja wake; nilimsifu sana huyo mama nakumtia moyo awashauri na wenzie!
 
Tatizo kubwa kwa sasa ni hii habari ya kuchemsha Asali. Kwa mara ya kwanza nilikutana na habari hii wakati niliposafiri kwa Garimoshi kwenda Shy. Tulipofika maeneo ya Vijiji vya Tabora nikasikia wauzaji wa asali wakiinadi asali yao kuwa mbichi. Kwa kweli nilishindwa kuwaelewa kwani mimi nilikuwa naifahamu asali kuwa ni asali tu hakuna cha mbichi wala mbivu. Baada ya kuulizia ndo nikaambiwa kuwa huwa wanaichemsha kwa lengo la kutoa nta, na kwa kufanya hivyo huipotezea ubora wake. Sasa kazi ni kuitambua ipi ni mbichi na ipi imechemshwa; yale yale ya bidhaa za Kichina pale unapoenda dukani afu unaambia bidhaa hii nni orijino na kukiangalia nyingine unaambiwa hii ndo orijino zaidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom