Ukweli wa yaliyojiri Arusha-Kesho Star TV

Ama chadema nao wanaichakachua kuweka matukio ambayo hayakuwepo.tutaamini vipi kama hiyo cd ndo hali halisi ktk tukio?
 
Ukweli tutaujua mahakamani sio propaganda nyingine yoyote, alie kaidi amri ya jeshi duniani kokote hukumu yake inaeleweka na imani na mahakama ya tanzania watakuwa seriouse na kesi hii ya kuvuruga amani

Ulikuwa wapi kuwapa ushauri huo kina Mwema na intelejensia yake wakati wanatoa version yao TBC? Bull unatumia mapembe kufikiri?
 
Ukweli tutaujua mahakamani sio propaganda nyingine yoyote, alie kaidi amri ya jeshi duniani kokote hukumu yake inaeleweka na imani na mahakama ya tanzania watakuwa seriouse na kesi hii ya kuvuruga amani

Nipe ushahidi wa hukumu tatu zilizo wahi kutolewa na mahakama za tanzania kuhusu maandamano haramu, ambazo hukumu yake waandamanaji walifungwa au kukutwa na hatia. Kuanzia wakati wa kashkash za mchungaji mtikila, hekaheka za mrema na ungangari wa CUF. Ushahidi huo ndio utakao bainisha ukweli au upotoshaji wa thread yako. (zingatia mahakama za tanzania)
 
Ni vyema mkakumbuka mahakamani mbowe,slaa,lema na wenzao ni watuhumiwa na Andengenye, Mwema na Polisi wao ni mashahidi wa jamhuri. Na upande wa mashtaka(jamhuri) unapaswa kuthibitisha bila shaka yeyote kuwa maandamano ya CDM yalikuwa haramu Hivyo maswali haya ni lazima yapate majibu moja kibali cha maandamano na mkutano kilitolewa au la? kama ilitolewa je kilifutwa au la? Na kama kilifutwa aliyekifuta ana mamlaka hayo kwa mujibu wa sheria. kumbuka aliyefuta maandamano ni mwema na si OCD(sheria ina bainisha mwenye mamlaka ni afisa wa polisi mwenye dhamana ya wilaya ambayo mkutano /maandamano ufanyika ambaye ni OCD).
Tatu je sababu za kuzuia maandamano zilikuwa sahihi? hapo lazima uhalisia wa taarifa za kiinteligensia uthibitishe pasi na shaka yeyote uwepo wa tishio la uvunjifu wa amani endapo maandamano hayo yangefanyika. Nne lazima upande wa mashtaka utoe ushahidi wa kutolewa kwa zuio la maandamano, na kama zuio hilo liliwafikia walengwa ndani ya muda muafaka. na lilitolewa kwa kufuata taratibu sahihi za utendaji wa serikali na jeshi la polisi.
Kwa uelewa wangu mdogo wa sheria mabo hayo niliyoyataja yanapaswa kuthibitishwa na upande wa mashtaka pasi na shaka yeyote ili kuwa tia hatiani watuhumiwa kumbuka ktk kuthibitisha tuhuma any doubt ni advantage kwa mtuhumiwa. Na jambo la msingi ni kuwa haki ya kujieleza na kuonyesha hisia zako ni haki ya kikatiba ( hii ni Advantage ya watuhumiwa) na mkumbuke kesi wameitengeneza polisi na nia na madhumuni ni kuficha aibu ndio maana wakaikimbiza mahakamani haraka kuna uwezekano hata DPP hakushirikisha au alishinikizwa iende mahakamani hivyo utaona jinsi wanasheria wa serikali wanavyoteseka kuthibitisha kosa maana kesi haijaandaliwa kiuchunguzi amini usiamini utasikia kila mara kesi inahairishwa kisa ushahidi hauja kamilika(tuhuma za kupika kuzithibitisha ni kazi kwelikweli)
 
Yaani mi ndo ningekua kikwete nine resign Zamani nipumzike ...maana mojarra haikai mbili haikai

Akimbie kwa nauli ipi mkuu? subiri alipwe Dowans zake ndo maana wakomaa akishalipwa anatambaa Saudia kaiba kura inchi aitawaliki :nono:
 
Back
Top Bottom