Ukweli wa ndoto !.

Maalim Jumar

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
1,259
117
Habari jamvini JF!.
Nimekua nasikia maneno mengi kuhusu ndoto mbali mbali...
Wasomi na wasio wasomi wakijadili hili swala la ndoto.
Nami nimefurahi japo nitoe mchango wangu kuelimisha ni nini maana ya Ndoto na zinz mafungu mangapi?
Naamini tukifahamu hayo itawasaidia wengi kuelewa.
Pia Ndoto na maana au faida zake zimeelezwa kwenye vitabu vitukufu.
Unakaribishwa uweke mchango wako humu au maswali ntajitahidi kujibu vile ntaweza...
Nawakilisha.
 
Ndoto zimegawanyika sehemu tatu:
1-Ndoto walizokua wakiota mitume/manabii. (P.b.u.t)
2-Ndoto zinazootwa na watu wema/waovu.
3-Ndoto zinazooteshwa na Shaytwan(Lucifer).
....kundi la kwanza ndio ndoto ambazo hazihitaji tafsiri(interpretation) hizo huoteshwa mitume hasa kama hawakupata hawakupata fursa ya kuendewa na malaika Jibriil(Gabriel).
....kundi hilo la pili ndio ndoto zote nazoota mimi au wewe na wengine ...hizi hua zinahitaji kutafsiria maana yake. Kwa wale ambao wanafaham taratibu za kutafsiri wanaelewa. Na hapa ndipo patakua muhim katika hoja za watu wengi.
...kundi la tatu mara nyingi huwa hazitafsiriwi maana yake. Ila zinaweka taswira ya muotaji vile alivyo. Kama asubuhi kabla hujaamka uote umeletewa saduku la mali...ilhali hara pesa ya kulipa madeni yako huna.
 
Ungeanza na kutuambia ndoto maana yake nini!
Kila mtu anaota Ndoto.
Pale mwanaadam anapolala usingizi atachoona ndio Ndoto.
Maana halisi ni ujumbe!.
Huo ujumbe utaendana na vile vifungu vitatu nlivyo ainisha hapo awali.
 
Maalim, JE NDOTO ZINAZOOTWA KWA MAOMBI MAALUM YAKIAMBATANA NA DUA, FUNGA, IBADA, SADAKA AU VINGINEVYO ILI DHAMIRA YAKE ITIMIE. Je akiota chochote chenye muelekeo huo wa azma/dhamira yake...je ni aina gani ya ndoto hiyo? Inahitaji tafsiri au!
 
Maalim, JE NDOTO ZINAZOOTWA KWA MAOMBI MAALUM YAKIAMBATANA NA DUA, FUNGA, IBADA, SADAKA AU VINGINEVYO ILI DHAMIRA YAKE ITIMIE. Je akiota chochote chenye muelekeo huo wa azma/dhamira yake...je ni aina gani ya ndoto hiyo? Inahitaji tafsiri au!
Sadaqta!
Ungefafanua mfano unaomba dua au umefunga swaum unataka uote nini?
Mara nyingi dua na swaum huenda pamoja lengo utakua kuna kitu unahitaji ukipate....ukimaliza utalala ili uone imekujibu vipi? Nayo itakua kwenye kundi la pili. Japo kuna ikhtilaf kwenye maombi aina hiyo.....hadi uipate hiyo ndoto. Umenielewa?
 
Ukijua maana ya ndoto yako itakusaidia kutenda mambo yako kwa utaratibu mzuri.
 
Back
Top Bottom